Mazungumzo yakiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Panama Mhe. Janaina Tewaney (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba. |
Mazungumzo yakiendelea |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Panama Mhe. Janaina Tewaney (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba. |
Mazungumzo yakiendelea |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezishauri nchi za Afrika kuwa na sera ya lugha za asili ambayo itazingatia mchango wa lugha za asili katika kukuza uchumi.
Ushauri huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati wa kufunga Kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu dhima ya lugha za asili katika kukuza na kujenga Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni.
Katika Hotuba hiyo Dkt. Mwinyi, amesema Bara la Afrika ndilo bara lenye idadi kubwa ya vijana duniani na linategemewa kuwa na nguvu kazi ya dunia hivyo ni lazima kujiandaa kuona Afrika inaandaa nguvu kazi yenye ustadi na maarifa inayosimamia utamaduni na lugha zake za asili.
Dkt. Mwinyi amesema kuwa kuna umuhimu wa kujadili maarifa kupitia lugha za asili yanavyoweza kupatikana na jamii zikaweza kutumia ili kunufaika katika kulinda maliasili na kuendeleza shughuli za uzalishaji kama vile kilimo, uvuvi na utamaduni wa ufinyanzi, ususi na nyenginezo.
“Katika jamii za kiafrika, mfungamano uliopo baina ya lugha za asili na maisha ya kazi, ya ubunifu na ya ugunduzi wa biashara siyo wa kinadharia, bali ni ukweli tunaoishi nao. Kuwapo kwa lugha hizi za asili na hasa matumizi yake ni lazima kuchangie katika maendeleo ya kiuchumi ambayo yatakuwa endelevu,” alisema Dkt. Mwinyi katika hotuba yake.
Kadhalika, Dkt. Mwinyi amewataka wataalamu wa lugha kuongeza ushawishi na mchango katika kuhakikisha Kiswahili kinakuwa daraja muhimu la kukuza diplomasia ya uchumi na kiutamaduni katika ukanda wa Afrika kwa kuzingatia nafasi yake miongoni mwa lugha za asili za kiafrika.
Kongamano hilo limeshirikisha wataalamu wa lugha na watafiti, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, watu mashuhuri na Viongozi Wastaafu na mahiri katika kutumia lugha adhimu ya Kiswahili ikiwa ni miongoni mwa lugha za asili ambayo inazidi kupata mafanikio.
Rais Mwinyi pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia nafasi ya lugha, matumizi ya kidijiti na uchumi wa buluu ambapo alisema kuwa Bara la Afrika lina idadi kubwa ya vijana wanaotarajiwa kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, ugunduzi na matumizi ya vifaa vya kidijiti.
“Tunapaswa kujiuliza ni kwa namna gani wingi wa lugha za asili za kiafrika unavyoweza kutumika kujenga uchumi wa mataifa yetu na kuona kwa vipi tutatumia tofauti za rasilimali tulizonazo na lugha katika kujifunza mifumo ya ikolojia ya bahari ya hindi ili kukuza uchumi wa buluu,” alisema Dkt. Mwinyi.
Katika hatua nyingine Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano ametembelea makumbusho ya Taifa na Kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kutembelea makumbusho ya Taifa, Mhe. Chissano amesema kuna haja ya kuendelea kuhifadhi historia zinazohusu waafrika ili kuonesha ulimwengu juu ya maendeleo yaliyofikiwa na waafrika kabla ya ukoloni.
Mhe. Chissano alikuwa nchini kuhudhuria Kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu dhima ya lugha za asili katika kukuza na kujenga Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni. lililofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 20 na 21 Februari 2024.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano akimsikiliza mmoja kati ya maafisa wa Kijiji cha makumbusho wakati alipotembelea makumbusho hiyo Jijini Dar es salaam |
mazungumzo yakiendelea |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na ujumbe wa wabunge na maseneta kutoka Canada walipokutana naye ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma |
Baadhi ya Wabunge na Maseneta wa Canada wakimsikiliza Naibu Waziri Mbarouk Nassor Mbarouk walipokutana naye ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) amekutana na Ujumbe wa Jumuiya ya Maseneta na Wabunge wa Canada (Africa Parliamentary Association (CAAF) ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma Februari 20, 2024.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Balozi Mbarouk ameelezea kuridhishwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Canada, hususan katika sekta za sekta za elimu, afya, biashara na uwekezaji.
