Wednesday, October 30, 2024

WANANCHI WA BOTSWANA WAPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU

 

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya SADC (SEOM) Mhe. Mizengo  akiwa na wajumbe wa SEOM wakiangalia moja ya sanduku la kuwekea karatasi za kupigia kura  katika kituo cha Taasisi ya sayansi ya Afya alipotembelea kituo hicho kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza jijini Gaborone tarehe 30 Oktoba, 2024


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya SADC (SEOM) Mhe. Mizengo  akiwa katika chumba cha kupigia kura akiangalia zoezi hilo lilivyoendelea  katika kituo cha kupigia kura alipotembelea kituo hicho jijini Gaborone tarehe 30 Oktoba, 2024

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana wa SADC( SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiangalia mmoja wa wapiga kura wenye uhitaji maalum akipokea karatasi ya kupigia kura huku asaidiwa na mmoja wa watu waliokuwa katika kituo hicho kutekeleza haki yake katika moja ya kituo cha kupiga kura alipotembelea  kuangalia zoezi linaendaje katika Uchaguzi Mkuu wa Botswana  tarehe 30 Oktoba, 2024

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Mhe. Pinda akisalimiana na Rais wa zamani wa Botswana Mhe. Festus Mogae alipokutana naye katika kituo cha kupigia kura alipotembelea kituo hicho kuangalia upigaji kura unavyoendeshwa  tarehe 30 Oktoba, 2024

Wananchi wa Botswana wakiwa nje ya kituo cha kupigia kura wakisubiri kuingia ndani ya  kituo hicho kupiga kura zao kuchagua wabunge na wenyeviti wa mabaraza ya serikali za mitaa katika uchaguzi mkuu wa Botswana uliofanyika tarehe 30 Oktoba, 2024

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi uchaguzi Mkuu ya SADC (SEOM) Mhe. Mizengo  akiwa na wajumbe wa SEOM wakiwa nje ya kituo cha kupiga kura baada ya kuangalia zoezi la kupiga kura lilivyokuwa likiendelea

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiwa na   Rais wa zamani wa Nigeria na  Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan walipokutana katika moja ya kituo cha kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na  

 Rais wa zamani wa Nigeria na  Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa walipokutana katika moja ya kituo cha kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024

Rais wa zamani wa Nigeria na  Mkuu wa Misheni ya uangalizi ya Umoja wa Afrika (AU EOM) Mhe. Goodluck Jonathan (katikati) akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi Uchaguzi Mkuu wa Botswana wa SADC (SEOM) Mhe. Mizengo Pinda (kulia) walipokutana katika moja ya kituo cha kupigia kura jijini Gaborone Botswana tarehe 30 Oktoba, 2024





















Wananchi wa Botswana leo tarehe 30 Oktoba 2024 wamepiga kura kuchagua wabunge watakaounda Bunge la 13 la nchi hiyo na wenyeviti wa Serikali za mitaa ambao wataongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na timu yake wametembelea vituo vitatu vya kupigia kura katika jiji la Gaborone na vituo viwili katika kijiji cha   Mochudi kujionea hali ya upigaji kura inavyoendelea.

Jumla ya Viti 61 vya ubunge na vinagombewa na wagombea kutoka vyama vinne vya siasa vya Botswana Democratic Party (BDP); Umbrella for Democratic Change (UDC); Botswana Congress Party (BCP) na Botswana Patriotic Front (BPF) ambapo Viti 609 vya mabaraza ya Serikali za mitaa vinagombewa na vyama mbalimbali vya siasa na wagombea binafsi ambao wamekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo (IEC).

Uchaguzi mkuu wa Botswana umeshuhudiwa na waangalizi wa kimataifa kutoka wa Misheni za Umoja wa Afrika (AUEOM) iliyoongozwa na Rais wa Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Goodluck Jonathan, Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Madola iliyoongozwa na Mhe. Gideon Moi, na Jukwaa la Tume za Uchaguzi kutoka nchi za SADC lililoongozwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Mhe. Jaji Jacob Mwambegele.  

Sambamba na hilo, uchaguzi huo umeshuhudiwa na Ubalozi wa Marekani, Japan, Indonesia, Namibia na waangilizi kutoka katika taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya siasa kutoka nchini humo.

Misheni hizo zimewapongeza wananchi wa Botswana kwa kuendesha shughuli za uchaguzi kwa amani na usalama katika siku ya uchaguzi mkuu ambapo waangalizi hao wameshuhudia idadi kubwa ya wapiga kura ikiwa imejitokeza kupiga kura katika hali ya amani na usalama katika jiji la Gaborone.

Kwa mujibu wa utaratibu wa uchaguzi nchini humo chama kitakachopata zaidi ya viti 31 vya Bunge ndicho kitakachotoa Rais ambaye ataunda Serikali itakayoongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

MAFANIKIO YA RAIS SAMIA KATIKA SEKTA YA AFYA YALETA HAMASA KWENYE MKUTANO WA MERCK FOUNDATION


Mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya yamewavutia wabia wa maendeleo katika sekta hiyo kuwekeza zaidi nchini, ili kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya na kukuza maendeleo ya Taifa. 

Hayo jamejili leo tarehe 29 Oktoba 2024 kwenye Mkutao wa 11 wa Taasisi ya Merck Foundation Africa Asia Luminary unaoendelea katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam ambao umefunguliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia.

Mkutano huo uliofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza umewakutanisha wadau wa Afya, Wenza wa Marais kutoka Mataifa 15 ya Afrika na Asia, Wawakilishi kutoka taasisi za kimataifa, Wanadiplomasia, waandishi wa habari na Wanataaluma mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kujadili na kutafuta suluhu dhidi ya changamoto mbalimbali za afya na kijamii zinazokabili bara la Afrika na Asia. 

Wenza hao 15 wa Marais wanatoka; Zanzibar, Burundi, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Ghana, Liberia, São Tomé and Príncipe, Malawi, Maldives, Zimbabwe, Msumbiji, Cabo Verde na Gambia. 

Akifungua mkutano Rais Samia amesema Serikali imefanya maboresha makubwa katika sekta ya afya ikiwemo uboreshaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya ikijumuisha ongezeko la vituo vya afya, vifaa tiba na kuimarika kwa huduma bora za afya za mama na mtoto.

“Nikiwa kama Mwanamke na Mama nimefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wadau katika kuboresha mifumo ya matibabu na utoaji wa elimu kwa umma ili kupiga vita ongezeko la magojwa katika jamii ikiwemo magonjwa yasiyo ambukiza” Alisema Mhe. Rais Samia. 

Rais Samia ameeleza kuwa juhudi hizo zilizofanywa na Serikali zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya ikiwemo kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na upatikanaji wa huduma bora za afya katika jamii. 

Aidha Rais Samia ameishukuru Taasisi ya Merck Foundation kwa kufadhili miradi mbalimbali inayochangia kuboresha huduma za afya kwa mwanawake na kutoa mafunzo stahiki kwa watumishi katika sekta ya afya hatua ambayo imewezesha kuimarisha sekta za hiyo kwa nchi za Afrika na Asia. 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Dkt. Rasha Kelej amemwelezea Rais Samia kuwa ni Kiongozi mahiri Mwanamke na mwenye ushawishi duniani kutokana juhudi zake za kuibua na kutetea agenda zinazowezesha kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kitaifa na kimatiafa. 

“Tumefarijika na kuvutiwa na namna Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha sekta ya afya, elimu, kuwezesha wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia. Hii imetupa hamasa kubwa ya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutanua uwigo wa huduma zetu hapa nchini ili kuhakikisha jamii ya Tanzania inapata maendeleo endelevu.” Alisema Dkt. Rash 

Awali Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawanake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameeleza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana. Amebainisha kuwa mazingira hayo yamechangiwa na Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023, uanzishwaji wa Programu madhubuti za Elimu kwa Wasichana na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kupitia mikopo na mafunzo ya ujuzi wa biashara. 

Mkutano huo wa siku mbili wa Merck Foundation ambao unatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 30 Oktoba 2024 umehudhuriwa na washiriki takriban 6000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2024.
Sehemu ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliokuwa ukiendelea katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2024.
Mkutano ukiendelea
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb.) akisalimiana na wageni mbalimbali kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam
Mwenza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Mama Mariam Mwinyi akifurahia jambo kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wenza wa Wakuu wa nchi mbalimbali Barani Afrika wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliokuwa ukiendelea katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Merck Foundation Dkt. Rasha Kelej akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.



Mwanza wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Mama Mbonimpaye Mpango kwenye Mkutano wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Mama Rebecca Victoria Akufo-Addo akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Mama Rachel Ruto akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Maldives Mhe. Mama Sajidha Mohamed akiwasalimia washiriki wa Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

Tuesday, October 29, 2024

RAIS SAMIA WATAKIA HERI WANANCHI WA BOTSWANA KATIKA UCHAGUZI WA TAREHE 30 OKTOBA, 2024

 TAARIFA YA MHESHIMIWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, NA MWENYEKITI WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC - ORGAN) KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA JAMHURI YA BOTSWANA TAREHE 30 OKTOBA, 2024.

 


 

Sunday, October 27, 2024

MHE. PINDA , SEOM WAKUTANA NA MACHIFU WA BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

 

 

 

Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa akizungumza na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

 Baadhi ya Machifu wa Botswana wakifuatilia kikao chao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

mmoja wa Machifu wa Botswana akizungumza  kikao cha machifu  na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

 Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative Bw.  Gaontebale Mokgosi akizungumza  kikao cha machifu  na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative Bw.  Gaontebale Mokgosi akizungumza  kikao cha machifu  na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024


Baadhi ya Machifu wa Botswana katika picha ya pamoja na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024




Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chifu Gaborone wa kabila la Batlokwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa huku Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda akiwaangalia walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative Bw.  Gaontebale Mokgosi (wapili kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda na ujumbe wake (hawako pichani) walipokutana jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba, 2024

 

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na machifu kutoka koo mbalimbali za nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 27 Oktoba 2024 ikiwa ni sehemu ya vikao ambavyo SEOM imekuwa ikifanya na wadau mbalimbali wa uchaguzi nchini humo.

 

Mhe. Pinda ametumia kikao hicho kuwajulisha machifu hao kuhusiana na kazi ya uangalizi wa uchaguzi mkuu wa Botswana kuanzia maandalizi, mwenendo wake na jinsi mambo yalivyo wakati huu wa uchaguzi ikiwa ni kutekeleza jukumu la Uangalizi kwa kuzingatia misingi na miongozo ya uchaguzi wa kidemokrasia iliyowekwa na SADC.

 

Aliwaambia machifu hao kuwa SEOM imekuwa ikikutana na wadau mbalimbali na  kuzungumza nao moja kwa moja na hivyo kupata picha halisi ya jinsi mwenendo na maandalizi ya uchaguzi huo yalivyo na kuongeza kuwa SEOM imepeleka waangalizi wake katika majimbo yote ya uchaguzi ili kuangalia hali inavyokwenda, itakavyokuwa siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

 

Akizungumza katika kikao hicho Kiongozi wa Machifu wa Botswana Chief Gaborone toka kabila la Batlokwa alisema wao kama machifu wana jukumu la kuhakikisha koo zao hazigawanyiki licha ya kuwa wananchi wao ni wafuasi wa vyama vya siasa na kwa kufanya hivyo  amani na usalama vitaendelea kuwepo katika maeneo yao.

