Tuesday, October 31, 2023

UHUSIANO KATI YA MISRI NA ZANZIBAR NI MZURI LICHA YA MISRI KUFUNGA UBALOZI MDOGO ZANZIBAR

Serikali imeeleza leo kwamba, Uhusiano kati ya Misri na Zanzibar umeendelea kukua na kuimarika licha ya Serikali ya Misri kufunga Ubalozi wake mdogo Zanzibar kwenye miaka ya 1990.

Hayo yalielezwa Bungeni leo na Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa akijibu Swali la nyongeza la Mhe. Ali Juma Mohamed, Mbunge wa Shaurimoyo, aliyetaka kujua sababu za nchi ya Misri kufunga Ubalozi wake Mdogo Zanzibar.

Mheshimiwa Naibu Waziri alifahamisha kwamba Misri haikutoa sababu za kufunga Ubalozi wake mdogo Zanzibar. Hata hivyo, alieleza zaidi kuwa pamoja na kufungwa kwa ofisi hizo, mahusiano na ushirikiano kati ya Misri na Zanzibar yameendelea kukua na kuimarika siku hadi siku kupitia Ubalozi wake uliopo Dar es Salaam.

Awali, katika suala lake la msingi, Mhe. Mohamed alitaka kujua idadi ya Balozi ndogo zilizopo Zanzibar, ambapo alijibiwa kuwa hadi kufikia Agosti, 2023, nchi zilizofungua Ofisi ndogo za Ubalozi Zanzibar ni China; India; Msumbiji; Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Aidha, Mheshimiwa Naibu Waziri alieleza kuwa suala la kufungua na kufunga Ubalozi ni suala la kawaida katika ulimwengu wa Kidiplomasia. Alitaja sababu za nchi kufunga Ubalozi kuwa ni pamoja na; Kutetereka au kuharibika kwa mahusiano ya nchi husika; nchi kubadili mwelekeo wa kimaslahi na kistrategia; kukosekana kwa usalama katika nchi husika; na mwisho ni hali ya kiuchumi ambapo nchi hufunga Ubalozi au Konseli Kuu kwa ajili ya kubana matumizi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akijibu swali Bungeni jijini Dodoma 

Waheshimiwa Wabunge wakisikiliza majibu ya swali kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk 


Monday, October 30, 2023

RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI MHESHIMIWA FRANK-WALTER STAINMEIER AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier amewasili nchini leo tarehe 30 Oktoba 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu (3) kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi 1 Novemba 2023, na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akikabidhiwa maua alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba (Mb.) wakati alipompokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimian Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani Mhe. Thomas Terstegen alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na America katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swaiba Mndeme alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier  wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta
kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Y. Makamba na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier wakifurahia ngoma za jadi (hawapo pichani) kwenye hafla ya mapokezi ya Rais huyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiwasalimia Watanzania waliojitokeza kumlaki (hawapo pichani) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA MAPOKEZI 














BALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA

 





Balozi wa Tanzania Nchini Algeria Mhe. Iman Njalikai amekutana na kuzungumza na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha Ukombozi ambaye alikuwa Balozi wa Kwanza wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Noureddine DJoudi .

Mazungumzo na Balozi huyo mwenye historia na kumbukumbu kubwa ya uhusiano wa Algeria na Tanzania yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers.

Mheshimiwa Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na Serikali ya Algeria.

Katika mazungumzo yao Balozi Njalikai alimshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Ubalozi na Mamlaka mbalimbali za Algeria ikiwemo sekta binafsi.


Mhe. Balozi Joudi ameuomba Ubalozi kuimarisha kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini hapo kwa lengo la kuitangaza Lugha hiyo na kuifundisha kwa Wa' Algeria wengi zaidi.

Sunday, October 29, 2023

DMI YAINGIA MKATABA WA KUBADILISHANA UZOEFU NA CHUO CHA ITALY.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italy ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu

MOU hiyo imesainiwa nchini Italy na Dkt.Tumaini Gurumo, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM) Bw. Eugenio Massolo. 

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa makubalino hayo ya miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia” Alisema Dkt. Tumaini.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi.

