Thursday, February 19, 2015

Marekani kushirikiana na Tanzania kudhibiti uingizaji wa bidhaa haram Nchini

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwafafanulia jambo maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalamaya nchini Marekani katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikiwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto)na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho.Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula(watatu kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama ya nchini Marekani. Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington DC kujadiliana masuala mbalimbali likiwemo la Maafisa hao wakitarajia kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.