Monday, March 20, 2023

NCHI ZA SADC ZAWEKA MIKAKATI YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI




Waziri wa Mtangamano wa Kikanda wa DRC na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, Mhe. Didier Mazenga Mukanzu akisoma hotuba yake wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (kushoto) pamoja na Mawaziri wenzake wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuimba nyimbo za Taifa wakati wa hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC

Waheshimiwa Mawaziri na wajumbe wengine wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitenda jambo na Msaidizi wake, Bw. Seif Kamtunda.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya je na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akifuatilia hotuba za viongozi wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitenda jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushurikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Waziri wa Zambia wakati waliposhiriki hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akiongea na mmoja wa Mawaziri walioshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri
Kikundi cha Utamaduni kikiwaburudisha wageni wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
uliofanyika Kinshasa, DRC

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzaia ulioshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri

Waheshimiwa Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi uliofanyika Mkutano wa Baraza la Mawaziri 


 


Saturday, March 18, 2023

KAMPUNI YA MABASI YA CLASSIC COACH KUTANGAZA FILAMU YA THE ROYAL TOUR NCHINI DRC

 




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akibofya batani ili kucheza filamu ya The Royal Tour kwenye Basi la abiria la Kampuni ya Classic Coach ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampuni hiyo kuonesha filamu hiyo kwa abiria wanaotumia mabasi yake. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akitoa maelezo mafupi kwa wageni (hawapo pchani) walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kuonesha filamu ya the Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach. Wengine katika picha, watatu kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said Mshana na watatu kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akielezea kuhusu faida za kuitangaza Filamu ya the Royal Tour, huku akipigiwa makofi na ujumbe aliongozana nao kwenye hafla ya uzinduzi.

Wageni waalikwa walioshiriki hafla ya uzinduzi wa uoneshaji wa filamu ya The Royal Tour katika mabasi ya kampuni ya Classic Coach.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) akimshukuru Mwakilishi wa kampuni ya Classic, Bw. Jonathan kwa uamuzi wao wa kukubali kuonesha filamu ya the Royal Tour kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.

Baadhi ya wageni walioshiriki hafla ya uzinduzi wakiwa kwenye moja ya basi litakalotumika kuoneha filamu ya the Royal Tour

Moja ya basi linalomilikiwa na Kampuni ya Classic litakalotumika kuonesha filamu ya The Royal Tour kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.





Friday, March 17, 2023

NAFASI YA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA HAKI MILIKI DUNIANI (WIPO)

 


TANZANIA, DRC WAJADILI FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) na Wakala wa Kitaifa wa Kukuza Uwekezaji (ANAPI) cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekutana kujadili fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania na DRC.

Akiongea Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Habari wa TIC, Bw. Mafutah Bunini amesema ANAPI imekuja Tanzania kuelezea fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini Kongo DRC.

 “Kama tunavyofahamu Serikali ya Awamu ya Sita imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hivyo ndugu zetu wa DRC wamekuja kuangalia fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania ili waweze kuwekeza zaidi,” alisema Bw. Bunini. 

Bw. Bunini ameongeza kuwa Tanzania imejipanga kushirikiana na DRC kuwekeza katika sekta za kilimo hususan uzalishaji wa mbegu za mafuta, mazao ya chakula kama mchele, mifugo, madini, utalii pamoja na usafirishaji.

Amesema DRC Kongo ina wawekezaji wake Tanzania na ndiyo maana ANAPI imekuja hapa kuhamasisha wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza zaidi nchini Kongo, hivyo uwekezaji na biashara ni wa pande zote mbili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ANAPI, Bw. Anthony Nkinzo Kamole amesema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuna fursa nyingi za uwekezaji hususan katika sekta za madini, usafirishaji, utalii, nishati, afya na viwanda. 

“Tuna makubaliano ya biashara kati yetu (Kongo) na Tanzania na ndiyo maana tumekuja hapa kuelezea fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini kwetu ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania kuwekeza zaidi Kongo,” alisema Bw. Kamole

Pamoja na Mambo mengine, Mkurungenzi Mtendaji wa ANAPI aliongeza kuwa “mazingira ya biashara nchini Kongo ni mazuri na yakuridhisha, kwanza tuna sera ya kulinda uwekezaji, tumeboresha pia taratibu za kujisajili kampuni nchini Kongo, tumepunguza kodi kwa wawekezaji ili kuwawezesha kufanya biashara na uwekezaji katika mazingira mazuri na salama zaidi kuliko ilivyokuwa awali,”.

Septemba, 2022 Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zilikutana katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) na kukubaliana maeneo ya ushirikiano yenye tija ya moja kwa moja kwa nchi hizo na watu wake hasa biashara na uwekezaji.

DRC imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika sekta za miundombinu, nishati, utalii, elimu, afya, huduma za kifedha, biashara, uwekezaji, kilimo, maliasili na ufugaji. Aidha, zinashirikiana na kuungana mkono kwenye masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi kwa pande zote mbili.

 Sehemu ya Wafanyabiashara na wawekezaji wakifuatilia Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na DRC. Kongamano hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Mifumo ya Habari wa TIC, Bw. Mafutah Bunini akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara

Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini, Mhe. Jean-Pierre Massala akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na DRC Jijini Dar es Salaam

Picha ya pamoja 


Thursday, March 16, 2023

University of Ibadan (UI) Nigeria, and University of Dar es Salaam, Tanzania sign Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili.


University of Ibadan (UI) Nigeria, and University of Dar es Salaam, Tanzania sign Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili.

The University of Ibadan and the University of Dar es Salaam have signed a Memorandum of Understanding for teaching Kiswahili language.

The symbolic virtual signing of the document was facilitated by the High Commissioner of Tanzania to Nigeria, H.E. Dr. Benson A. Bana, who set up the virtual meeting between the two universities.

Speaking after the signing event, Dr. Bana said it was part of his Commission's efforts to advance Tanzania/Nigeria bilateral ties.

The MoU will take the form of development of joint research activities; exchange of undergraduate and postgraduate students; exchange of staff on sabbatical basis; mutual assistance in the establishment of new programs; exchange of information and publications; and organization of seminars, colloquia, symposia, conferences and workshops.

The Vice-Chancellors of both universities said they were happy about the MoU, given that both institutions are the oldest public universities in their different countries.

The the two Universities have shared antecedents. The University of Ibadan was established as a college of the University of London in 1948 and became a full-fledged University in 1962. The University of Dar es Salaam was established as a campus of the University of London in 1961 but became a full-fledged University in 1970.

The Vice Chancellor of Dar es Salaam University, Professor William A. L. Anangisye said the understanding will afford both institutions to learn more about each other.

He added he was pleased that the MoU would allow the teaching of Kiswahili, the lingua franca of Tanzania, and one of the official languages of the Organization of African Unity.

The Vice-Chancellor of the University of Ibadan, Professor Kayode O. Adebowale, mni, FAS, was represented at the ceremony by the Deputy Vice-Chancellor, Research Innovation and Strategic Partnerships, Professor Oluyemisi A. Bamgbose, SAN.

Professor Bamgbose stated that mutual understanding had existed between the University of Ibadan and Tanzania long before now.



She recalled that the University of Ibadan in 1976 conferred the Honorary Doctor of Laws on the late President Julius Mwalimu Nyerere in recognition of his contributions to the development of Africa. She said this was an indication that the two countries shared values.

Professor Bamgbose appreciated the efforts of the High Commissioner to strengthen the relationship between the two countries.

The newly signed MoU will lead to the teaching of Kiswahili as an African language in the University of Ibadan's Department of Linguistics and African Languages.

The Head of the Department, Professor Oye Taiwo, assured that necessary steps will be taken to ensure that the course is approved soon by the University of Ibadan Senate
Deputy Vice-Chancellor, Research Innovation and Strategic Partnerships, Professor Oluyemisi A. Bamgbose, SAN at the signing ceremony of Memorandum of Understating (MoU)

A delegation from the University of Ibadan poses in a group photo after the signing event

A delegation from the University of Ibadan poses in a group photo after the signing event

BALOZI SHELUKINDO ATETA NA BALOZI WA UTURUKI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na Uturuki na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu wakati alipomtembelea Balozi Shelukindo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Wednesday, March 15, 2023

MAWAZIRI WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI WASHIRIKI MKUTANO WA PILI WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO

 

Mawaziri wa kisekta wa Serikali za Tanzania na Afrika Kusini wamekutana jijini Pretoria, Afrika kusini kushiriki Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation - BNC) ngazi ya Mawaziri kati ya nchi hizo uliofanyika tarehe 15 Machi 2023.

Mkutano huu wa siku moja ulitanguliwa na mkutano ngazi ya wataalamu uliofanyika tarehe 13 na 14 Machi 2023 ambao pamoja na mambo mengine ulikuwa na jukumu la kuandaa taarifa kwa ajili ya mkutano wa ngazi ya Mawaziri.

Mkutano wa Mawaziri umepitia na utawasilisha taarifa katika itakayojadiliwa na kufanyiwa maamuzi katika mkutano wa Wakuu wa Nchi hizo unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi 2023.

Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri ulifunguliwa kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mwenyekiti mwenza Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor ambao wameongoza ujumbe wa nchi hizo mbili katika mkutano huo.

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Dkt. Tax ameeleza kuwa Mkutano wa Pili wa Tume ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaonesha nia ya dhati ya mataifa hayo ya kuendeleza ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo.

“Mkutano huu unatoa fursa ya kujadili na kuamua masuala ya msingi ya kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya nchi na watu kupitia muingiliano uliopo katika shughuli mbalimbali za kijamii, biashara na uwekezaji” alisema Dkt. Tax

Pia akaeleza mkutano huo wa BNC utaweka msisitizo katika masuala ya ustawi wa jamii wa mataifa hayo mawili pamoja na watu wake.

Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano yenye tija kwa nchi hizo na kupelekea maamuzi yatakayoleta matokeo chanya na kutoa ufumbuzi wa changamoto za wananchi.

Dkt. Tax amesema sekta binafsi ni chachu katika kuendesha uchumi wa nchi, pia ni wadau muhimu kwa sekta za umma hivyo ni jukumu la Serikali kuwezesha upatikanaji wa mazingira mazuri ya biashara ili ziweze kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wa Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Nalendi Pandor ameeleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Afrika kusini umejengwa na historia yenye uhalisia iliyoasisiwa tangu enzi za harakati za kupinga ubaguzi wa rangi pamoja na za ukombozi wa Kusini mwa Afrika.

Ameongeza kuwa Afrika Kusini itaendelea kushirikiana na Tanzania hususan katika shughuli za kijamii, kiuchumi na masuala ya kiutamaduni.

“Napongeza jitihada za mshikamano zilizooneshwa na wafanyabiashara wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania kwa kusaidia madawati 400 katika shule za Wilayani Kongwa na vifaa wezeshi vya usafi katika shule ya miyembeni mwaka 2018” alisema Dkt. Pandor.

Aidha, akaeleza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zina matamanio makubwa ya kukuza uchumi utakaotengeneza ajira na kuondoa umasikini na kujenga usawa wa hali ya kimaisha kwa wananchi wake.

Vilevile, Tanzania na Afrika Kusini zina mtazamo unaofanana katika masuala ya usalama, uchumi na misimamo ya kimaendeleo ya kikanda na kimataifa hivyo, BNC ni sehemu ya jitihada zitakazowezesha kuongezeka kwa miradi ya maendeleo na mshikamano imara utakaopelekea kukuza na kuimarisha ushirikiano uliopo.

Mkutano wa BNC unajadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa na nchi hizo. Sekta hizo ni pamoja na; Siasa na Diplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha na Uchumi, Nishati, Mifugo na Uvuvi, Madini, Habari, Mawasiliano na teknolojia ya mawasiliano, Kilimo, Uchukuzi, Elimu na Mafunzo, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Maji na Misitu, na Afya.

Kwa pamoja viongozi hao walizitaka sekta zilizopo katika maeneo hayo ya ushirikiano kuhakikisha wanatekeleza na kutatua kwa wakati masuala ya kiutendaji ili kuruhusu sekta hizo kustawi kiuchumi na kuyafikiwa kwa wakati malengo ya Wakuu wa Nchi katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini.