Kwa upande wake Balozi Kombo amesema kuwa Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilevile Balozi Kombo ametoa wito kwa upande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili izae matunda yanayotarajiwa.

Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijiNI Roma, Italy.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakipongezana baada ya kusaini MOU ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia, tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijini Roma, Italy.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijiNI Roma, Italy.

ZIARA YA KIKAZI YA RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI NCHINI, MHESHIMIWA DKT. FRANK-WALTER STEINMEIER

 







Mkataba wa Euro Milioni 36 kwa Ajili ya Mradi wa Umeme wa Kakono Wasainiwa

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila A. Mkumbo (kushoto) akifurahia baada ya uwekaji saini wa mkataba baina ya EU na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ambapo EU imetoa msaada (grant) kwa Tanzania wa Euro milioni 36 sawa na Shilingi bilioni 95 kwa ajili ya Mradi wa Uzalishaji wa Umeme kwa njia ya Maji wa Kakono, mkoani Kagera wa MW 87.8).

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila A. Mkumbo (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas A. Nyamanga (wa kwanza kulia) wakifutilia majadiliano ya Mkutano wa Global Gateway Forum uliofanyika Brussels, Ubelgiji tarehe 25 na 26 Oktoba 2023 






 

Saturday, October 28, 2023

KAMATI YA BUNGE YA NUU YATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU ARUSHA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipokutana katika ofisi za Mahakama hiyo jijini Arusha

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato  akizungumza kitu alipokutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud (katikati) kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa walipotembelea Mahakama hiyo jijini Arusha


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa (kushoto) akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipotembelea Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato  na wajumbe wengine wa Kamati hiyo katika picha ya pamoja na watendaji wengine wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha



 
 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama imetembelea Mahakama ya Afrika ya Haki za  Binadamu na Watu (AFCHPR) yenye makao yako jijini Arusha na kuzungumza na Rais wa Mahakama hiyo Mhe. Jaji Iman Aboud.
 
Kamati ya NUU pia imetembelea Eneo la Lakilaki jijini Arusha ambako Serikali ya Tanzania inajenga  Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR)
 
Kamati imeipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuigawia  Mahakama hiyo eneo la Lakilaki na kwa kutimiza ahadi ya kujenga Mahakama hiyo.
 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NUU YATEMBELEA AICC



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) akiwa na baadhi wa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo walipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) walipotembelea kituo hicho jijini Arusha kujionea  kinavyotekeleza majukumu yake na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru akiwaelezea Waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) walipotembelea majumba ya Kituo hicho yaliyopo eneo la uzunguni jijini Arusha  walipotembelea kituo hicho  na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa kwanza kulia) akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (wa pili kulia) na baadhi wa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) walipotembelea kituo hicho jijini Arusha



Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru akiwaelezea Waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) walipotembelea majumba ya Kituo hicho yaliyopo eneo la uzunguni jijini Arusha  walipotembelea kituo hicho  na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC


Mwenyekiti wa Kamati ya NUU  Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) akimsikiliza mmoja wa Wabunge na mjumbe wa kamati hiyo akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru  wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha 

Mwenyekiti wa Kamati ya NUU  Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wakwanza kulia) akiwa na  Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa wakimsilikiza wasilisho kutoka AICC  wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa AICC Balozi Begam Taj  akizungumza kuwakaribisha Wajumbe wa Kamatiya NUU walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya NUU wakifatilia majadiliano kati ya Kamati ya NUU na Menejimenti ya AICC wakati  Kamati ya Bunge ya NUU ilipotembelea Kituo hicho jijini Arusha

 

 

        
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imetembelea  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)  na kuzitaka  Taasisi za Umma na Binafsi zinazo daiwa na kituo hicho kulipa madeni yao ili Kituo hicho kiendeshe shughuli zake kwa ufanisi na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuvutia utalii wa Mikutano Nchini.
 
Wito huo umetolewa na 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) alipotembelea AICC na kamati yake kujionea Kituo hicho kinavyotekeleza majukumu yake na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC  jijini Arusha.
 
