Wednesday, September 21, 2022

DKT. MPANGO ASHIRIKI KIKAO CHA DEMOKRASIA UN

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki  kikao cha majadiliano ya  Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika kikao cha majadiliano ya Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

kikao cha majadiliano ya Demokrasia kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa kikiendelea jijini New York

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki  kikao cha majadiliano cha  Ajenda ya Demokrasia jijini New York.

Kikao hicho kiliwakutanisha Wakuu wa Nchi, Serikali na Mashirika ya Kimataifa kimefanyika  kando ya  Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea Jijini New York nchini Marekani kiliandaliwa na Shirika la la Maendeleo  ya Kimataifa la Marekani (USAID).
 
Katika majadiliano hayo , Makamu wa Rais amesema serikali ya Tanzania imeweka mkazo katika mageuzi ya kuimarisha uchumi na utawala wa kidemokrasia kwa kuhakikisha sekta binafsi inashiriki vema katika ujenzi wa taifa pamoja na kushirikiana na wadau wa kimataifa katika kufikia maendeleo.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango yuko nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu HassanNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.