Friday, January 8, 2016

Tanzanian Mbwana Samatta wins African Player of the Year based in Africa



Mr. Mbwana Aly Samatta-2nd from left receiving an Award as the African Player of the Year based in Africa during an event that took place in Abuja, Nigeria on 7th January, 2016
=============================================




Press Release


The Tanzania Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation wishes to inform the world and all football fans that Mr. Mbwana Aly Samatta, the African Player of the Year based in Africa is a citizen of Tanzania and not of Botswana or Tunisia as was reported by NBC Sports.com and several other international media.  

Mr. Samatta is one of the star players of the Tanzania national team (Taifa Stars) currently playing for TP Mazembe Club in the Congo DRC.


The Tanzanian icon was announced by the Confederation of African Football (CAF) as the African Player of the Year based in Africa in an event that took place in Abuja, Nigeria on 07th January, 2016. Mr. Samatta becomes the first player from   East Africa to win the prestigious title.


The Ministry takes this opportunity to thank Mr. Samatta for placing Tanzania on the international football stage and congratulate him for the victory well deserved.


Issued by:

Government Communication Unit
Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation

8th January, 2016




Wednesday, January 6, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mashauriano kuhusu mgogoro wa Burundi baina ya Tanzania, Angola, Uganda na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameihakikishia dunia leo kuwa mazungumzo ya kuleta amani nchini Burundi bado yanaendelea vizuri licha ya taarifa zilizosambaa kuwa mazungumzo hayo yamegonga mwamba.
Dkt. Mahiga ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashauriano baina yake na Mhe. George Pinto Chicoti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR); Mhe. Dkt. Crispus Kiyonga, Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye ni mwakilishi wa msuluhishi wa mgogoro wa Burundi Rais Yoweri Kaguta Museveni, pamoja na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha tarehe 6 Januari 2016.
Akielezea madhumuni ya mashauriano hayo Dkt. Mahiga alisema kuwa wadau hawa wanaunga mkono na kusifu jitihada zinazofanyika ndani na nje ya Burundi zenye lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa kisiasa na kiusalama nchini humo kwa njia ya majadiliano.
Aidha Waziri Mahiga alisema mazungumzo hayo pia yanalenga kubadilishana ushauri, mawazo na kuandaa taarifa ya pamoja kabla ya mikutano mikubwa ya kikanda; yaani ule wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR Summit), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Summit) na Umoja wa Afrika (AU Summit) inayotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka huu.
Dkt. Mahiga alisema mazungumzo yao yaliyojumuisha nchi za Tanzania, Angola na Uganda ambazo zimekasimiwa majukumu ya uenyekiti na usuluhishi na jumuiya zao, yatatoa uelewa wa pamoja wa jinsi ya kuendesha mashauriano ya kuleta amani ya kudumu kabla ya mikutano tarajiwa ambayo pamoja na mambo mengine, itajadili pia suala la amani na usalama nchini Burundi.
“Naomba nirudie tena mbele yenu waandishi wa habari kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli; kama wenyekiti wa jumuiya hii, bado tuna nia ya dhati kabisa ya kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunapata suluhu ya mgogoro huu, ambayo ni muhimu sana kwa usalama na maendeleo ya eneo letu na bara la Afrika kwa ujumla” alisisitiza Dkt. Mahiga kabla ya kuanza mazungumzo ya faragha na viongozi wenzake.
Waziri Dkt. Mahiga alipongeza jitihada za wadau wengine na jumuiya ya kimataifa zinazoendelea ili kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo.
           
MWISHO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa.
06 Januari 2016


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Balozi wa India nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba (Mb.) akizungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya (kushoto), katika mazungumzo yao Mhe. Kolimba aliupongeza Ubalozi wa India kwa kuendelea kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na India katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya maji. Kwa upande, Balozi Arya alimpongeza Mhe. Naibu Waziri Kolimba kwa kuteuliwa katika wadhifa huo.
Balozi Arya naye akizungumza alipokutana na Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Kolimba
Mkutano ukiendelea.


Picha na Reginald Philip.

Tuesday, January 5, 2016

Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini, Mhe. Song Geum-young. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Januari, 2016.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (wa kwanza kulia) akiongoza ujumbe wa Wizara kwenye hafla ya uwasilishwaji wa Hati za Utambulisho zilizofanyika Ikulu. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki ( wa pili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatib Makenga
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Song Geum-young Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.).
Mhe. Rais akizungumza na Balozi Song Geum-young
Balozi Song Geum-young akisaini Kitabu cha wageni alipowasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho
Picha ya Juu: Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Song Geum-young akisikiliza wimbo wa taifa uliopigwa na Bendi ya Polisi (picha ya chini) wakati alipowasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais. Wengine katika picha ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na Mnikulu.

Balozi Song Geum-young akiagana na kiongozi wa Bendi ya Polisi

Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa EU nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Roeland Van De Geer. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Januari, 2016.
 
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Roeland Van De Geer,  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.).
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Anthony Mtafya.
Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Roeland Van De Geer
Mhe. Rais akizungumza na Balozi Roeland Van De Geer mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho

Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Van De Geer, Mhe. Dkt. Kolimba, Msaidizi wa Rais masuala ya Diplomasia, Bi. Zuhura Bundala (wa kwanza kulia)  pamoja na wajumbe kutoka Ubalozi wa EU.
Balozi Roeland Van De Geer akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu
Balozi Roeland Van De Geer akisikiliza wimbo wa taifa wa Tanzania na EU kutoka Bendi ya Polisi ikiwa ni kwa  heshima yake
Mhe. Balozi Roeland Van De Geer akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi

Mhe. Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Palestina nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Januari, 2016.
Mhe. Rais Magufuli akimtambulisha kwa Balozi Shabat Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.).
Mhe. Balozi Shabat akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya  Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. Batholomeo Jungu.
Mhe. Rais Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Shabat
Mhe. Rais Magufuli akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Shabat mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Shabat akisaini Kitabu cha wageni alipowasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho
Balozi Shabat (katikati) akisikiliza wimbo wa taifa lake ulipopigwa na Bendi ya Polisi kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Kushto kwake ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na kulia kwake ni Mnikulu.
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana akifuatilia wimbo wa Taifa
Balozi Shabat akiagana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi.