Thursday, February 12, 2015

Tanzania na Argentina kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia.

 Tanzania na Argentina zimetiliana saini mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya kisiasa, ambao unaashiria mwanzo wa uhusiano mpana zaidi Kati ya Nchi hizo. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo Kati ya  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Argentina Mhe. Balozi Eduardo Zuian (Kushoto), na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalim, jijini Dar es Salaam Februari 12, 2015. Mawaziri hao pia walitiliana saini mkataba wa ushirikiano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na kile cha Argentina. 
Mhe. Zuian (Kushoto) na Mhe. Dr Mahadhi wakisani mikataba hiyo. Naibu Waziri huyo wa Argentina aliwasili leo alfajiri (February 12) kwa ziara ya siku mbili. 
Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Joseph Sokoine (Kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Fedha, Mipango na Utawala Dkt. Bernard Archiula kwa pamoja wakishuhudia uwekaji saini wa mikataba mikataba hiyo.
Mhe. Balozi Zuian na Mhe. Dkt Mahadhi wakibadilishana Mikataba mara baada ya kumaliza zoezi la kutia saini.
Dkt. Mahadhi (Kulia) wakati wa mazungumzo na Balozi Zuian kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje. 

Mkurugenzi idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Sokoine (kushoto) Naibu Mkurugenzi mipango, fedha na utawala wa Chuo cha Diplomasia Dkt Archiula, na Afisa Mambo ya Nje Frank Mhina (kulia), wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Balozi Zuian na Dkt Mahadhi.
Msaidizi wa Mhe. Dkt. Mahadhi, Bw. Adam Isara (kushoto), na Maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Argentina wakati wa mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea.
Naibu Waziri Dkt. Mahadhi akimkabidhi mgeni wake zawadi ya Picha ya Mlima Kilimanjaro.

Mhe. Balozi Zuian Akimkabidhi mwenyeji wake zawadi ya Kikombe cha kiutamaduni kutoka Argentina.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.