 

Alisema wao wakiwa viongozi wa kimila na kijadi nchini humo wana wajibu wa kuwahimiza wananchi kushiriki katika michakato ya siasa ili waweze kuchagua viongozi wa kisiasa ambao wataongoza nchi kwa kipindi husika.

 

Amesema wao sio wanasiasa ila wanashirikiana na viongozi serikali kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika shughuli za siasa kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo akitolea mfano wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Botswana ilivyowafuata na kuwajulisha juu ya juu ya kufanyika kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura na kuwaomba kuwasaidia kufikisha ujumbe huo wa uandikishaji wapiga kura kwa wananchi kwenye maeneo yao.

 

Naye Chifu Lotlamoreng kutoka kabila la Barolong amesema kama chifu akitaka kujihusisha moja kwa moja na masuala ya siasa ni lazima aondoke katika kazi ya uchifu ili aweze kuwa huru kujihussiha na masuala ya siasa nchini humo.

 

Wamesema machifu hawajazuiwa kugombea nafasi za siasa ila wanatakiwa wajue kuwa ukiamua kugombea na kushiriki kama mgombea unatakiwa kuondoka katika ofisi ya chifu ili kuepuka mgogoro wa maslahi na sheria Sheria ya Machifu ya mwaka 2008 ambayo inawatambua machifu na Ofisi zao nchini Botswana.

 

Ameongeza kuwa katiba ya Botswana pia inatambua Ofisi ya Machifu na inawatambua machifu hao ambo wako zaidi ya 500 wakiwamo machifu wananwake ambao wanakaribia 100.

Katika mkutano mwingine, SEOM ilikutana na Kiongozi wa wa Chama cha Real Alternative Bw.  Gaontebale Mokgosi ambaye alionyesha wasiwasi kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo ambayo yamefanywa na Tume Huru ya Uchaguzi (IEC), akitaja kuchelewa kwa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura kama mfano wa mandalizi duni ya uchaguzi huo na wanadhani kuwa IEC haiko tayari kuendesha uchaguzi huru na wa na haki.

Chama hicho kilisisitiza umuhimu wa kuongeza utoaji wa elimu ya wapiga kura na kupendekeza kuwa IEC inapaswa kushirikiana kwa karibu na vyama vya siasa nchini Botswana ili kuhamasisha watu wengi zaidi kushiriki zoezi la kuandikisha wapiga kura na kujitokeza kupiga kura. Pia walisisitiza umuhimu wa ofisi ya ushirikiano wa vyama vya kisiasa kutakiwa kufanya kazi zaidi mwaka huu wa uchaguzi kinyume na ilivyokuwa kwakuwa ofisi hiyo ina jukumu muhimu la kuunganisha IEC, vyama vya kisiasa, na raia kwa ujumla.

 


MHE. PINDA AKUTANA NA JUMUIYA YA WANADIPLOMASIA WANAOWAKILISHA NCHI ZAO BOTSWANA


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, na ujumbe wake katika  kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, na ujumbe wake (kulia) katika  kikao na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (Kushoto) akiwa na Mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutiliamkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa Angola nchini Botswana Mhe. Beatriz Morais (kushoto) akiwa na mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutilia mkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Balozi wa Tanzania nchini Botswana Mhe. James Bwana (Kushoto) akiwa na Mabalozi wenzake wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana wakifutiliamkutano wao na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, katika picha ya Pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana baada ya mkutano kati ya SEOM na Jumuiya ya wanadisplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024 uliolenga kusikiliza maoni na mtazamo wa Mabalozi kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Botswana unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024.


Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Botswana, Mhe. Howard Van Vranken, baada ya mkutano kati ya SEOM na Jumuiya ya wanadisplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana uliofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024 ambao ulilenga kusikiliza maoni na mtazamo wa Mabalozi kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi mkuu wa Botswana unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Oktoba 2024.

