Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda akihutubia kwenye uzinduzi wa utekelezaji wa Mpango wa Ushirikiano kati ya sekta binafsi na wakulima wadogo wa zao la kahawa uliohusisha Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa ushirikiano wa Wizara ya Kilimo, Misitu na Uvuvi ya Japan (MAFF) na sekta binafsi chini ya makampuni makubwa ya Japan, Septemba 20, 2024. |
Sunday, September 22, 2024
TANZANIA NCHI YA MFANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA BINAFSI JAPAN NA WAKULIMA WADOGO WA KAHAWA UNAOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO YA KILIMO (IFAD)
Friday, September 20, 2024
NJE - SPORTS Netiboli YAANZA VIZURI SHIMIWI, YAIBAMIZA RAS LINDI
Timu ya netiboli ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje - Sports) imeanza kwa kishindo Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) baada ya kuitandika bila huruma Timu ya Ras Lindi kwa magoli 39 -16.
Kama wahenga wasemavyo Nyota njema huonekana asubui, katika mchezo huo nyota ya Nje - Sports Netiboli ilianza kuangaza tangu kipenga cha mwamuzi wa mchezo kilivyopulizwa, ikionyesha ustadi wao wa hali ya juu.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Kapteni wa Netiboli Nje – Sport Bi. Faraja Kessy, amesema ushindi huo umetokana na maandalizi mazuri ya muda mrefu, hata hivyo mchezo ulikuwa na ushindani Mkubwa sana lakini tumeibuka na Ushindi Mnono.
"Hakika tunafuraha sana kwa kuanza vizuri katika mchezo wetu wa kwanza wa netiboli. Na matarajio yetu ni kuendelea kufanya vyemza zaidi na kuweza kuibuka washindi katika Michezo hii ya SHIMIWI”.
Vilevile, Bi. Faraja Kessy ameushukuru Uongozi na menejimenti ya Wizara kwa ujumla kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele kutoa hamasa kwa wanamichezo na kuahidi kuendelea kufanya vyema katika michezo iliyobakia katika kundi letu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Michezo Nje – Sports, Bw. Ismail Abdallah ameendelea kuwapongeza na kuwapa hamasa zaidi wana michezo woote. “Kwakweli leo Mambo yako mazuri nifuraha sana kuona tokea asubui tunapata ushindi tuu”.
Kesho Tarehe 21 Septemba, 2024 Nje – Sports wanawake wanatarajia kurusha karata yao ya pili ambapo watamenyana na Mahakama, kwa upande wa Mpira wa Miguu Nje – Sports wanashuka dimbani kucheza mchezo wao wa kwanza ambao watachuana na Utumishi.
Nifuraha kweli kweli. |
Thursday, September 19, 2024
NJE - SPORTS YAJIGAMBA KUFANYA VYEMA KWENYE MASHINDANO YA SHIMIWI - MOROGORO
Ratiba ya makundi katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoanza kufanyika mkoani Morogoro imetolewa hadharani, huku Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Wanaume (Nje-Sports) inatarajia kurusha karata yake ya kwanza tarehe 21 Septemba, 2024 kwa Kuvaana na Timu ya Ras Mara.
Mwenyekiti wa Nje - Sports Bw. Ismail Abdallah amesema kuwa katika mpira wa miguu, timu ya Nje Sports imepangwa kundi G pamoja na timu za Utumishi, Wizara ya Ujenzi, Ras Mara na Ras Lindi.
Ameeleza pia kuwa timu ya Nje – Sports Kamba (Ke) imepangwa katika kundi B na itapepetana na timu za Hazina, Kilimo na Ras Shinyanga, huku mpira wa Pete ikipangwa kundi H na itaumana na Mahakama, Maadili, na Ras Lindi.
Kwa upande wa Kocha wa Nje – Sports, Bw. Shabani Maganga amesema vijana wote wapo salama na wapo tayari kupambana katika mashindano hayo ili kuibuka na ushindi kwenye kila mchezo kutokana na ubora wa timu waliyonayo.
Leo jioni tarehe 19 Septemba, 2024, Nje Sports imeendelea kufanya mazoezi mepesi ya kujiandaa na mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kesho tarehe 19 Septemba, 2024.
