Saturday, September 24, 2022

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA AU

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Robert Kahendaguza aliposhiriki katika  Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Robert Kahendaguza akizungumza  katika  Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York tarehe 23/09/2022

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Mussa Faki Mahamat (kushoto ) katika meza kuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York tarehe 23/09/2022

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York wakifuatilia mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa  Jijini New York.


Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula ameuhakikishia Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania iko tayari na itaendelea kushirikiana na jumuiya hizo kushughulikia changamoto za amani na usalama.


Amesema utayari huo wa Tanzania unakwenda sambamba na kufanya mapambano dhidi ya ugaidi wa aina zote lazima uwe kipaumbele katika nchi zote na kutoa wito wa kuanzishwa kwa kamati ya mawaziri  ya kukabiliana na ugaidi kama ilivyokubaliwa wakati wa mkutano wa AU uliofanyika mjini Malabo.
 
Amesema vita dhidi ya ugaidi na vitendo vya kihalifu vinahitaji nguvu ya kushirikiana pamoja kwa ngazi zote kuanzia taasisi, nchi, kanda na taasisi za kimataifa na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuunganisha kazi ya uangalizi ya Umoja wa Afrika  na Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ili kuwa na uratibu wa pamoja.
 
Amezisihi nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kusaini na kuridhia mikataba muhimu kama  Mkataba wa  kuzuia na kupambana na ugaidi; Mkataba wa Umoja wa Afrika wa ushirikiano wa kuvuka mipaka na Mkataba wa Afrika wa  Ulinzi wa Usafiri majini,usalama na maendeleo ili kuimarisha nguvu katika kupambana na ugaidi, vitendo vya kidhalimu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.