Monday, September 19, 2022

DKT. MPANGO: DIASPORA ENDELEENI KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa alipowasili kwa ajili ya kukutana na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiawa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston (kulia)  wakati wa kikao na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani katiuka hafla iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York



 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi wa Jumuiya ya WanaDiaspora wa Tanzania waishio katika miji ya  New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani, baada ya Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini New York.

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman (kushoto) akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dkt. Elsie Kanza na Mkurugenzi wa Idara ya Multilateral Balozi Kahendaguza na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Balozi Swahiba Mndeme na mtumishi mwingine wa Ubalozi wa New York wakifuatilia mazungumzo ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Diaspora wa Tanzania walioko katika jiji la New York

Baadhi ya washiriki wa wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana na Diaspora wa Tanzania waliopo katika miji ya New York, Connect Cut na New Jesry nchini Marekani na kuwasihi kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Jijini New York alipokutana kwa mazungumzo na viongozi pamoja na wanajumuiya ya wanadiaspora hao Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Mpango amesema kitendo cha wanaDiaspora hao na wengine walioko duniani kote kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kinaendeleza jitihada za serikali za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.
 
''Muendelee kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kwani kufanya hivyo mnachangia maendeleo ya nchi yenu, mnaiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa watu  wake," alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia amewasihi wanadiaspora hao kufuatilia na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa manufaa yao binafsi, ndugu na jamaa na Taifa lao kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango amewataka wanadiaspora hao kuendelea kutafuta na kushawishi wawekezaji wengi kuja nchini na kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini na kuendelea kuisemea vizuri nchi yao ya Tanzania.

Amewapongeza Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa wa uwekezaji hasa kupitia mfuko wa UTT Amis ambapo aliasema kuwa hadi kufikia mwaka 2021 wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wamewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 3.9 za kitanzania katika mfuko huo.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.