Amesema Serikali ya Canada imekuwa mdau mkubwa katika harakati za kusaidia uboreshwaji na uimarishwaji wa mifumo ya afya nchini kwa kusaidia kuimarisha huduma za afya ya uzazi na vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini.
“Canada imekuwa mdau wetu mkubwa katika sekta ya afya nchini, imetupatia Dola za Canada zipatazo Milioni 15 kupitia mfuko wa bajeti ya afya, msaada huu una maana kubwa kwa Tanzania, unasaidia sana kuboresha sekta ya afya nchini,” alisema
Amesema Canada pia imekuwa ikisaidia Tanzania katika sekta ya elimu ambapo imetoa msaada wa Dola za Canada milioni 53 ambazo kwa kiasi kikubwa zimesaidia kuboresha kiwango cha elimu hasa kwa watoto wa kike nchini.
Kuhusu Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mbarouk amesema kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi kinaendelea kuimarika na kuongeza kwamba takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha miaka 26 kiwango cha mauzo ya Canada kwa Tanzania kimeongezeka kwa asilimia 9.27 kutoka Dola milioni 16.1 za Canada hadi kufikia Dola Milioni 194 za Canada kwa mwaka 2023, na mwaka huo huo, Tanzania iliiuzia Canada bidhaa zenye thamani ya Dola za Canada Milioni 19.9.
Amewahakikishia Wabunge na masenator hao kutoka Canada kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi kutoka Canada kuja nchini kuwekeza mitaji yao hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania ina soko kubwa kutokana na uanachama wake katika jumuiya za kikanda za EAC na SADC.
Naye Kiongozi wa Ujumbe huo wa wabunge na masenata, Bi Brenda Shanahan (MP) amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuwajengea uwezo wabunge hao katika nchi wanazozitembelea na kuona jinsi ambavyo Serikali yao inavyoshirikiana na Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Ujembe huo upo nchini kwa ziara ya kikazi tangu tarehe 18 Februari 2024 na umeshatembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kukutana na Spika wa Bunge hilo ambaye pia ni Rais wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt Tulia Ackson pamoja na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama. Ujumbe huo pia unatarajiwa kwenda Zanzibar tarehe 21 Februari 2024 ambapo pamoja na mambo mengine utakutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Canada hususan baina ya Bunge la Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge la Canada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewasihi washiriki wa Kongamano la lugha za asili kujielekeza kupanga mikakati itakayohakikisha lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za asili zinapata fursa katika uchumi wa kidijiti ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo.
Dkt. Mpango amesema hayo wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni linalofanyika kwa siku mbili (2) tarehe 20 - 21 Februari, 2024 Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais amesema Kongamano hilo linapaswa kuangazia namna ambayo Kiswahili na lugha nyingine za asili za Afrika zitakavyotumika kuendeleza teknolojia za asili, kuchochea uvumbuzi, uwekezaji na kukuza diplomasia.
Aidha, Makamu wa Rais ameongeza kuwa Kongamano hilo linapaswa kusaidia kuonesha fursa zilizopo katika matumizi ya lugha za asili ili kuwafanya vijana kujipatia stadi na maarifa mbalimbali katika kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia ndani na nje ya bara la Afrika.
Makamu wa Rais amesema kupitishwa kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi katika Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kumepanua wigo wa matumizi ya Kiswahili na kuleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kiutamaduni.
“Kongamano hili muhimu linabeba jukumu kubwa la kuibua fursa zaidi na kuendeleza historia ndefu ya Kiswahili katika kujenga uhusiano kati ya watu wa tamaduni, lugha na misingi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii,” alisema Dkt. Mpango.
Amesema Katika muktadha wa ukuaji na maendeleo ya Kiswahili, ni pamoja na kuhifadhi lugha nyingine za asili, sambamba na tamaduni na mifumo yake. Afrika Mashariki na Kati, wafanyabiashara wadogo na wanaoinukia “Wamachinga” wametoa mchango ambao hauna budi kutambuliwa na kuthaminiwa
Dkt. Mpango ameongeza kuwa lipo hitaji la kufanya utafiti wa kina ili kuona jinsi nchi za Kiafrika zinavyoweza kuendeleza mifumo inayozingatia ushiriki wa vijana na makundi kama ya wafanyabiashara waliojiajiri katika diplomasia ya uchumi na kukuza biashara.
