Tuesday, June 23, 2020

PROF. KABUDI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI LA SADC



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel (wa kwanza kushoto) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ijinia Isack Kamwelwe (katikati) wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC  unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa  Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa  Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amefungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC na kuzitaka nchi wanachama kushirikiana na kuchukua hatua zinazotekelezeka katika kukabiliana na madhara yatokanayo na mlipuko wa janga la Virusi vya Corona.
 
Amesema changamoto zitokanazo na ugonjwa wa COVID 19 zipo wazi na zinazikabili nchi zote hivyo hazina budi kuungana na kutafuta suluhisho la pamoja ili  kunusuru uchumi na athari nyingine za kijamii.


Prof. Kabudi amesema ili kupata suluhisho la kudumu dhidi ya janga hilo Nchi za SADC  ni vyema zikashirikiana na Jumuiya nyingine za kikanda kama EAC na COMESA ili kuwa na miongozo na viwango vya pamoja katika kuendesha shughuli za usafirishaji wa binadamu, bidhaa na huduma huku hatua za kujikinga zikuichukuliwa. 


Amesema ni muhimu kwa nchi za SADC  kuzingatia miongozo ya wataalamu wa afya wakati zikiendesha biashara na usafirishaji wa bidhaa na huduma ili kulinda uchumi na kuondoa umasikini huku zikikabiliana na ueneaji wa janga la Corona.


Mkutano wa Baraza la Mawaziri umejadili utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Mawaziri dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, kupokea taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Wataalamu ya SADC ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC uliofanyika tarehe 05 Juni 2020 na upendeleo utakaotolewa na India kwa nchi za SADC zitakaponunua dawa, vifaa kinga na vifaa tiba kwa ajili ya COVID 19.


Mkutano pia umepitia na kujadili Mwongozo wa Kikanda wa Urazinishaji (harmonization) na uwezeshaji wa shughuli za usafirishaji ndani ya SADC pamoja na masuala ya uratibu, usimamizi na uangalizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara katika vituo vya kuingilia, ukaguzi dhidi ya Virusi vya Corona vinavyotambuliwa na SADC na namna ya kuendeleza shughuli za biashara wakati huu wa janga la CORONA ili kunusuru uchumi na kupunguza umasikini ndani ya jumuiya.


Mkutano huo umekutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Uchukuzi, Utalii na Afya kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


MKUTANO WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC WAANZA DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akifungua kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa waandamizi/ Makatibu Wakuu wa SADC kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongoza Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa waandamizi/ Makatibu Wakuu wa SADC katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Mabula Mchembe (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nziku (kulia) na Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa waandamizi/ Makatibu Wakuu wa SADC kinachofanyika jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa waandamizi/ Makatibu Wakuu wa SADC wakifuatilia kikao hicho.



Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam  tarehe 23 Juni, 2020.

Mkutano huo umeanza kwa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
  
Mkutano wa Baraza la Mawaziri utajadili utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Mawaziri dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, kupokea taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Wataalamu ya SADC ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC uliofanyika tarehe 05 Juni 2020 na upendeleo utakaotolewa na India kwa nchi za SADC zitakaponunua dawa, vifaa kinga na vifaa tiba kwa ajili ya COVID 19.

Mkutano pia utapitia na kujadili Mwongozo wa Kikanda wa Urazinishaji (harmonization) na uwezeshaji wa shughuli za usafirishaji ndani ya SADC pamoja na masuala ya uratibu, usimamizi na uangalizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara katika vituo vya kuingilia, ukaguzi dhidi ya Virusi vya Corona vinavyotambuliwa na SADC na namna ya kuendeleza shughuli za biashara wakati huu wa janga la CORONA ili kunusuru uchumi na kupunguza umasikini ndani ya jumuiya.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na unakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Uchukuzi, Utalii na Afya kutoka nchi 16 wanachamawa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Monday, June 22, 2020

BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC KUKUTANA KWA DHARURA 23 JUNI 2020

Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika tarehe 23 Juni, 2020 kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela, mkutano huo utatanguliwa na kikao cha Kamati ya Kudumu ya Maafisa Waandamizi/ Makatibu Wakuu chini ya uenyekiti wa Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kufuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri utajadili utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Mawaziri dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, kupokea taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Wataalamu ya SADC ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Afya ya SADC uliofanyika tarehe 05 Juni 2020 na upendeleo utakaotolewa na India kwa nchi za SADC zitakaponunua dawa, vifaa kinga na vifaa tiba kwa ajili ya COVID 19.
Mkutano pia utapitia na kujadili Mwongozo wa Kikanda wa Urazinishaji {harmonization) na uwezeshaji wa shughuli za usafirishaji ndani ya SADC pamoja na masuala ya uratibu, usimamizi na uangalizi wa usafirishaji kwa njia ya barabara katika vituo vya kuingilia, ukaguzi dhidi ya Virusi vya Corona vinavyotambuliwa na SADC na namna ya kuendeleza shughuli za biashara wakati huu wa janga la CORONA ili kunusuru uchumi na kupunguza umasikini ndani ya jumuiya.
Mkutano huo utakuwa chini ya Uenyekiti wa Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Fedha na Mipango, Viwanda na Biashara, Uchukuzi, Utalii na Afya kutoka nchi 16 wanachamawa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Friday, June 19, 2020

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUAPISHWA RAIS MPYA WA BURUNDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye leo Juni 18, 2020. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwa. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye Juni 18,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete  wakiwa katika picha ya pamoja na  Rais  Mpya  wa Burundi Mhe.  Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega nchini Burundi Juni 18,2020. Kulia mwa Mhe. Samia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye punde baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa Burundi Juni 18, 2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  

Makamu wa Rais wa Jarmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) wakiwa na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya Rais Ndayishimiye kuapishwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi Juni 18, 2020 katika Uwanja wa Igoma nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shughuli hiyo.

Rais Mpya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikaguwa Gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi katika Uwanja wa Ingoma 

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha maombolezo Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  


Wednesday, June 17, 2020

NAFASI ZA AJIRA KATIKA JUMUIYA YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR)






JOB OPPORTUNITY AT AFRICAN CONTINENTAL FREE TRADE AREA (AfCTA)



Picha ya Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza wakati wa uhai wake.
Waziri wa mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Balozi
wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Gervais Abayeho.

Prof. Kabudi amekwenda Ubalozini hapo kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki Juni 09,2020.

Prof. Kabudi amekwenda Ubalozini hapo kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki Juni 09,2020.

    Waziri wa mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Burundi Nchini Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki Juni 09,2020.
 Kulia kwake aliyesimama ni Balozi wa Tanzania nchini Burundi Balozi Gervais Abayeho

   Waziri wa mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Balozi Gervais Abayeho mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki Juni 09,2020.

Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Balozi Gervais Abayeho akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Burundi Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki June 09,2020.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Balozi Gervais Abayeho  mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Burundi Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Mhe. Pirre Nkurunziza aliyefariki June 09,2020.

Sunday, June 14, 2020

WACHEZAJI WA MASHINDANO YA DIPLOMATIC GOLF' WAMUAGA MKURUGENZI MKAAZI WA WFP


Wachezaji wa Mashindano ya Diplomatic Golf mchezo ambao  unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wamemuaga mchezaji mwenzao ambae pia ni Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, amebainisha hayo wakati walipokuwa wakifanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine akiwemo, Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford leo katika viwanja vya gymkhana jijini Dar es Salaam. 

Tumekutana Jijini Dar es Salaam, kumuaga mcheza mwenzetu Michael Danford gofl ambaye anakwenda Nairobi kikazi……. limekuwa pambano kali lakini tumemaliza salama.

Pia tutakuwa na fursa ya kumpa zawadi zilizoandaliwa na wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na washindi wengine.

Mchezo wa leo ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kumuaga Bw. Michael Dunford ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini ambapo kwa sasa amepangwa kikazi katika nchi jirani ya Kenya.

"Diplomatic Golf, ni fursa mahsusi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wapenda golf," Amesema Dkt. Ndumbaro.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wakufurahisha.

"Mchezo wetu wa leo ulikuwa mzuri sana na wakufuraisha…..mimi pamoja na Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro tumepata alama sawa," Amesema Bw. Dunford 

Mwaka 2019, Mashindano ya Diplomatic Golf yalifanyika visiwani Zanzibar katika Viwanja vya Zanzibar Golf Course Sea Cliff, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuwa tofauti huku vitu vingi vikiwa vimeboreshwa zaidi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam


Wachezaji wa Mashindano ya Diplomatic Golf wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akimkabidhi Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford moja kati ya zawadi zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje


Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akipokea moja kati ya zawadi zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akiagana na Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford