Sunday, February 15, 2015

Waziri Membe mgeni rasmi kwenye sherehe za kuukaribisha mwaka Mpya waKichina

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akipokelewa kwa furaha na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing alipowasili katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina. Waziri Membe amemwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam







Waziri Membe akisalimiana na Brigedia Genral. Rogastian Laswai, Mkuu wa Kikosi cha wanamaji nchini
Waziri Membe akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiq mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mmnazi mmoja.

Waziri Membe akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Bibi. Julieth Kairuki
Mhe. Membe pamoja na Balozi Lu Youqing wakiimba wimbo wa Taifa katika Hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina
Waziri Membe akitoa Salaam za pongezi za kuadhimisha mwaka mpya wa Kichina kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Pia Mhe. Membe alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya china katika kudumisha uhusiano mzuri baina ya Tanzania na China katika nyanja ya Uchumi, Siasa na kijamii.


Balozi Youqimg(Wakwanza kushoto), Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (Wapili kutoka kushoto), Naibu Balozi wa China nchini, na wanne kutoka kushoto ni Mkurugenzi Idaya ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe akihutubia katika Hafla hiyo iliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini.
Waziri Membe akiendelea kuhutubia
Wachina waishio nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini Hotuba kutoka kwa Mhe. Waziri
Sehemu ya Viongozi mbalimbali kutoka Jeshi la Wananchi la Tanzania walioudhuria katika Hafla hiyo 
Kikundi cha maonyesho ya Utamaduni wa Jamhuri ya watu wa China kikisherehesha
Waziri Membe akifurahia onyesho  lililokuwa likiendelea kuonyesha na kikundi cha nyimbo za tamaduni za Kichina


Maonyesho yakiendelea


Waziri Membe akichukua nambari ya Mshindi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, katika bahati nasibu iliyochezeshwa katika hafla hiyo, mshindi wa zawadi kubwa kabisa katika Bahati nasibu hiyo alikabidhiwa Pikipiki. 

 Balozi Mbelwa Kairuki (wakwanza kulia) akishuudia Bahati nasibu ikichezeshwa na Waziri Membe.
Waziri Membe akiagana na Balozi Lu Youqing mara baada ya kumaliza kufungua maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina

Mkurugenzi Kituo cha uwekezaji Tanzania Bibi. Julieth Kairuki(Katikati), Mkurugenzi Idaya ya Habari Maelezo Bwa. Assah Mwambene (wakwanza kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga wakiwa katika picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.