Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amepokea nakala za hati za utambulisho kutoka
kwa mabalozi wateule wa nchi za Finland, Hispania na Canada katika hafla
iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es salaam.
Mabalozi wateule waliowasilisha nakala za Hati za
Utambulisho kwa Mhe. Waziri Mulamula leo
ni Balozi wa Canada Nchini, Mhe. Kyle Nunas, Balozi wa Finland Nchini, Mhe.
Zitting Maria Theresa na Balozi wa Hispania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.
Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti
Mhe. Waziri amewaahidi kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao
kikamilifu hapa nchini na kuwasihi kuendeleza kile ambacho mabalozi
waliowatangulia wamekifanya katika nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya
nchi zao na Tanzania.
Akizungumza baada ya kuwasilisha nakala ya hati
zake kwa Mhe. Waziri, Balozi mteule wa Finland Mhe. Zitting Maria Theresa
aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Finland na kuongeza
kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na
mabadiliko ya Tabia nchi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, masuala ya
jinsia na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake.
Naye Balozi Mteule wa Canada Mhe. Kyle Nunas
amesema Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuibua maeneo mapya
ya ushirikiano yakiwemo biashara na uwekezaji, sekta ya madini,elimu , maji na
ulinzi na usalama.
Naye Balozi Mteule wa Hispani Nchini, Mhe. Jorge
Moragas Sanches amemuahidi Mhe. Waziri kuwa Hispania itaendelea kushirikiana na
Tanzania katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, afya, michezo, maji, elimu
na umeme vijijini ili kuleta tija nchini.
Katika hatua nyingine Balozi Mulamula amekutana na
kuzungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende Malepe.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili jinsi ya kuendelea kushirikiana
kwa kuzingatia makubaliano ambayo nchi hizi mbili ziliingia kwa lengo la
kufungua maeneo zaidi ya ushirikiano kupitia fursa za kujengeana uwezo kati ya
wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini. | Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula jijini Dar Es Salaam
|
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.