Monday, February 9, 2015

Hotuba ya Waziri Membe kwenye Maadhimisho ya Kanisa la Wasabato SDA

Waziri Membe akiwahutubia mamia ya Waumini wa Kanisa la Sabatoikiwa ni siku ya kilele cha Kongamano la Kimataifa la Utume kwa  Makanisa ya Sabato.  Wengine katika picha waliokaa ni Rais wa Kanisa hilo duniani, Askofu Wilson na Mkewe pamoja na Mhe. Wasira wakimsikiliza.
=============================


Before I start my speech, let me also recognize the presence of Honorable Minister Stephen Wasira the Seventh Day Adventist disciple, who has traveled 500 kilometers to be here. Mheshimiwa Wasira karibu sana.

Before I continue with my speech let me also mention other government officials who are also members of the SDA apart from Honorable Wasira;
The Chief Secretary, Hon. Sefue is an SDA member,
The Attorney General of Tanzania Mr. Masaju is an SDA member,
The Permanent Secretary Mr. Maswi of Energy and Mineral, is an SDA member,

So, I mean there are so many others in government that are not only members but they acknowledge many good things that the SDA has been doing.
….continue in English version, see the Swahili translation….


Before I start my speech, let me also recognize the presence of Honorable Minister Stephen Wasira the Seventh Day Adventist disciple, who has traveled 500 kilometers to be here. Mheshimiwa Wasira karibu sana.

Before I continue with my speech let me also mention other government officials who are also members of the SDA apart from Honorable Wasira;
The Chief Secretary, Hon. Sefue is an SDA member,
The Attorney General of Tanzania Mr. Masaju is an SDA member,
The Permanent Secretary Mr. Maswi of Energy and Mineral, is an SDA member,

So, I mean there are so many others in government that are not only members but they acknowledge many good things that the SDA has been doing.
….continue in English version, see the Swahili translation….


Kwa muhtasari tu kwa Watanzania mlioko wengi, na Watanzania wanaotusikiliza;

Nimemshukuru Rais wa Baraza Kuu la Makanisa ya Sabato Duniani, kwa kujumuika nasi na kuamua Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano hili kubwa sana la bara la Afrika.

Na ni imani yangu kwamba mtapokea salamu hizi nilizotoa kwa niaba ya Serikali…...

Nimemshukuru kwa mwaliko wake kwangu kuja kujumuika nanyi na kufunga Kongamano hili. Nimekubali kwa sababu mbili, kwanza, jambo lenyewe hili la kiroho mnalosimamia na kulifanya ni jambo jema sana kwa ustawi wetu sote. Pili, kongamano hili ni la kimataifa na hivyo linauhusiano na kazi yangu ya uanadiplomasia. Katika miaka 9 ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na miaka 8 ya kuwa Mshauri wa Balozi wa Tanzania nchini Canada, nimejifunza kuwa diplomasia na hofu ya Mungu/imani vikifanya kazi kwa kushirikiana, hakuna changamoto yoyote ya kidunia isiyoweza kukabiliwa. (MAKOFI)

 Nimezungumzia uhusiano kati ya Serikali na Dini. Nimesema kuwa vitu hivi viwili havitenganishiki, ni sura mbili za sarafu. Kwa sababu, binadamu ni mwili na roho na kila kimoja hakina budi kuendelezwa. Serikali inashughulika na miili na akili, Dini zinashughulika na roho. Dini na Serikali zikifanya kazi pamoja sawasawa, tutahitaji sheria chache, polisi wachache, magereza machache. Dunia itakuwa mahala pazuri pa kuishi. Tunahitajiana.(MAKOFI)

Wenzetu wa vyombo vya dini wanahubiri amani wanakiri imani, sisi wanadiplomasia na Serikali tunatengeneza amani na wakati mwingine tunatumia vyombo vya dola kuitengeneza hiyo amani. Kwa hiyo lengo letu ni moja, kuleta amani, utulivu, katika nchi. Wenzetu njia yao ni nyembamba --sorry-- ni nyembamba lakini ina mapana na ni nzuri zaidi, kuliko ile tunayoitumia sisi. (MAKOFI)

Lakini diplomasia na dini zinakutana kwenye kukuza amani, ulinzi na usalama duniani.

Lakini pia tunakutana kwenye maadili. Viongozi wanaolelewa vizuri na dini zao, wanakuwa waadilifu. Na SDA ni miongoni mwa dini zinazoweka viongozi wazuri sana wa nchi yetu. (MAKOFI)

Na kwasababu hiyo basi, unapoona diplomasia inatengeneza mahusiano mazuri ya dunia, dunia inaangalia uadilifu kwanza, kama kigezo cha uongozi bora, na kama kigezo cha watu wenye amani na utulivu. Na kawaida Serikali, diplomasia na dini hata Rais mwenyewe, tunakutana tunapozungumzia masuala ya uadilifu wa viongozi wake. (MAKOFI)

Tunzeni hiyo, hubirini uadilifu, na mshiriki katika kutengeneza viongozi bora kwa misingi ya uadilifu. (MAKOFI)

Lakini jingine, nimeshukuru sana Kanisa la Sabato kwa kazi na mwenendo mzuri unaofanywa katika nchi yetu. Unapoona kwamba watu milioni nne waliomo nchini kwetu, wa SDA, wana shule za msingi 10, wana shule za sekondari 15, wana vyuo vikuu 2, wana hospitali kubwa 2, wana vituo vya albino vinavyofanya kazi hapa nchini. (MAKOFI)

Hivi kama kingekua chama cha siasa, nani angeshindwa kuwapa ushindi wa utawala wa nchi hii. (MAKOFI)

Nani angeshindwa kuwapa ushindi. Lakini ukiachia hayo, ni Chama cha Mapinduzi peke yake chenye kumudu kazi hiyo. (MAKOFI, VIGELEGELE, VICHEKO)

Lakini naomba niweke wazi kabisa, kama chombo cha dini, kama SDA, kinajali wananchi wake, kitaacha vipi kupanuka kutoka watu 15,000 mwaka 1960 hadi kufikia watu milioni nne mwaka 2012. (MAKOFI) Wataacha vipi kupanuka na kuwa watu wengi kwa huduma hii, wanayoitoa kwa wananchi. (MAKOFI)

Nawapongeza sana watu wa SDA, mbele ya kiongozi wenu wa dunia, kwa kazi nzuri mnayoifanya na shule mnayofundisha Watanzania kwamba ukitaka kuongoza Watanzania, fanya kama SDA. (MAKOFI)

Nalipongeza kanisa la SDA kuwa mfano mzuri wa ustahimilivu na uvumilivu wa dini na imani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yangu yote ya nafasi yangu ya uwaziri, na kaka yangu Mzee Wasira ataniunga mkono kwenye hili, sijawahi kusikia mgogoro wa kimatatizo wala mfarakano unaoongozwa na SDA (MAKOFI) dhidi ya madhehebu mengine, au dhidi ya wananchi. (MAKOFI)

Mpo, mnafanya kazi zenu, mnachapa shuguli zenu kwa amani na utulivu, hamjachokoza mtu, na hamtachokoza mtu, na hiyo ni sifa mojawapo ya nchi yenye amani duniani. (MAKOFI)

Hongereni sana wana SDA. (MAKOFI)

Narudia, kama wananchi wote wa dini zote tukiiga mfano wenu, Tanzania tutasonga mbele kama Taifa. (MAKOFI)

Nawashukuruni kwa kunisikiliza na ninawatakia maandalizi mazuri ya kongamano la kidunia litakalofanyika baadae mwaka huu huko Marekani. (MAKOFI)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.