Nje - Sports inayoshiriki katika michezo mbalimbali mwaka huu, ikiwemo Mpira wa Miguu Wanaume, Kamba wanawake, Mpira wa Pete, Bao, Karata, iliwasili mkoani Morogoro jumatatu tarehe 16 Septemba, 2024 na kuzua gumzo kwenye viunga na mitaa mbalimbali ya mjini Morogoro (Mji kasoro Bahari).
Wednesday, September 18, 2024
Balozi Shelukindo aongoza Kikao na Sekretarieti ya SADC
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, ameiongoza timu ya Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-ORGAN) katika siku ya pili ya kikao na Sekretarieti ya SADC.
Kikao hicho kilichoratibiwa na Bw. Terry Rose, Afisa Mkuu Kamati ya Siasa na Diplomasia ya SADC kimejikita katika kujadili masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa kamati hiyo na majukumu yake ndani ya kanda ikiwemo uangalizi wa uchaguzi kwa nchi zinazotarajia kufanya uchaguzi. Nchi hizo ni pamoja na Jamhuri ya Msumbiji, Botswana, Namibia na Mauritius chini ya Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC (SEOMs) na Baraza la masuala ya Uchaguzi la SADC (SEAC). Aidha, Kikao hicho kimejadili masuala mengine ikiwemo utekelezaji wa maamuzi yanayohusu siasa na diplomasia katika Kanda, sera na mikakati ya siasa na diplomasia pamoja na mifumo ya usuluhishi na kuzuia migogoro ili kuimarisha demokrasia na ushirikiano kati ya Nchi Wanachama kupitia Baraza la Usuluhishi (MRG) na Jopo la Wazee (PoE). |
Thursday, September 12, 2024
Monday, September 9, 2024
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amwakalisha Rais Samia kwenye ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi za Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezitaka Mamlaka za Udhibiti na Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi, maadili na uwajibikaji ili kuleta ufanisi uliokusudiwa.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi za Afrika Mashariki na uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) lililofanyika Septemba 9, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) cha jijini Arusha.
Mhe.Dkt. Biteko amesema Serikali inatambua kuwa fedha nyingi zinazotengwa kwenye bajeti yake kila mwaka zimekuwa zikitumika kwenye ununuzi wa umma na kuongeza kuwa Serikali imekuwa makini kuhakikisha fedha hizo zinapata usimamizi makini.
“Naomba Wizara ya Fedha mlisimamie hili na haya ni maelekezo ya Mhe. Rais. Majukwaa yaliyofanyika yote yametilia mkazo maadili, weledi, uwazi na uwajibikaji kwani bila ya maadili wananchi hawawezi kupata huduma, pia fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya wananchi kupata huduma zinaamriwa na kundi hili na kama hatuna taasisi imara za ugavi na ununuzi hatutapata matokeo tarajiwa na hivyo umasikini utaongezeka,” amesema Dkt. Biteko.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Dkt. Leonada Mwagike ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia kwa kufanya maboresho makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma na hivyo kuleta tija na kuongeza uwajibikaji ili kupata thamani halisi ya fedha zinazotumika.
Hafla ya ufunguzi wa Jukwaa hilo la 16 la Ununuzi wa Umma kwa Nchi za Afrika Mashariki na uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), umehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia maswala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Shaibu Mussa.
Jukwaa hilo la Ununuzi wa Umma kwa nchi za Afrika Mashariki na uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) linafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa AICC, jijini Arusha.
Saturday, September 7, 2024
RAIS SAMIA AWAHIMIZA DIASPORA KUWEKEZA NCHINI
Thursday, September 5, 2024
CHINA KUTOA USD 50 BILIONI KUSAIDIA MAENDELEO AFRIKA
Wednesday, September 4, 2024
HATI YA MAKUBALIANO YA KUBORESHA RELI YA TAZARA YASAINIWA
RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA CHINA
Katika mazungumzo hayo Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping ameutaja uhusiano wa Tanzania na China kuwa ni wa mfano barani Afrika.
Mheshimiwa Rais Samia yupo nchini China kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC)