Monday, March 4, 2024

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE ASHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA KUDUMU YA MAKATIBU WAKUU WA SADC


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.

Kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Kamati ya Fedha tarehe 6 Machi, 2024 ambapo kwa pamoja vikao hivyo ni maandalizi ya Baraza la Mawaziri litakalofanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2024 jijini Luanda, Angola.

Aidha, pamoja na mambo mengine vikao hivi vya awali vitapokea na kujadili taarifa zifuatazo: Tathmini ya utekelezaji wa maamuzi ya Mikutano iliyopita, Hatua iliyofikiwa katika kugharamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC wa 2020–2030, Taarifa  ya Kamati ya Fedha, Taarifa ya Kamati ya Rasilimali Watu na Utawala, Hatua iliyofikiwa katika kutafsiri nyaraka muhimu za SADC kwa lugha ya Kiswahili na nyinginezo.

Kauli mbiu ya Baraza la Mawaziri la mwaka huu ni ‘’Rasilimali Watu na Fedha: Nyenzo muhimu kwa ukuaji Endelevu wa Viwanda katika Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”.


      Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.

       Meza kuu ikiongoza majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024. Katikati ni Katibu Mtendaji wa SADC, Bw. Elias Magosi na kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Angele  Makombo N’tumba

   Ujumbe kutoka Eswatin ukifuatilia Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Kikao kikiendelea.

     Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa SADC wanaoshiriki Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 4 – 5 Machi, 2024.







WAZIRI MAKAMBA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE UJERUMANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani. Uhusiano baina ya Tanzania na Ujerumani ni ya kihistoria na yanaonekana katika sekta za utalii, elimu, afya, utamaduni, biashara na uwekezaji pamoja na ushirikiano kupitia miji dada (Twin sister city relations).

Mhe. Keul aliwasili nchini tarehe 29 Februari 2024 kwa ziara ya kikazi ya siku nne (4) ambapo amehitimisha ziara yake nchini leo tarehe 04 Machi, 2024. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayehusika na Afrika, Mhe. Katja Keul, kikiendelea jijini Dar es Salaam




Friday, March 1, 2024

WAZIRI KEUL AZINDUA KITABU CHA MAISHA NA TAMADUNI ZA KICHAGA KILICHOANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI.

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (kulia) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata wakizindua  kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 01 Machi 2024.

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

 

 

 Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata akimkabidhi nakala ya kitabu mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Naomi Zegezege katika hafla ya kuzindua kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta (katikati) aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa  kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili iliyofanyika Old Moshi mkoani Kilimanjaro



Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili



Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo  Dkt. Resani Mnata , Balozi wa Tanzania Ujerumani (wa pili kulia) wakitoa heshima katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani wakati wa utawala wao
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akiweka shada la maua katika kaburi la Mangi Meli aliyeuawa na wakoloni wa kijerumani  wakati wa utawala wao



wananchi wa kabila la Kichaga wakicheza ngoma za asili wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili

 

 

 

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul ameshiriki uzinduzi wa kitabu kinachoelezea maisha na tamaduni za kabila la kichaga kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

 

Wakati wa uzinduzi ambao umefanyika katika kigango cha Kidia,  Old Moshi, imeelezwa kuwa kitabu hicho ambacho kimetafsiri kazi ya mwandishi mchungaji Bruno Gutmann, kinalenga kutambua utumishi wa mchungaji huyo raia wa Ujerumani ambaye aliishi eneo hilo kwa miaka 28 na kushirikiana na wananchi wa maeneo hayo huku akieneza injili.

 

 

Kitabu hicho ni miongoni mwa vitabu 400 vilivyoandikwa kwa lugha ya Kijerumani na mchungaji huyo ambapo mpaka sasa vitabu vitano vimeandikwa kwa  lugha nyingine ikiwemo kichaga na kiswahili.

 

Uzinduzi huo pia umeshuhudiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mhe. Kısare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassan Mwamweta na Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Resani Mnata.

 

Naibu Waziri Keul yuko nchini kwa ziara ya siku nne ya kikazi kuanzia tarehe 29 Februari hadi Machi 4 2024.

TANZANIA NA ETHIOPIA ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA ZA KILIMO, NISHATI NA UTAMADUNI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia la Ethiopia zimesaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za kilimo, nishati na utamaduni katika haflabiliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 01 Machi 2023.

Utiaji saini huo ambao umeshuhudiwa na Viongozi Wakuu  wa Nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali ni matokeo chanya ya ziara ya Mhe. Dkt. Abiy ambaye yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu. 

Kwa upande wa Tanzania, makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na kwa upande wa Serikali ya Ethiopia makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo, Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie.

Hati za Makubaliano zilizosainiwa na  Mhe. Makamba ni Hati ya Ushirikiano katika sekta ya Kilimo ambayo itaanzisha ushirikiano katika utafiti wa mbegu za ngano, kubadilishana uzoefu katika teknolojia ya kilimo, kilimo cha umwagiliaji, kuhudumia mazao baada ya mavuno, kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao na Kilimo cha biashara.

Pia, amesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kuhusu Biashara ya Umeme katika utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA). Hati hii imeanzisha ushirikiano katika usambazaji, biashara ya umeme na kuanzisha jukwaa la majadiliano la kuwezesha na kuanzisha biashara ya umeme utokanao na vyanzo vya maji.

Aidha, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Sanaa na Utamaduni ambapo hati hii itaanzisha ushirikiano wa pamoja katika kuendeleza sekta ya Sanaa na utamaduni ikiwemo kushirikiana katika  matamasha ya kitamaduni,  utafiti, filamu, kuongeza ujuzi kwa wadau wa sekta hiyo na   kuandaa maonesho ya Sanaa.

Tanzania na Ethiopia zinashirikiana katika sekta za usafiri wa anga, nishati, Kilimo, mifugo, uhamiaji, biashara na uwekezaji, elimu, ulinzi na usalama.

    Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Ethiopia wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za kilimo na nishati kulia ni Mhe. January Makamba (Mb.) na kushoto Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie akisainiIkulu jijini Dar es Salaam tarehe 1 Machi, 2024..

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiaopia, Mhe.  Balozi Taye Atseke Selassie wakisaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya Sanaa na Utamaduni Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 1 Machi, 2024.








NAIBU WAZIRI WA MAMBO NJE UJERUMANI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul (aliyebeba begi mngongoni) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya America na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Naomi Zegezege  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Kisare Makore (kuli) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) tarehe 29 Februari, 2024.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul akizungumza na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda (wa pili) kulia na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta ( wa pili kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA)  tarehe 29 Februari, 2024

Mazungumzo yakiendelea katika chumba cha kupumzikia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)

 

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Katja Keul amewasili nchini tarehe 29 Februari, 2024. Mhe. Keul yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku Nne.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Keul amelakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kisare Makore, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Hassan Mwamweta na viongozi wengine wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akiwa nchini Mhe. Keul atatembelea Hospitali ya KCMC, kuzuru kaburi la Mangi Meli na kutembelea Parish ya kidia ambako atahudhuria sherehe za kukumbuka maisha ya kazi za mwandishi wa Ujerumani mchungaji Bruno Gutmann aliyeishi eneo hilo kwa miaka 28 na kuzindua kitabu cha maisha ya kiutamaduni ya wachaga kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili.

Mhe. Keul pia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Ziara ya Mhe. Keul pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pia inalenga kuendelea kuimarisha Uhusiano na ushirikiano Kati ya Tanzania na Ujerumani.

Thursday, February 29, 2024

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ATUA NCHINI KWA ZIARA YA KITAIFA YA SIKU TATU

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali amewasili nchini leo tarehe 29 Februari 2024 kuanza ziara yake ya  kitaifa ya siku tatu.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Waziri Mkuu Abiy amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba.

Mhe. Dkt. Abiy atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 01 Machi 2024.

Pamoja na mambo mengine ziara ya Waziri Mkuu Abiy inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafirishaji kwa njia ya anga, nishati, kilimo na mifugo, biashara na uwekezaji na Ushirikiano katika sekta za elimu, uhamiaji, na ulinzi na usalama 

Ziara hiyo ambayo itakamilika tarehe 02 Machi 2024 inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Matukio katika picha:

Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali akishuka kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali mara baada ya kuwasili Tanzania kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Shamrashamra wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Shamrashamra wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Dkt. Abiy Ahmed Ali nchini Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.



Wednesday, February 28, 2024

TANZANIA NA URUSI KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI



Tanzania na Urusi zimesisitiza kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa maslahi ya pande zote kupitia ushirikiano wa kidiplomasia ulioanzishwa tangu mwaka 1961.

Msisitizo huo umetolewa katika mazungumzo kati ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Februari 28, 2024. 

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika ufuatiliaji wa masuala ya uchumi, biashara, uwekezaji na masuala ya kibinadamu yaliyojadiliwa wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali Urusi – Afrika uliofanyika nchini Urusi mwaka 2023.

Aidha, wamejadili juu ya utaratibu mpya wa kuanzishwa kwa mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na Afrika unaotarajiwa kufanyika nchini Urusi mwezi Oktoba mwaka 2024 ambao utaishirikisha Sekretarieti ya Umoja wa Afrika kama sehemu ya marafiki waalikwa wa Urusi.

Kadhalika, mkutano huo utaongeza nafasi kwa Nchi za Afrika kujadili utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubaliwa na Serikali zao katika nyakati tofauti, sambamba na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za kimkakati.

Akiainisha maeneo ya kimkakati, Mhe. Mbarouk ameeleza kuwa Tanzania ina nia ya dhati ya kuimarisha sekta ya utalii, hivyo ni wakati sahihi wa kuangalia namna bora ya kuhuisha mifumo mbalimbali inayowezesha kuongeza idadi ya watalii na huduma nyingine za kitalii.

