Tuesday, February 17, 2015

Naibu Waziri mgeni rasmi ufunguzi wa Taasisi ya Sheria za Kimataifa

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Taasisi ya Sheria za Kimataifa ya Afrika-AIIL yenye Makao Makuu yake Jijini Arusha hivi karibuni.
Sehemu ya Wajumbe akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa pili kulia) wakimsikiliza Mhe. Maalim (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Taasisi hiyo.
Mhe. Maalim (wa tano kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria ufunguzi rasmi wa Taasisi ya Sheria za Kimataifa ya Afrika iliyopo Arusha.
Mhe. Maalim akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo kwa Waandishi wa Habari

Monday, February 16, 2015

Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima awasilisha Hati za Utambulisho nchini Laos

Dkt. Aziz Ponary Mlima Balozi wa Tanzania nchini Malaysia akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Laos Mheshimiwa Choummaly Sayasone. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Vientiane nchini Laos.
Dkt Aziz Mlima akifanya mazungumzo na Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Laos ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Laos kwenye Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu Mheshimiwa Alounkeo Kittikhoun.Ubalozi wa Tanzania nchini Malaysia unawakilisha nchi nyingine 6 katika ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia.

Sunday, February 15, 2015

Waziri Membe mgeni rasmi kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka Mpya waKichina

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akipokelewa kwa furaha na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing alipowasili katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina. Waziri Membe amemwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam







Waziri Membe akisalimiana na Brigedia Genral. Rogastian Laswai, Mkuu wa Kikosi cha wanamaji nchini
Waziri Membe akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiq mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mmnazi mmoja.

Waziri Membe akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Bibi. Julieth Kairuki
Mhe. Membe pamoja na Balozi Lu Youqing wakiimba wimbo wa Taifa katika Hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina
Waziri Membe akitoa Salaam za pongezi za kuadhimisha mwaka mpya wa Kichina kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Pia Mhe. Membe alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya china katika kudumisha uhusiano mzuri baina ya Tanzania na China katika nyanja ya Uchumi, Siasa na kijamii.


Balozi Youqimg(Wakwanza kushoto), Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (Wapili kutoka kushoto), Naibu Balozi wa China nchini, na wanne kutoka kushoto ni Mkurugenzi Idaya ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe akihutubia katika Hafla hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini.
Waziri Membe akiendelea kuhutubia
Wachina waishio nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini Hotuba kutoka kwa Mhe. Waziri
Sehemu ya Viongozi mbalimbali kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania walioudhuria katika Hafla hiyo 
Kikundi cha maonyesho ya Utamaduni wa Jamhuri ya watu wa China kikisherehesha
Waziri Membe akifurahia onyesho  lililokuwa likiendelea kuonyesha na kikundi cha nyimbo za tamaduni za Kichina


Maonyesho yakiendelea


Waziri Membe akichukua nambari ya Mshindi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, katika bahati nasibu iliyochezeshwa katika hafla hiyo, mshindi wa zawadi kubwa kabisa katika Bahati nasibu hiyo alikabidhiwa Pikipiki. 

 Balozi Mbelwa Kairuki (wakwanza kulia) akishuudia Bahati nasibu ikichezeshwa na Waziri Membe.
Waziri Membe akiagana na Balozi Lu Youqing mara baada ya kumaliza kufungua maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina

Mkurugenzi Kituo cha uwekezaji Tanzania Bibi. Julieth Kairuki(Katikati), Mkurugenzi Idaya ya Habari Maelezo Bwa. Assah Mwambene (wakwanza kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga wakiwa katika picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Friday, February 13, 2015

WAZIRI MEMBE APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA KUWAIT,MALAWI,AFRIKA KUSINI NA KENYA.

Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kuwait.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini, Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Mheshimiwa Waziri Bernard Membe akizungumza na Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam mara baada ya zoezi la kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kukamilika.
 Mazungumzo yakiendelea huku maofisa wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati (kushoto), Bi.Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali (kulia) na Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
 
Mheshimiwa Waziri akipokea zawadi kutoka kwa balozi mpya wa Kuwait hapa nchini mara baada ya kuwasilisha Nakala ya Hati ya Utambulisho.
 Balozi mpya wa Kuwait hapa nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe (kulia) pamoja na Mheshimiwa Balozi Hassan Simba 
 Yahya. 

Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mpya wa Malawi
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe.Hawa Ndilowe leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Balozi mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe akimsikiliza Mhe.Membe mara baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho ofisini kwa Waziri jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mpya wa Malawi hapa nchini Mhe. Hawa Ndilowe 

Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Afrika Kusini
 Balozi mpya wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanqa Dennis Msekelu akiwasilisha Nalaka za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa waziri Membe akifanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini ofisini kwake muda mfupi baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.


Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi wa Kenya
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Kenya hapa nchini Mhe. Chirau Ali Mwakwere leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kenya hapa Nchini pamoja na Naibu wake wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho.
 Balozi wa Kenya hapa Nchini pamoja na Naibu wake wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe baada ya kukabidhi Nakala za Hati za Utambulisho,huku afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi.Zulegha Tambwe akinukuu mambo muhimu katika mazungumzo hayo.

 Mheshimiwa Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Kenya hapa nchini.
===========
Picha na Reuben Mchome.

Thursday, February 12, 2015

Tanzania na Argentina kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia.

 Tanzania na Argentina zimetiliana saini mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya kisiasa, ambao unaashiria mwanzo wa uhusiano mpana zaidi Kati ya Nchi hizo. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo Kati ya  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Argentina Mhe. Balozi Eduardo Zuian (Kushoto), na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalim, jijini Dar es Salaam Februari 12, 2015. Mawaziri hao pia walitiliana saini mkataba wa ushirikiano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na kile cha Argentina. 
Mhe. Zuian (Kushoto) na Mhe. Dr Mahadhi wakisani mikataba hiyo. Naibu Waziri huyo wa Argentina aliwasili leo alfajiri (February 12) kwa ziara ya siku mbili. 
Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Joseph Sokoine (Kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha, Mipango na Utawala Dkt. Bernard Archiula kwa pamoja wakishuhudia uwekaji saini wa mikataba mikataba hiyo.
Mhe. Balozi Zuian na Mhe. Dkt Mahadhi wakibadilishana Mikataba mara baada ya kumaliza zoezi la kutia saini.
Dkt. Mahadhi (Kulia) wakati wa mazungumzo na Balozi Zuian kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. 

Mkurugenzi idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Sokoine (kushoto) Naibu Mkurugenzi mipango, fedha na utawala wa Chuo cha Diplomasia Dkt Archiula, na Afisa Mambo ya Nje Frank Mhina (kulia), wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Balozi Zuian na Dkt Mahadhi.
Msaidizi wa Mhe. Dkt. Mahadhi, Bw. Adam Isara (kushoto), na Maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Argentina wakati wa mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea.
Naibu Waziri Dkt. Mahadhi akimkabidhi mgeni wake zawadi ya Picha ya Mlima Kilimanjaro.

Mhe. Balozi Zuian Akimkabidhi mwenyeji wake zawadi ya Kikombe cha kiutamaduni kutoka Argentina.

Picha na Reginald Philip