Wednesday, October 18, 2023

WATANZANIA WALIOKUWA ISRAEL WAREJEA NYUMBANI

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama nchini humo wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) (wa pili kushoto) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama nchini humo wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo



Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akisalimiana na Bw. Lucas Malaki ambaye ni mmoja wa  vijana wa Kitanzania waliorejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama  zilizoikumba nchini hiyo

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na vijana wa Kitanzania (hawapo pichani ) ambao wamerejeshwa nyumbani na Serikali kutoka nchini Israel kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo, nyuma yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima walipofika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea vijana hao
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akimsikiliza kijana Lucas Malaki aliyerejea nchini kutoka Israel  kufuatia changamoto za kiusalama zilizoikumba nchini hiyo




Watanzania 9 waliokuwa nchini Israel wamerejea nyumbani leo tarehe 18 Oktoba 2023 na kulakiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika mapokezi ya Watanzania hao Naibu Waziri Byabato amesema kurejea nyumbani kwa Watanzania hao kunatokana na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuwarejesha nyumbani raia wake walioko nchini Israel ili waendelee kuwa salama.

 

Amesema Serikali kupitia Ubalozi wake wa nchini Israel iliweka utaratibu wa kuwarejesha Watanzania wote ambao wangetaka kurudi nyumbani na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuwashawishi Watanzania walioko nchini humo ili waone haja ya kurudi nyumbani hadi pale hali itakapotengemaa.

 

Amesema Serikali imefarijika kwa Watanzania hao kuitikia wito wa kuokoa maisha yao na anaamini kuwa Watanzania waliobaki nchini humo busara zao zitawaongoza na kuamua kurejea nyumbani ili wawe salama na kuongeza kuwa Serikali itawarejesha nyumbani watakapokuwa tayari kufanya hivyo.

 

Akizungumza baada ya mapokezi hayo mmoja wa Watanzania hao Bw. Lucas Malaki ameishukuru Serikali kwa kitendo cha kuwarejesha nyumbani na kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya wajisikie fahari kuwa watanzania na kuwaondolea unyonge na kuongeza kuwa wanakichukulia kitendo hicho kuwa ni cha upendo na cha kizalendo na kuahidi kuwa wataendelea kuwa raia wema.

 

Watanzania hao wamerejeshwa nyumbani na Serikali kufuatia kuendelea kuzorota kwa  hali ya amani na usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani tangu kikundi cha HAMAS kilipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba, 2023.


AFRIKA NA NORDIC ZAKUBALIANA KUBORESHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Mawaziri wa nchi za Nordic wakubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji, kubadilishana ujuzi, teknolojia pamoja na kukuza uwekezaji baina ya nchi hizo.

Makubalianao hayo yameafikiwa wakati wa Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers, Algeria ambapo mkutano huo ulianza tarehe 16 – 18 Oktoba 2023.

Akizungumza baada ya makubaliano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Y. Makamba (Mb.) amesema kuwa mkutano huo umekuwa na mazungumzo ya tija kuhusu ushirikiano wa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Afrika na nchi za Nordic, kubadilishana ujuzi, teknolojia pamoja na kukuza uwekezaji. 

“Tumekuwa na mazungumzo yenye tija yanayolenga kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi Afrika na nchi za Nordic, kubadilishana ujuzi, na teknolojia pamoja na kukuza uwekezaji baina ya nchi zetu,” alisema Mhe. Makamba.

Waziri Makamba ameongeza kuwa katika mkutano huo, Mawaziri wa nchi za Afrika na Nordic wamekubaliana kufanya kazi kwa bidii ili kuchochea ongezeko la uwekezaji kati ya nchi hizo.

“Nimepata bahati ya kuwa Mwenyekiti katika mjadala wa uliohusu ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi za Afrika na Nordic na tumekubaliana kuna kazi kubwa ya kufanya kuongeza uwekezaji na biashara kati ya nchi zetu na kuna maazimio yatatoka kuhusu masuala hayo ambayo ndiyo yatatuongoza kuanzia sasa kuhusu nini tunafanya ili nchi yetu ya Tanzania na nchi zetu za Afrika zipate mitaji zaidi, ujuzi zaidi, teknolojia zaidi, na ifanye zaidi biashara na nchi za Nordic,” aliongeza Waziri Makamba. 

Awali akifungua Mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf alisema kuwa Afrika inaendelea kujizatiti kuimarisha zaidi ushirikiano wake na nchi za Nordic kwa maslahi mapana ya pande zote hususan katika vipaumbele kwenye masuala ya amani na usalama, biashara na uwekezaji, na elimu ya ufundi ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi na maarifa.

Akiongea kwa niaba ya Nchi za Nordic, Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark, Mhe. Lars Løkke Rasmussen alisema kuwa Nordic itaendelea kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) na Afrika kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa amani na usalama vinaendelea kudumishwa. 