Kadhalika, Makamu wa Rais amesema Tanzania imeweka kipaumbele katika kukuza lugha ya Kiswahili, ambapo inalenga kuifanya lugha hiyo kuendelea kuleta umoja, amani na kuvumiliana katika bara zima la Afrika.
Aidha, Dkt. Mpango amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuendelea kushirikiana na Vyuo na Taasisi za nje katika kukuza Kiswahili na kuendeleza diplomasia ya kiutamaduni.
Kongamano hilo limehudhuriwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Joaquim Chissano, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, Mabalozi wa nchi za nje nchini, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. James G. Bwana, Watunga sera, Wafanyabiashara, Wajasiriamali na wenye Viwanda, Viongozi wa Dini, Wanataaluma na Wakuu wa Taasisi za Utafiti, Vijana, Wanawake na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kiraia.
Kongamano limeandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kwazulu-Natal cha Afrika Kusini.
Sehemu ya mabalozi wakifuatilia Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024 |
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni lililofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 20 Februari 2024 |
Mmoja kati ya Washiriki akichangia jambo katika Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni |
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, Mhe.Uhuru Kenyatta akifuatilia mada katika Kongamano la Kimataifa la Dhima ya Lugha za Asili katika kuendeleza Diplomasia ya Kiuchumi na Kiutamaduni |
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.
Samwel Shelukindo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na Ujumbe wa Chuo cha Taifa cha
Ulinzi (NDC) jijini Dodoma, Februari 19, 2024.
Ujumbe
huo unaongozwa na Mkuu wa Chuo cha NDC, Balozi Meja Jenerali Wilbert A. Ibuge,
upo katika ziara ya mafunzo ya kutembelea taasisi mbalimbali kujifunza kuhusu
mchango wa taasisi
hizo katika maendeleo ya nchi hususan kwenye sekta ya ulinzi. Ujumbe huo wenye
jumla ya washiriki 88, unahusisha Wakufunzi 33, na Wanachuo 55 kutoka Tanzania
na mataifa ya Afrika ikiwemo Nigeria, Namibia, Misri, Zambia na Zimbabwe.
Mej.
Gen. Ibuge alieleza kuwa malengo ya chuo hicho ni kuwandaa Maafisa Waandamizi
ndani na nje ya nchi kutoka
vyombo vya Usalama na Watumishi wa Umma katika nyanja ya Usalama na Stratejia. Wakati wa ziara hiyo,
ujumbe huo umeshiriki kwenye mjadala kuhusu Umuhimu wa Kuimarisha usalama wa
jamii zinazoishi mipakani kwa ajili ya usalama endelevu wa Taifa (Enhancing Border
Community Security for Sustainable National Security).
Ujumbe
huo umepokea wasilisho kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, ambapo Balozi Dkt. Shelukindo alielezea majukumu ya Wizara hususan
katika kuhamasisha usalama mipakani. Majukumu hayo yanahusisha uratibu wa
mikutano ya ujirani mwema na Tume za Kudumu za Pamoja za Ushirikiano (JPCs),
Vituo Vya Utoaji Huduma Kwa Pamoja Mipakani (OSBPs), na kuratibu itifaki za
kikanda na kimataifa.
Mwanachuo akijitambulisha |
Mwanachuo akijitambulisha
|
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akijibu maswali mbalimbali yayoulizwa na wanachuo wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi |
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza wakati wa kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi |
Mwanachuo akiuliza swali baada ya kusikiliza wasilisho kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Mhandisi Abdillah Mataka akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Vituo vya Pamoja vya Mipakani |
Mwakilishi kutoka Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Amani Mwatonoka akifafanua masuala ya usalama katika mipaka wakati wa kikao baina ya kikao baina ya uongozi wa Wizara na ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi
|
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Mej. Gen. Wilbert Ibuge akitoa zawadi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo baada ya ujumbe wa chuo hicho kufanya ziara ya mafunzo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma. |