Tuesday, September 13, 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDONESIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele mapema leo tarehe 13/09/2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta. 

Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji. 

Hatua hiyo ya Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo. 
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasili katika Kasri la Merdeka jijini Jakarta ambapo aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.