Mhe. Rasmussen aliongeza kuwa Nordic itaendelea kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama Barani Afrika vinapewa kipaumbele, ufadhili endelevu wa mfuko wa amani na usalama wa Umoja wa Afrika; kuboresha sera zinazohusu maendeleo ya vijana ili waweze kuchangia kwenye maendeleo ya jamii.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umejadilia masuala ya ulinzi na usalama hususan kwenye mapambano dhidi ya ugaidi na mageuzi katika Umoja wa Mataifa; kuweka mikakati ya kuboresha elimu Barani Afrika; kukuza biashara na uwekezaji baina ya pande mbili na umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa ambazo zinahitaji ushirikiano ili kuzitatua.

Mkutano kati ya nchi za Afrika na Nordic ulianza mwaka 2000 ambapo mwaka 2001 Mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Sweden na imekuwa ikifanyika kwa kupokezana kati ya nchi za Nordic na Bara la Afrika.

Imwaka 2019, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 18 kati ya Nordic na Afrika mwaka 2019 ambapo nchi 34 zilishiriki katika mkutano huo.  Tanzania ni moja kati ya marafiki wakubwa wa nchi za Nordic na imekuwa ikishiriki mikutano ya Afrika – Nordic inapokuwa ikifanyika.  Mkutano wa mwaka 2022 kati ya Nchi za Afrika na Nordic ulifanyika mwezi Juni 2022 Helsinki, Finland.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Y. Makamba (Mb.) akifuatilia Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers, Algeria. Mkutano huo ulianza tarehe 16 – 18 Oktoba 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Y. Makamba (Mb.) akifuatilia Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers, Algeria. Mkutano huo ulianza tarehe 16 – 18 Oktoba 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Y. Makamba (Mb.) akizungumza na baadhi ya Mawaziri wa Nchi za Nordic wakati wa Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers, Algeria. Mkutano huo ulianza tarehe 16 – 18 Oktoba 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January ambaye ni mwenyekiti wa mjadala uliohusu ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi za Afrika na Nordic akiongoza kikao wakati wa Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Lauri Tierala. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January ambaye ni mwenyekiti wa mjadala uliohusu ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi za Afrika na Nordic akiongoza kikao wakati wa Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic unaoendelea Jijini Algiers. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Lauri Tierala. 


Monday, October 16, 2023

WAZIRI MAKAMBA AWASILI ALGERIA KUSHIRIKI MKUTANO WA 20 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Y. Makamba (Mb.), amewasili nchini Algeria kushiriki Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 16 – 18 Oktoba 2023, Jijini Algiers, Algeria.

Mara baada ya kuwasili nchini Algeria, Mhe. Makamba alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene Jijini Algiers na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Bw. Lounes Magramane.

Mkutano wa 20 wa nchi za Afrika na Nordic unahusisha nchi tano (5) za Nordic ambazo ni Finland, Sweden, Denmark, Norway na Iceland pamoja na nchi 25 za Afrika ambazo ni marafiki (wenye ushirikiano na Nordic) wa Nordic.

Mkutano kati ya nchi za Afrika na Nordic ulianza mwaka 2000 ambapo mwaka 2001 Mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Sweden na imekuwa ikifanyika kwa kupokezana kati ya nchi za Nordic na Bara la Afrika.

Itakumbukwa kuwa Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa 18 kati ya Nordic na Afrika mwaka 2019 ambapo nchi 34 zilishiriki katika mkutano huo.  

Tanzania ni moja kati ya marafiki wakubwa wa nchi za Nordic na imekuwa ikishiriki mikutano ya Afrika – Nordic inapokuwa ikifanyika.  Mkutano wa mwaka 2022 kati ya Nchi za Afrika na Nordic ulifanyika mwezi Juni 2022 Helsink, nchini Finland.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Bw. Lounes Magramane baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene Jijini Algiers, Algeria kushiriki Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 16 – 18 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Bw. Lounes Magramane baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene Jijini Algiers, Algeria kushiriki Mkutano wa 20 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic utakaofanyika tarehe 16 – 18 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Bw. Lounes Magramane baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene Jijini Algiers, Algeria

Tuesday, October 10, 2023

DKT. MWINYI AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea vitabu kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye

  

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipomtembelea Ikulu Zanzibar


Ujumbe ulioshiriki kikao kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar  kuzungumza naye


Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati -Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima akaiwa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji waliposhiriki kikao kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi aliyemtembelea Ikulu Zanzibar 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) katika picha ya pmoja na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake alipomtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi alipomtembelea Ikulu Zanzibar na kuzungumza naye

 

 

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.
Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake Ikulu Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Mhe. Rais Dkt.Mwinyi amemkaribisha Mhe. Jamal al-Moosawi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa nchi hizo zina historia maalum na kuongeza kuwa kupitia historia hiyo nchi hizo zinaweza kunufaika na fursa za kubadilisha taarifa za kihistoria, uzoefu wa kutunza na kuhifadhi mali kale na kujengeana uwezo katika eneo la uendeshaji wa Makumbusho za Taifa.

“Ni kweli kuwa Tanzania na hasa Zanzibar tuna historia maalum na Oman, tunaweza kutumia kigezo hicho kama fursa za kuendeleza ushirikiano kati yetu katika nyanja tofauti za historia, uhifadhi wa mali kale na ni wahakikishie kuwa Serikali iko tayari kuendeleza ushirikiano wetu,” alisema Dkt . Mwinyi.

