Mazungumzo yakiendelea |
Friday, November 24, 2023
NAIBU WAZIRI BYABATO AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KOREA
KISWAHILI NYENZO MUHIMU KATIKA KUKUZA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA MALAWI
Serikali ya Tanzania itaendelea kukuza na kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili ili kuimarisha biashara inayovuka mipaka hususan katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwemo Malawi.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe.
Agnes Kayola alipokitembelea Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi cha nchini humo
kwa lengo la kujadiliana na Uongozi wa Chuo hicho kuhusu namna bora ya
kuanzisha ushirikiano baina na taasisi za elimu za Tanzania hususani katika
kufundisha Lugha ya Kiswahili.
Katika mazungumzo yake na Mkuu wa Kitivo cha Elimu, Mawasiliano na masuala ya
Habari wa Chuo hicho, Dkt. Kizito Elijah, Mhe. Balozi Kayola alisema kuwa, upo
mwingiliano mkubwa wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi unaosababisha
mahitaji makubwa ya kujifunza lugha ya Kiswahili ili kurahisisha mawasiliano
katika biashara.
Aliongeza kusema Serikali ya Tanzania itaendelea kusimamia na kutekeleza makubaliano
yote yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini humo mwezi Julai 2023 ikiwemo
masuala ya ufundishaji wa Kiswahili nchini Malawi.
Kwa upande wake, Dkt. Elijah alisema kuwa, Chuo hicho kimepanga kuanzisha Kituo
cha Lugha na kuonesha nia ya kushirikiana na Tanzania hususan Taasisi za Elimu
na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ili kutekeleza azma ya kufundisha
Lugha ya Kiswahili chuoni hapo na kwamba chuo hicho kipo tayari kuanzisha
ushirikiano na Vyuo Vikuu vya Tanzania ikiwa ni pamoja na kubadilishana
wakufunzi na wanafunzi.
Wakati huohuo, Mhe. Balozi Kayola ameitembelea Kampuni ya Kitanzania ya
Bakhresa ambayo imewekeza nchini Malawi tangu mwaka 2003 katika viwanda vya
uzalishaji Unga wa ngano, sabuni za kufulia na inatarajia kukamilisha kiwanda
cha kutengeneza mafuta ya kupikia mwezi Mei 2024.
Akiwa katika Kampuni hiyo Mhe. Balozi Kayola amepongeza uwekezaji mkubwa
uliofanyika na kuwahamasisha kuendelea kukuza wigo wa uwekezaji wa bidhaa
mbalimbali nchini humo kwani mahitaji bado ni makubwa.
Kadhalika, Mhe. Balozi Kayola alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya
Watanzania waishio katika Mkoa Kusini, Malawi ikiwa ni mara yake ya kwanza
tangu ateuliwe kuiwakilisha Tanzania nchini humo.
Katika mazungumzo yake na Jumuiya hiyo aliwaasa kuendelea kuwa wawakilishi
wazuri wa nchi yao kwa kufuata sheria za nchi waliyopo ili kulinda
taswira nzuri ya Tanzania.
Pia alisisitiza umuhimu wa wao kuendelea kujiandikisha kwenye Mfumo wa
Kidigitali wa kuwatambua Diaspora (Diapora Digital Hub) ili iwe rahisi
kuwaunganisha na fursa mbalimbali za biashara, masoko, na uwekezaji zilizopo
nchini pamoja na kurahisisha utoaji wa msaada wakati wa dharura zinazoweza
kuwapata katika nchi wanazoishi.
Mhe. Balozi Kayola alitumia fursa hiyo pia kuwajulisha kuhusu hatua kubwa ya
maendeleo iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.
Rais Dkt. Samia huku akitaja Miradi mikubwa inayokamilishwa ikiwemo Mradi wa
Bwawa la Kufua Umeme la Nyerere, Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR na miradi
mingine kwenye sekta ya Kilimo, Biashara na Uwekezaji.
Vilevile, Mhe. Balozi Kayola aliwaeleza Diapora hao kuwa, Ubalozi upo tayari
kushirikiana nao na kuwasisitiza kuwa huru katika kuwasilisha maoni,
mapendekezo na ushauri kwa manufaa mapana ya Tanzania.
Mkuu
wa Kitivo cha Elimu, Mawasiliano na masuala ya Habari wa Chuo Kikuu cha Biashara na Sayansi cha Malawi, Dkt.
Kizito Elijah wakati wa mkutano kati yake na Balozi Kayola (hayupo pichani) |
Mhe. Balozi Kayola akiagana na Dkt. Elijah mara baada ya kukamilisha mazungumzo baina yao |
Mhe. Balozi Kayola akiendelea kupata maelezo wakati wa ziara yake kwenye moja ya kiwanda cha Kamapuni ya Kitanzania ya Bakhresa ambayo imewekeza nchini Malawi |
|
Mhe. Balozi Kayola akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Bakhresa Malawi Limited akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Mahesh Josyabhatla (wa pili kulia) |
Sehemu ya Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kusini, Malawi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Balozi Kayola (hayupo pichani) |
Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Mkoa wa Kusini Malawi, Bw. Suleiman Marijani akizungumza wakati wa Mkutanoo kati ya Jumuiya hiyo na Balozi Kayola |
RAIS SAMIA ASHIRIKI MAJADILIANO YA JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA USALAMA WA CHAKULA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifafanua jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha |
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Balozi Dkt. Bernard Kibesse akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto akisisitiza jambo kwenye Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula uliofanyika jijini Arusha |
Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula ukiendelea |
Thursday, November 23, 2023
BALOZI NAIMI AWASILISHA HATI KWA RAIS WA AUSTRIA
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria na Katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van Der Belen tarehe 21 Novemba, 2023.
Baada ya kuwasilisha Hati hizo za utambulisho Serikali ya Jamhuri ya Austria ilimuahidi ushirikiano Mhe. Balozi Aziz kwa kipindi chote atakachohudumu katika kituo hicho na kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kuendelea kuimarsiha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria.
Naye Mhe. Balozi Aziz alishukuru na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Austria katika utekelezaji majukumu yake na kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Austria unafikia hatua za juu