Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahaya akisalimiana na Bw. Screedharan |
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Omar Mjenga akisalimiana na Bw. Screedharan |
Mhe. Suluhu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ndege hiyo itakayoanzisha safari zake moja kwa moja kutokea Dar es salaam mpaka Dubai |
Makamu Mkuu Bw. Screedhana (wakwanza kulia), wa kwanza kushoto Balozi Mdogo Mhe. Mjenga na (katikati) ni Bw. Riyaz Jamal wakimsikiliza Mhe. Waziri alipokuwa akizungumza. |
Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza Bw. Screedharan alipokuwa akizungumza |
Sehemu ya wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Mdogo. |
Picha ya pamoja |
Picha na Reginald Philip
==============================================================
Na Reginald Philip
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu (Mb.) ameupongeza Uongozi wa Shirika la Flydubai la Dubai kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya Dubai na Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar kwa gharama nafuu.
Akizindua huduma hiyo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, jijini Dar es Salaam, Jumatano tarehe 22 Oktoba, 2014, Mhe. Suluhu alimwambia Makamu Mkuu wa Shirika la Flydubai, Bw. Sudhir Sreedharan, kuwa kuja kwao Tanzania kutafungua njia za kiuchumi na nchi nyingine za Kiafrika.
Alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo pia kutatoa fursa ya ajira kwa watanzania, na akawahimiza wananchi kuchangamkia fursa hizo.
Shirika hilo, ambalo ndege zake zina bei nafuu- kutokea Dar es salaam kwenda dubai na kurudi (DSM-DXD-DSM) kwa bei ya dola za Kimarekani 399 tu (budget Airline) litafanya safari zake kati ya Dar es salaam, KIA na Zanzibar. Baadae, shirika hilo litaongeza safari zao kutokea Mbeya kuelekea Dubail.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyoandaliwa na shirika la Flydubai kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Mhe. Suluhu aliipongeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa kuratibu uanzishwaji wa safari za bei nafuu kupitia kwa Balozi Mdogo wa Tanzania nchini Dubai, Mhe. Omar Mjenga, ambaye alihudhuria hafla ya uzinduzi.
Baada ya Dar es Salaam, hafla nyingine ya uzinduzi ilifanyika Zanzibar baadaye hiyo jana, Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
-Mwisho-