Akizungumza katika kikao hicho Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi ameelezea nia ya Serikali ya Oman katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la uhifadhi na ulinzi wa malikale, usimamizi wa Makumbusho za Taifa, uandaaji wa taarifa katika makumbusho na uwasilishaji wa taarifa kwa watalii na wageni mbalimbali na kuiwezesha sekta ya Malikale na Makumbusho za Taifa kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Mhe. Jamal alisema hii ni mara ya kwanza kwa taaisisi yao kuja Tanzania kwa lengo la kujifunza na kuona jinsi historia kati ya Tanzania na Oman ilivyotunzwa na kuhifadhiwa nchini.

Amesema ni matarajio yao kuwa ujio wao utawawezesha kuelewa jinsi wanavyoweza kushirikiana na Tanzania katika eneo hilo la makumbusho na uhifadhi wa malikale na namna wanavyoweza saidia na kuwekeza katika eneo hilo.

Aliongeza kuwa ziara yao hiyo itawawezesha kujua aina ya msaada wanaoweza kutoa ikiwa ni pamoja na kuona maeneo mapya ya ushirikiano ambayo wanaweza kuanzisha na kushirikiana na Tanzania.

Ukiwa nchini ujumbe huo kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman ulishiriki Mkutano wa Kwanza wa Pamoja wa Wataalamu kati ya Tanzania na Oman uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulitembelea Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Makumbusho ya Kijiji cha Makumbusho, Makumbusho ya Kunduchi na Mji Mkongwe wa Bagamoyo na kujionea historia na malikale zilizopo katika makumbusho hayo.

Ukiwa Zanzibar ujumbe huo umekutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Fatma Mbarouk na watendaji wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale.

 

Ujumbe huo pia umetembelea Mji Mkongwe, Makumbusho ya amani na historia ya Mnazi Mmoja, Jumba la Kibweni na Magofu ya Mtoni, Pango la Kuumbi la Jambiani, Makumbusho ya Unguja Kuu na kujifunza na kujionea historia na mali kale zilizopo Zanzibar.


Ujio wa ujumbe huo ni matunda ya ziara zilizofanywa na viongozi wa Tanzania nchini Oman katika miaka ya hivi karibuni ina lenga kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.

 

Ujumbe huo unatarajiwa kuondoka nchini tarehe 12 Oktoba 2023 kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

RAIS DKT. SAMIA AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA INDIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India lililofanyika jijini New Delhi tarehe 10 Oktoba 2023.



Akifungua Kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo “Strong, Togerher ," Mhe. Rais Dkt. Samia amewakaribisha wawekezaji wa India kuja nchini  kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, afya, Tehama,  Utalii na Miundombinu na kuwahakikishia mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara.



Amesema Tanzania imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kurekebisha  baadhi ya sheria za usimamizi wa biashara, kuboresha huduma na miundombinu,  teknolojia pamoja na kuishirikisha kikamilifu  sekta binafsi.

 

Ameongeza kuwa kutokana na jitihada hizo,  viwango vya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India  vimeongezeka mwaka ha ambapo kwa takwimu za  Tanzania za mwaka 2021/2022 India  ni miongoni mwa nchi tano zinazoongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwekeza miradi 630 yenye thamani ya Dola za Marekani 3.7 ambayo imetengeneza ajira kwa watanzania 60,000.



Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa India Mhe.  Shri Piyush Goyal amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali  ya Tanzania katika kuboresha mazingira yabuwekezaji na kwamba ziara ya Mhe. Dkt. Samia inafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kwenye sekta muhimu ikiwemo biashara na uwekezaji.



Awali akizungumza kwenye kongamano hilo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Bi. Angelina Ngalula amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali hizi mbili katika kuboresha mazingira ya uwekezaji  na biashara.



Amesema kutokana na jitihada hizo jukwaa hilo limehudhuriwa na zaidi ya  wafanyabiashara na wawekezaji 250 kutoka  Tanzania na India ambapo kati yao 80 wanatoka Tanzania katika sekta za   Benki, Uchukuzi, Uzalishaji viwandani, TEHAMA,   Burudani na Ubunifu wa mitindo.



Kongamano hilo ambalo limebeba mada isemayo " Nafasi ya Sekta Binafsi katika kuimarisha Biashara kati ya Tanzanaia na India litahitimishwa kwa kupitisha Azimio na Mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha sekta ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan akifungua rasmi Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India lililofanyika jijini New Delhi tarehe 10 Oktoba 2023.Mhe. Rais yupo nchini India kwa zara ya kitaifa ya siku tatu

Mhe. Rais Dkt. Smia akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimweleza jambo wakati wa Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na India lililofanyika India hivi karibuni
Sehemu ya wawekezaji kutoka Inida pamoja  jumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India
Mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na India ukiendelea

Mhe. Rais Dkt. Samia akishuhudia ubadlishanaji wa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India kwenye sekta ya uwekezaji

Mhe. Rais Dkt. Samia akishuhudia ubadlishanaji wa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India kwenye sekta ya biashara