Thursday, July 20, 2017

Makamu wa Rais Mhe. Samia Azindua Ripoti ya Nchi ya APRM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzindua ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Ummoja wa Afrika kujipima kwa vigezo vya Utawala (APRM.), kushoto ni kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Silvia Mabandla, uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, APRM, na taasisi nyingine za kiserikali. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wawakilishi wa Nchi mbalimbali na Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Sehemu ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).
Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu chenye ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo.
Bi. Brigitte Silvia Mabandla, naye akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa kuishukuru Tanzania kwa kutoa ushirikiano mzuri wa kuhakikisha Ripoti hiyo inakamilika kwa wakati, pia alitumia fursa hiyo kulipongeza Jopo zima la watendaji walioshiriki katika kuiandaa ripoti hiyo kwa  ufanisi wa hali ya juu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki naye akizungumza katika uzinduzi huo, ambapo pia alitumia fursa hiyo kumkaribisha Bi. Brigitte Silvia Mabandla nchini, pia kuipongeza APRM kwa kufanya kazi nzuri.
Sehemu ya viongozi Mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa.
Profesa Hasa Mlawa naye akielezea namna ripoti hiyo ilivyo kusanywa na kuhakikiwa na viongozi wanachama.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiongozwa na Mkufunzi wao Bw. Jambo (wa tatu kutoka kusoto), nao walishiriki katika uzinduzi wa Ripoti hiyo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga akitoa mwongozo wa ratiba kwenye hafla ya Uzinduzi wa ripoti hiyo.
Hafla ya Uzinduzi ikiendelea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kutoka kulia), Bi. Mabandla (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Aziz Mlima (wa pili kutoka kulia) Balozi Ombeni Sefue (wa kwanza kulia ) na Profesa Mlawa (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa hapa nchini. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kutoka kulia), Bi. Mabandla (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Aziz Mlima (wa pili kutoka kulia) Balozi Ombeni Sefue (wa kwanza kulia ) na Profesa Mlawa (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi kutoka chuo cha Diplomasia

DKT. MAHIGA AFUNGUA MKUTANO MAWAZIRI WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM


Wednesday, July 19, 2017

Chungulia Fursa Boda to Boda

Kituo Kikuu cha Mabasi, Dodoma
Bw. Justin Kisoka, Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye amebobea katika masuala ya uchumi akitoa somo namna vijana wa Kitanzania watakavyoweza kuuza bidhaa zao ndani ya soko la Afrika Mashariki lenye nchi sita na idadi ya watu wanaofikia milioni 165. 
Mfanyabiashara akielezwa namna bidhaa zake ambazo amezibeba kichwani atakavyoweza kuziuza katika nchi za Afrika Mashariki na kupata faida kubwa.

Ujumbe wa kutaka vijana na Watanzania kwa ujumla wazinduke ili wanufaike na soko la Afrika Mashariki ulifikishwa kwa njia tofauti ikiwemo sanaa ya maigizo.

Baadhi ya watu waliojitokeza kupata mbinu za kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hapa ilikuwa Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Dodoma.


Gandhi Hall , Mwanza 

Bw. Justin Kisoka akiwa kwenye bustani ya Gandhi Hall mjini Mwanza akitoa somo namna Wanamwanza watakavyoweza kuuza Sato, Sangara na bidhaa nyingine katika soko la Afrika Mashariki.

Wanamwanza acheni woga, vukeni mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zenu, ni baadhi ya maneno aliyokuwa anayatumia Mchumi huyo katika kuwashajihisha vijana wachangamke kuvuka mipaka ya Tanzania kuuza bidhaa zao.

Dada somo limemkolea anapata maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa Wizara ili shughuli ya kuvuka mipaka ianze mara moja.


Viwanja vya Furahisha, Mwanza
Bw. Abel Maganya, Mtaalamu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje akitoa somo kwenye viwanja vya  furahisha. 

Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatimiza majukumu yake kwa kuweka mazingira mazuri ikiwemo sheria, kanuni na miundombimu ili wanajumuiya mfanye biashara katika nchi unayopenda bila bugdha. Msijifungie ndani vukeni mipaka kupeleka bidhaa mbalimbali.

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya furahisha.

Mzee anasema somo limengia barabara hivyo na  uzee wangu nawahimiza wajukuu zangu kufanya biashara ya kuvuka mipaka. Anafikisha ujumbe wake kwa kushiriki kusakata dance linalohimiza biashara za kuvuka boda.

Tuesday, July 18, 2017

Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa SADC ngazi ya Wataalam wafunguliwa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Organ Dkt. Aziz Mlima akitoa hotuba ya ufungunzi  wa Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa SADC kwenye Ushirikiano wa Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ngazi ya wataalam.
Mkurugenzi mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Tax (wa pili kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa 19 wa Mawaziri wa SADC mara baada ya ufunguzi wa ngazi ya wataalam, kulia kwake  ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Organ Dkt. Aziz Mlima, kushoto ni Mkurugenzi wa Organ kwenye masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Jorge Cardoso, Mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Innocent Shiyo, Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 17 - 21 Julai.
Juu na Chini ni wajumbe wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa 19 wa Mawaziri wa SADC kwenye ushirikiano wa masuala ya siasa, ulinzi na Usalama ngazi ya wataalam.
Balozi Innocent Shio (wa kwanza kulia), akichangia hoja wakati mkutano ukiendelea, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Usalama nchini Dkt. Modestus Francis Kipilimba, kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mhe. Simon Sirro na anayefuata ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Mhe. Valentino Mlowola wakimsikiliza balozi Shiyo

Friday, July 14, 2017

Vijana wahimizwa kuchangamkia fursa katika boda za EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga akiwahutubia vijana kwenye kongamano la kuwahimiza kuchangamkia fursa za biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hususan mipakani. Kongamano hilo lenye kaulimbiu "Chungulia Fursa Border to Border limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Taasisi ya Sekta Binafsi  na Trade Mark East Afrika ambao ni wafadhili wakuu wa kongamano hilo. Kongamano litafanyika kwa siku 10 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza na Arusha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed akiwasilisha hotuba katika kongamano hilo. Waziri Mohammed alisema lazima vijana wapewe fursa kwa kuwa wao ndio nguzo ya usalama na amani kwenye Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, alisema wao ni waanzilishi tu lakini uhai wa Jumuiya unategemea vijana namna watakavyoilinda na kuidumisha jumuiya hiyo.

Waziri Mohammed akiendelea kusoma hotuba yake kwa vijana wanaoshiriki kongamano hilo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa na washiriki wa kongamano la kuhamisha vijana kuchamkia fursa za EAC

Mkurugenzi Mkazi wa East Africa TradeMark, Bw. John Ulanga ambaye taasisi yake ni mdhamini wa kongamano hilo akieleza majukumu ya taasisi hiyo katika kutoa elimu ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga (katikati) akizindua moja ya kitabu cha tafiti zilizofanywa na REPOA kuhusu ajira na ushiriki wa Asasi za kijamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa TMEA na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sekta Binafsi

Washiriki wa kongamano wakionesha mshikamano ambao wataenda nao katika kuchamkia fursa za EAC

Burdani



Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya awasilisha Ujumbe Maalum
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed. Mhe. Mohammed amekuja nchini kwa ziara ya siku moja kwasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Kenya, Mhe Uhuru Kenyatta kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, John Pombe Magufuli. Mawaziri hao wamekubaliana na pendekezo la kuunda Kamati ambayo itaongozwa na wao wenyewe itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kwa haraka matatizo ya kibiashara yatakayojitokeza kati ya nchi hizo.

Ujumbe wa Tanzania na Kenya ukiwa katika mazungumzo

Waziri Mahiga akipokea Ujumbe Maalum kwa niaba ya Mhe. Rais Magufuli kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya
Picha ya pamoja

Thursday, July 13, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Lesotho aliwasilisha Ujumbe Maalum kwa Makamu wa Rais

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kulia), Mheshimiwa Lesego Makgothi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Lesotho (Katikati) kushoto kwake ni Mhe. Dkt. Suzan Kolimba -Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wanaofuata ni watalaam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakiwa katika mazungumzo baada ya Mhe.Lesego Makgothi kukabidhi ujumbe maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, katika Ofisi za Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Julai,2017




Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
( wa pili Kulia), Mheshimiwa Lesego Makgothi wa pili  kushoto, Mhe.Dkt. Suzan Kolimba -Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kwanza kushoto na Balozi. Innocent Shiyo- Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo katika Ofisi za Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Julai,2017

Ziara ya Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco nchini 12 -13 Julai, 2017


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ziara ya Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco nchini 12 -13 Julai, 2017

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Serikali ya Ufalme wa Morocco Mhe.Mounia Boucetta na ujumbe wake wametembelea Wizara leo tarehe 13 Julai, 2017 na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam. Mhe. Mounia Boucetta yupo nchini kwa ziara ya kikazi tangu tarehe 12 Julai, 2017.

Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Maazimio na makubaliano ya Ushirikiano kati ya taasisi za Tanzania na Morocco katika sekta mbalimbali, yaliyosainiwa wakati wa ziara ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco nchini Tanzania tarehe 23 – 25 Octoba, 2016. 

Itakumbukwa katika ziara hii jumla ya mikataba 21 ya Ushirikiano katika maeneo mbalimbali ilisainiwa. Mikataba hiyo ni katika masuala yafuatayo; Masuala ya Usafiri wa Anga, Kilimo na Uvuvi, Nishati, Utalii, Viwanda Usafiri wa Reli, Biashara, Masuala ya Bima, Masuala ya Afya, Masuala ya Gesi, Masuala ya Siasa, Uchumi, Sayansi na Utamaduni. 

Aidha Mheshimiwa Mfalme Mohamed VI aliahidi mambo makuu matatu
·        Ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa jijini Dar es salaam
·        Ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira mjini Dodoma
·        Kuanzisha programu ya mafunzo kwa maafisa wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

Tangu ziara hiyo ifanyike Serikali ya Ufalme wa Morocco, katika kuimarisha urafiki na ushirikiano ilifungua Ubalozi wake jijini Dar es salaam, na Mwezi Februari, 2017 Mheshimiwa Balozi Abdelillah Benryane aliwasilisha hati zake za utambulisho Nchini.

Wizara inawataarifu kuwa Ubalozi umeanza kufanya kazi nzuri, kazi mojawapo kubwa ni kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo iliyosainiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Mfalme.

Hivyo ujio wa Mheshimiwa Naibu Waziri Mounia Boucetta ni sehemu ya ufuatiliaji wa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mikataba hiyo iliyosainiwa.

Wizara ilifanya kikao na Mheshimwa Mounia Boucetta  na kupitia taarifa ya utekelezaji wa mikataba hiyo kwa sekta ya umma na sekta binafsi, na kwa kweli tunaridhishwa na kasi ya utekelezaji.

Pamoja na kasi nzuri hiyo ya utekelezaji Wizara imezielekeza taasisi husika kuongeza kasi zaidi ili tukamilishe utekelezaji wa maeneo hayo tuliokubaliana na kuwawezesha Watanzania wafanyabiashara, wakulima, wazalishaji na wasomi kunufaika na fursa mbalimbali.

Aidha, akizungumza katika majadiliano hayo Naibu Waziri Mhe. Dr. Suzan Kolimba (Mb) amesema wamekubaliana kuundwa Kamati ya Ufuatiliaji ya utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kati ya Tanzania na Morocco. 

Mhe. Mounia Boucetta pamoja na ujumbe wake leo saa 4:00 asubuhi watakutana na ujumbe wa wadau wa biashara na uwekezaji kutoka Wizara na taasisi za Serikali pamoja na taasisi binafsi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam

-Mwisho-

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 13 Julai, 2017
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa Morocco kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba (Mb) kusoma hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha kufuatilia utekelezaji wa maazimio na Makubaliano mbalimbali baina ya sekta za Tanzania na Morocco yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme VI wa Morocco nchini Tanzania.

Naibu Waziri Suzan Kolimba akisoma hotuba yake katika kikao hicho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Morocco, Mhe. Mounia Boucetta akisoma hotuba katika kikao kazi cha kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Tanzania na Morocco

Ujumbe wa Tanzania ukiwajumuisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wanaounda kikosi kazi cha kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya Morocco na Tanzania
Ujumbe wa Morocco katika kikao hicho
Washiriki wa kikao kazi cha kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kati ya Tanzania na Morocco wakiwa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji kilichofanyika Serena Hoteli

Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Suzan Kolimba (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka  Ufalme wa Morocco Mhe.Mounia Boucetta katika ukumbi wa Wizara- Dar es Salaam, tarehe 13 Julai,2017.
 
 Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt.Suzan Kolimba akipokea zawadi kutoka kwa, Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Morocco baada ya mazungumzo.

Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Suzan Kolimba, Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Morocco na ujumbe wake, wengine ni wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo