Thursday, March 9, 2023
Wednesday, March 8, 2023
TANZANIA, NAMIBIA KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia mkutano huo |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ikifuatilia mkutano huo |
BALOZI MBAROUK AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI DOHA QATAR
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Vallamvelly Muraleedharan pamoja na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Uhusiano wa Jumuiya za Kimataifa Mhe. Michelle Sison, Doha nchini Qatar.
Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi zinazoendelea (LDCs) unaendelea Doha nchini Qatar.
Tuesday, March 7, 2023
DKT. TAX AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na Uingereza na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha na kuendeleza uhusiano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Thursday, March 2, 2023
MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALIMBALI NCHINI AZERBAIJAN
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Azerbaijan, Mhe. Shahin Mustafayev. Mazungumzo hayo yalifanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valders Mesa. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya Isiyofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Baku, Azerbaijan
|
Tuesday, February 28, 2023
BALOZI SHELUKINDO ASISITIZA UMUHIMU WA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akipokea maua mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023. Balozi Shelukindo aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuushika wadhifa huo tarehe 27 Februari 2023.
|
TANZANIA KUANZA SAFARI ZA NDEGE MOJA KWA MOJA HADI SAUDI ARABIA
Tanzania inategemea kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hadi Saudi Arabia ambapo safari ya kwanza kati ya Dar es Salaam na Jeddah inatarajiwa kuanza tarehe 26 Machi 2023.
Hayo yamebainishwa katika mazungumzo ya Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab na kujadili maandalizi ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
Katika mazungumzo yao viongozi hao pia walijadili mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za Tanzania hususan nyama na matunda.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab wakikabidhiana zawadi baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia |
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Mhe. Ali Mwadini akijadiliana jambo na Meneja Mkuu wa Masoko, Kanda ya Kati wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia Bw. Abdulrahman Alabdulwahab katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia |