Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amewasihi watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kwa ushirikiano mkubwa ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake iliyojiwekea.
Balozi Fatma ametoa maelekezo hayo wakati alipokutana na watumishi wa Ubalozi katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za ubalozi Jijini Doha, Qatar na kuwataka kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, weledi na uaminifu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
"Nawasihi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano pamoja na kuwa wabunifu wa kuitangaza lugha ya Kiswahili, pamoja na Filamu ya Roya Tour, pamoja na vipaumbele vya Serikali hasa katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi," amesema Balozi Fatma.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Bi. Patricia Kiswaga amemhakikishia Balozi Fatma kuwa watafanya kazi kwa umoja, bidii, weledi na ubunifu kwa maslahi mapana ya Taifa.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Kiswaga ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar ni mzuri na unaendelea kuimarika kila wakati.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.