Naye Mhe. Avetisyan ameeleza kuwa Urusi imejipanga kuendeleza ushirikiano katika sekta ya utalii kwa kutoa mafunzo kwa kampuni za kitalii na watoa huduma za hoteli ambazo zitaenda sambamba na utangazaji wa filamu ya “Tanzania the Royal Tour”.

Pia Mhe. Balozi  Andrey Avetisyan ameeleza kuwa Urusi inaunga mkono jitihada za kutangaza utalii ambapo inafanya utaratibu kuliwezesha Shirika la Utangazaji la Urusi la “Russia Today” kuja nchini kuandaa makala za runinga zitakazorushwa nchini Urusi kwa lengo la kuendelea kuhamasisha utalii na utamaduni kwa pande zote mbili.

Vilevile viongozi hao wamejadili juu ya umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya elimu pamoja na kuendelea kutoa hamasa kufuatia fursa za ufadhili za masomo ya muda mrefu na mfupi zinazotolewa na Serikali ya Urusi kwa Watanzania


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 28 Februari, 2024.

Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan akieleza juu ya masuala mbalimbali ya ufuatiliaji yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa Urusi - Afrika uliofanyika jijini Moscow, Urusi mwaka 2023.

Maafisa kutoka Ubalozi wa Urusi walioambatana na Mhe. Avetisyan wakifatilia mazungumzo.

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea

Balozi Mbarouk akiagana na Mhe. Avetisyan.

 

Monday, February 26, 2024

WIZARA YAAHIDI KUBORESHA,KUIMARISHA MICHEZO

Ikiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya mbio zilizojipatia umaarufu kuliko mbio za nyikani, "Kili Marathon 2024", Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Balozi Dkt. Samwel Shelukindo umewapongeza wanariadha wa Wizara walioshiriki mbio hizo na kuahidi kuboresha mazingira ya michezo wizarani.

Akiongea na wanamichezo hao jana mjini Moshi, baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kili Marathon 2024, Dkt. Shelukindo alisema  kuwa michezo ni afya, hivyo watumishi wanapaswa kujituma kufanya mazoezi mara kwa mara siyo tu kwa ajili ya kuimarisha afya zao bali kuwawezesha pia kushiriki michezo mbalimbali ndani na Nje ya nchi.

"Natambua kuwa ndani ya Wizara yetu kuna watumishi wenye vipaji tofauti, nawasihi pamoja na ufinyu wa muda mlionao mjitahidi kufanya mazoezi ili muweze kumudu ushindani wa michezo mbalimbali na kuipaisha Wizara yetu ndani na Nje," alisema Dkt. Shelukindo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi aliwapa hamasa wanamichezo ya kuongeza idadi ya michezo wizarani ili kupanua wigo wa watumish kushiriki na kuitaja michezo hiyo kuwa ni pamoja na mpira wa kikapu, mpira wa tenesi, michezo ya Jadi na ndondi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Said Shaibu Mussa aliwataka wanamichezo wa Wizara kuendelea kujituma kwa bidii na kuwa na nidhamu ya mazoezi ili kuwawezesha kushinda michezo wanayoshiriki na kuipeperusha bendera ya Wizara vizuri kwenye kila mashindano wanayoshiriki ikiwa pamoja na kuwahimiza kuandaa bonanza za michezo yatakayoshirikisha wadau tofauti ili kuimarisha mahusiano, kukuza diplomasia ya michezo hatimaye kutangaza Wizara.

Awali akiongea katika kikao cha Viongozi na wanamichezo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo Wizarani (Nje sports Club), Bw. Ismail  Hamidu Abdallah aliushukuru Uongozi wa Wizara kwa kuwawezesha na kuwapa motisha wakati wote wanaposhiriki katika michezo mbalimbali.

"Tunawashukuru Viongozi wetu kwa kutuwezesha wanamichezo, kwa kweli kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwenu tunaahidi kuendelea kujituma kwa bidii katika michezo na kuipaisha vyema bendera ya Wizara," amesema Bw. Ismail

Wanamichezo wa Wizara wamegawanyika katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete kwa wanawake, volleyball, mchezo wa kuvuta kamba pamoja na riadha.

Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo Wizarani (Nje sports Club), Bw. Ismail  Hamidu Abdallah akizungumza wakati wa kikao kilichowakutanaisha Viongozi wa Wizara na wanamichezo wake, mjini Moshi jana jioni


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akizungumza wakati wa kikao baina ya viongozi wa Wizara na wanamichezo jana, mjini Moshi. Kulia (mwenye Tshirt nyeusi) ni Katibu Mkuu Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifuatiwa na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Wengine ni wanamichezo wa Wizara. 

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizarani, Bi. Ester Masigo akizungumza wakati wa kikao