 

Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao nchini Botswana katika kikao kilichofanyika jijini Gaborone tarehe 26 Oktoba 2024.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Pinda amewaarifu wanadiplomasia hao juu ya majukumu ya SEOM  katika kutekeleza jukumu la Uangalizi kama lilivyokasimiwa na SADC na kusisitiza kuwa SEOM inaifanya kazi hiyo kwa kuhakikisha nchi husika inazingatia na kufuata misingi na miongozo ya uchaguzi wa kidemokrasia ya SADC.

Ameeleza kuwa SEOM imekutana na wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya ratiba za misheni hiyo kusikiliza na kuzungumza moja kwa moja na wadau wa uchaguzi huo kupata picha halisi ya jinsi mwenendo na maandalizi ya uchaguzi huo unavyokwenda.

Amesema SEOM imekuwa ikiangalia jinsi mwenendo, mipango na utaratibu wa uchaguzi huo unavyoendeshwakwa, kuangalia kama elimu kwa wapiga kura imetolewa vya kutosha, kama inaendelea kutolewa kwa wadau wote wa uchaguzi huo na kama kumekuwa na ushirikishwaji kwa wadau wote wa uchaguzi nchini humo na hivyo kuwa na uelewa wa pamoja kuhusiana na uchaguzi mkuu wa Botswana uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba,2024.

Amesema SEOM imepeleka waangalizi wake katika majimbo yote ya uchaguzi ili kuangalia hali inavyokwenda , itakavyokuwa siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi na watakuwa na mikutano na watu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusikiliza na kupata maoni ili kuhakikisha kazi yao ya uangalizi inakwenda vizuri

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mabalozi hao na Balozi wa Jamhuri ya Angola Mheshimiwa Beatriz Morais ameishukuru SEOM kwa kufikiria kukutana na mabalozi kama moja ya wadau wa uchaguzi wa Botswana ili kusikiliza mtazamo wao kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi na kuwapongeza wananchi wa Botswana kwa hali ya utulivu waliyonayo na hivyo kuwa na amani na usalama katika maeneo yote.

Naye Balozi wa Ufaransa nchini Botswana amepongeza hali ya amani na utulivu iliyoko nchini Botswana wakati huu wakielekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa ni jambo la msingi na la mfano kwa nchi za Afrika na nyinginezo.

Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Mhe. James Bwana amepongeza Serikali ya Botswana kwa kuruhusu na kuwakaribisha waangalizi wa uchaguzi nchini humo na kuwa tayari kushirikiana nao na kuwapongeza wananchi wa Botswana kwa utulivu waliounesha katika kipindi hiki na kuwatakia kila la heri katika uchaguzi mkuu ujao.

SEOM pia imekutana na viongozi wa vyama vya siasa vya  BPF, BMD na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Botswana. Vyama vya siasa katika mikutano yao wameelezea kutokuridhishwa kwao na mwenendo wa uchaguzi huo huku wakisema kumekuwa na uhaba wa karatasi za kupigia kura hali ambayo inawatia mashaka juu ya uchaguzi huo kufanyika kwa uhuru na kwa haki na kuongeza kuwa kitendo cha kuchelewa kutangazwa mapema kwa tarehe ya uchaguzi kumevifanya vyama vya upinzani nchini humo kutokuwa na maandalizi mazuri ya uchaguzi huo.

Chama cha BPF kimesema wanaamini kuwa matokeo ya kurudiwa kwa kura za awali zilizohussisha Diaspora, vyombo vya ulinzi na usalama na majimbo matatu zitaongeza matumaini kwa wananchi na hivyo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.

Nayo MISA Botswana amesema taasisi yao imekuwa ikijishughulisha na utoaji wa elimu kwa waandishi wa Habari juu ya kuandaa na kuripoti taarifa za uchaguzi ila wanaelewa kuwa wnachama wao wanakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa taarifa zinazotolewa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii ambazo hazizingatii misingi na maadili ya uandishi wa habari.