Thursday, March 16, 2023

BALOZI SHELUKINDO ATETA NA BALOZI WA UTURUKI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na Uturuki na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo mawili

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehment Gulluoglu wakati alipomtembelea Balozi Shelukindo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es SalaamNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.