|
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw.
Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. |
|
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw.

mazungumzo yakiendelea
|
|
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw.
Maurizio Busatti na maafisa walioshiriki mazungumzo hayo katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi. |
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana
na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw.
Maurizio Busatti ambaye amejitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri katika ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika kikao hicho Waziri Mulamula ameipongeza IOM kwa kazi inazofanya nchini
na amemuhakikishia Bw. Busatti kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itaendelea kufanya kazi na Shirika hilo.
Amesema
Shirika hilo (IOM limekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika masuala ya wakimbizi, majanga ya asili na kuongeza kuwa ni matumaini
yake kwamba Bw. Busatti ataendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na
IOM kwa kuzingatia uzoefu wa muda mrefu alionao kwa kufanya kazi kwa muda mrefu
ndani ya shirika hilo.
Balozi
Mulamula ameipongeza IOM kwa kuendelea na shughuli za kuwarejesha nyumbani rai
awa Ethiopia waliokuwa katika magereza nchini na kuongeza kuwa kitendo hicho
kimesaidia Tanzania kukabiliana na msongamano wa watu katika magereza yake.
Ameipongeza
IOM na jitihada zake za kukijengea uwezo kituo cha mafunzo cha maafisa Uhamiaji
Kanda ya Afrika kilichoko ndani ya Kituo cha mafunzo cha Maafisa Uhamiaji cha mjini Moshi ambapo
pia maafisa uhamiaji wa Tanzania wananufaika nacho.
Naye Bw.
Busatti ameishukuru Serikali kwa jinsi inavyoshirikiana na Shirika hilo katika
kutekeleza majukumu yake hapa nchini.
Bw.
Busattia ameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri ambao shirika hilo umekuwa na
Serikali ya Tanzania kwani imekuwa mdau wake mkubwa katika kufanikisha majukumu
yake.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.