Mkutano huu unaenda sambamba na kongamano la biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini litakaalofanyika tarehe 16 Machi 2023 na kuhusisha  maonesho ya huduma na biashara kutoka sekta za umma na sekta binafsi ambapo washiriki wapatao 136 wanatarajiwa kushiriki katika kongamano na maonesho hayo jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kwa pamoja na Mwenyekiti mwenza Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor wamefungua Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini – ngazi ya Mawaziri uliofanyika tarehe 15 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Ujumbe wa Waheshimiwa Mawaziri wa kisekta kutoka Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliofanyika tarehe 15 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Kutoka kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakifuatilia hafla ya ufunguzi katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliofanyika tarehe 15 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz na maafisa kutoka Wizara hiyo wakifuatilia hafla ya ufunguzi katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliofanyika tarehe 15 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.


Picha ya Pamoja Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Dkt. Naledi Pandor na Waheshimiwa Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakati wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini uliofanyika tarehe 15 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.












Monday, March 13, 2023

MAKATIBU WAKUU WA SADC WAKUTANA KINSHASA




Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiwa katika meza ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ngazi ya Makatibu Wakuu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC kinachofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo.
Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC, ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika Kinshasa, Jamhui ya Kidemokrasia ya Congo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda wa DRC ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu, Balozi Songhu Kayumba akisoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho.







 

TANZANIA NA AFRIKA KUSINI KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO

Tanzania na Afrika Kusini zimekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za fedha na uchumi, kilimo, madini, maji, utalii, siasa na diplomasia, mawasiliano na uchukuzi, teknolojia ya habari, uchumi, nishati, elimu, wiwanda, biashara na uwekezaji, ujenzi, utalii, kilimo, uvuvi, afya, elimu na utamaduni.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Bi-National Cooperation) kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika tarehe 13 – 16 Machi 2023 jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Mkutano huu uliofunguliwa katika ngazi ya Maafisa Waandamizi unafanyika tarehe 13 na  14 Machi 2023 pia ni mkutano wa awali kwa ajili ya kuandaa taarifa zitakazopitiwa na kujadiliwa na mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 15 Machi 2023. 

Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini unalenga kujadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika masuala mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa kwanza wa BNC uliofanyika mwezi Mei 2017 jijini Dar es salaam.

Akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini, ngazi ya Maafisa Waandamizi, Balozi Fatma Rajab ameeleza kuwa mkutano huu unatoa nafasi ya kupitia hali halisi ya utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika kikao cha kwanza na kuweka mikakati imara ya kusonga mbele kimaendeleo.

 

 “Kikao hiki kitahusisha majadiliano yatakayowezesha kufikiwa kwa makubaliano katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano ya kisekta yatakayo rasimishwa kwa ajili ya utekelezaji na kuruhusu maeneo mapya ya ushirikiano” alisema Balozi Fatma.

Vilevile, akaeleza kuwa mkutano huu ni muhimu kwakuwa ushirikiano wa nchi zetu umejengwa katika misingi imara iliyopiganiwa kwa jasho na damu tangu enzi za ubaguzi wa rangi na hivyo BNC hiyo ni chachu ya kuimarisha na kuharakisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo yatakayokubaliwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini na Mwenyekiti mwenza za kikao hicho Bw. Zane Dangor, alieleza kuwa BNC inatoa fursa ya kuimarisha ushirikiano hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.

“Jukumu letu ni kuimarisha ushirikiano katika masuala yenye maslahi makubwa kwa mataifa yetu na kufungua fursa ya maeneo mapya ya ushirikiano” alisema Bw. Dangor.

Matarajio ya Wenyeviti wa Mkutano huu ngazi ya Maafisa Waandamizi ni kuhakikisha wajumbe wanawasilisha michango yenye tija ya kisekta katika majadiliano ili kuifikia hatua ya juu ya kimaendeleo kupitia ushirikiano uliopo.

Pia viongozi hao wamesisitiza kuwa Tanzania na Afrika Kusini zinauchukulia kwa upekee ushirikiano huo kwakuwa nchi hizo zina masuala mengi ya kushirikishana kupita uanachama wake katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC na kwa lengo la kujenga uchumi wa kanda hiyo na Afrika kwa ujumla.

Tanzania na Afrika Kusini zilikubaliana kuanzisha Tume ya Marais ya Uchumi (Presidential Economic Commission-PEC) mwaka 2005 na mwaka 2011 nchi hizo zilisaini Tume ya Ushirikiano wa Pamoja (Bi-National Commission) ambayo ilichukuwa nafasi ya PEC.



  

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Namibia, ngazi ya Maafisa Waandamizi, Balozi Fatma Rajab akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023.

Katibu Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini, Bw. Zane Dangor akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab na Katibu Mkuu Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Bw. Zane Dangor wakifafanua juu ya utaratibu wa mkutano huo ambapo walieleza kuwa majadiliano ya mkutano yanafanyika katika makundi manne ambayo ni; Siasa na Diplomasia; Ulinzi na Usalama; Fedha na Uchumi, na Huduma za kijamii.

Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika jijini Pretoria Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (BNC) kati ya Tanzania na Afrika Kusini unaofanyika jijini Pretoria Afrika Kusini tarehe 13 hadi 16 Machi 2023.

 

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MADOLA KUKABILI CHANGAMOTO ZA KIDUNIA

Tanzania imeahidi kushirikiana na Jumuiya ya Madola kukabiliAna na changamoto za kidunia zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, Uviko 19, migogoro, ugaidi na umasikini

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo aliposhiriki maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Balozi Shelukindo amesema licha ya uhusiano wetu na historia ya pamoja kama wanachama wa Jumuiya ya Madola tunaamini kuwa kwa umoja wetu tunaweza kuzikabili changamoto za kidunia kwa urahisi zaidi.

“Kila mmoja wetu akitimiza wajibu wake kwa wakati, itakuwa rahisi kuzikabili changamoto za kidunia hususan mabadiliko ya tabianchi, Uviko 19, migogoro, ugaidi na umasikini,” alisema Balozi Shelukindo

Kwa Upande wake, Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar amesema Jumuiya ya Madola imekuwa na mchango mkubwa kwa Tanzania hususan vijana ambao ndiyo taifa la kesho wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa masomo kwa ngazi mbalimbali, biashara na uwekezaji pamoja na ajira.

Balozi Concar amesema Jumuiya ya Madola imefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikizichukua katika masuala ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora, ulinzi na usalama na utawala wa sheria. 

“Tanzania imeboresha sana masuala ya demokrasia, haki za binadamu na utawala bora, ulinzi na usalama na utawala wa sheria….. mtakumbuka hivi karibuni mikutano ya kisiasa imeruhusiwa pamoja na uhuru wa vyombo vya Habari umeongezwa jambo ambalo linaashiria kukua na kukomaa kwa demokrasia,” alisema Balozi Concar.

Balozi Concar ameongeza kuwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya biashara na uwekezaji nchini na hivyo kuchangia uchumi wa Tanzania kukua. 

Maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yamehudhuriwa pia na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na baadhi ya wanamichezo wa Tanzania walioshiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola.

Maadhimisho yameongozwa na Kauli Mbiu isemayo ‘Kujenga mustakabali endelevu na wenye amani wa pamoja’.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo azungumza na Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba alipowasili katika makazi ya Balozi wa Uingereza Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar akiwasilisha salamu za Jumuiya ya Madola wakati wa maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akiwasilisha hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uingereza hapa Nchini, Mhe. David Concar akichangia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam




Picha ya pamoja


Saturday, March 11, 2023

BALOZI KOMBO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA JAMHURI YA MALTA

Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika Ikulu ya Malta. 

Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Vella viongozi hao walizungumza ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yaliakisi kuimarisha ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa na azma ya nchi ya Malta kuwa daraja baina ya Afrika na Umoja wa Ulaya. 

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walisisitiza suala la kuibua fursa zenye manufaa kwa pande zote mbili katika maeneo ya elimu, utalii, utamaduni, uvuvi, usafiri wa majini, biashara na uwekezaji. 

Uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Malta ulianza mwaka 2015 na tangu wakati huo, juhudi za kukuza uhusiano huo zimekuwa zikifanyika kupitia sekta za elimu, utalii na usafiri wa anga; na kupitia katika majukwaa ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola ambazo nchi zote mbili ni wanachama. 

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta 

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta 

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta, mara baada ya Balozi Kombo kuwasilisha Hati za Utambulisho

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta, mara baada ya Balozi Kombo kuwasilisha Hati za Utambulisho

Rais wa Jamhuri ya Malta, Mheshimiwa Dkt. George Vella katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malta mwenye makazi yake Roma nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika Ikulu ya Malta