Friday, February 6, 2015

Rais wa Ujerumani amaliza ziara yake nchini

Rais Joachim Gauck, akipata heshima ya nyimbo ya taifa lake ikiwa ni sehemu ya kumwaga mara baada ya kumaliza ziara ya siku tano hapa nchini. Katika ziara yake Rais Gauck ametembelea Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha na kutembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti. Kupitia Ziara ya Rais wa Ujerumani kume dhihirisha Uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Ujerumani, ukizingatia Ujerumani inaisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta maji 
Gwaride likitoa Heshima kwa Rais Gauk 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Daudi Felix Ntibenda akiongozana na Rais Gauck wakati wa kuagana naye 
Rais Gauck na Mkewe wakitazama ngoma ya kitamaduni la kabila la Kimaasai
Waziri wa Maji Mh. Prof. Maghemba akiagana na Rais Gauck mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akiagana na Rais Gauck.
Mkurugenzi Msaidiza Idara ya Amerika na Ulaya, Bibi. Victoria Mwakasege akiagana na Rais Gauck
Raid Joachim Gauck akiagana na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Itifaki Bwa. James Bwana mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano 
Rais Joachim Gauck na Mama Schadt wakiwaaga viongozi mbalimbali kwa kuwapungia tayari wa kuanza safari ya kurujea nchini Ujerumani
Viongozi Mbalimbali wa Serikali kwa pamoja wakimwaga Rais Gauck kwa kumpungia mkono katika kiwanja cha Ndege cha KIA.


Picha na Reginald Philip.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.