Akizungumza katika kikao na menejimenti ya AICC, Mhe. Kawawa amezitaka taasisi za umma na zile za binafsi kuhakikisha zinalipa madeni wanayodaiwa na Kituo hicho ili kiweze kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.
 
“Tumemsikia MD wa AICC, Bw. Mafuru akiongelea changamoto mbalimbali zinazoikabili AICC kuwa ni pamoja na madeni ambayo taasisi za umma na za binafsi zinadaiwa, naseme hivi, taasisi zote za umma na za binafsi zilipe madeni ya AICC, ili kituo kiweze kujiendesha kwa ufanisini, kuunga mkono harakati za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuvutia mikutano mikubwa nchini na kutoa mchango stahiki kwa pato la taifa,” alisema Mhe. Kawawa.
 

Amesema kwa AICC kufanya kazi kwa ufanisi ni lazima iondokane na hiyo changamoto ya madeni kwani kulipwa kwa madeni hayo kutaiwezesha kufanya kazi zake kwa tija na ufanisi na hivyo kupata matokeo chanya na kupongeza uendeshaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa na kituo hicho jijini Arusha
 
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, (Mb.) ameishukuru Kamati ya NUU kwa kutembelea AICC na kuitaka Bodi ya AICC kuhakikisha inashughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo yakiwemo madeni ya taasisi mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
 
Mhe. Byabato amewataka AICC wapitie upya na kwa ukamilifu orodha ya madeni wanayodai na kuangalia namna bora ya kukusanya  madeni hayo, kuwakumbusha kwa viambatisho na kuangalia mbinu mpya za namna ya kudai madeni hayo ikiwa ni pamoja na kuangalia kama utoaji wa "offer" za kulipa madeni hayo kama unaweza kusaidiwa kupunguzwa kwa madeni hayo.
 
“ pitieni upya madeni yenu, angalieni njia za kulazimishana pia kama itawezekana, muwe na mikakati mahususi ya wadeni na njia za kulipa madeni, kuna  madhara kwa madeni hayo kuendelea kuonekana katika vitabu vyenu nadhani mnajua kuwa yanaweza sababisha mshindwe kukopesheka pale mtakapotaka kufanya hivyo katika taasisi za kimataifa,” alisisitiza Mhe. Byabato.
 
Awali akizungumza katika kikao na Kamati ya NUU, Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Ephraim Mafuru amesema AICC inaandaa mkakati wa kipaumbele utakaoiwezesha AICC kutekeleza vipaumbele vyake ili iende na wakati na kuhimili ushindani wa soko la Diplomasia ya Mikutano.
 
Amesema AICC pamoja na kufanya shughuli zake katika mazingira ya ushindani, inakabiliwa na changamoto mbalimbali yakiwemo madeni ya muda mrefu ambayo taasisi za serikali na za binafsi hazijailipa AICC kwa muda mrefu sasa.
 
“Kwa sasa AICC inatekeleza shughuli zake kwa kuitangaza nchi katika nyanja ya utalii wa mikutano na matukio na hivyo kuvutia mikutano mingi kuja nchini kwa kuwa vituo vya mikutano duniani hufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine ambao ni wanufaika wa moja kwa moja wageni wanapo kuja nchini kwa ajili ya mikutano,” alisema Bw. Mafuru.
 
Amesema AICC imeamua kuwekeza katika miundombinu ya kisasa na kufanya mabadiliko yanayoendana na wakati kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Kituo wa mwaka 2022/2023-2026/2027 ulioidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi mwezi Juni 2022 na kuanza kutumika rasmi mwezi Julai 2022.  
 
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Saidi Shaib Mussa akizungumza katika kituo hicho ameipongeza Bodi na Menejimenti ya AICC kwa  kutokufanya kazi kwa mazoea na kuwaahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na kufanya nao kazi bega kwa bega ili kufanikisha utendaji wao.

Kamati Hiyo pia imekagua miradi mbalimbali ya uwekezaji ya nyumba za makazi, na hospitali na viwanja vya Kituo hicho na kuonyesha kuridhishwa na usimamizi na uendeshaji wa miradi hiyo.