Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili leo tarehe 15 Agosti 2018 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek, Namibia ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018.
Thursday, August 16, 2018
Wednesday, August 15, 2018
Ubalozi wa Tanzania nchini Korea waandaa kongamano kuhamasisha wawekezaji sekta ya afya
Balozi wa Tanzania nchini Korea
Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akitoa neno la ukaribisho katika Kongamano
hilo.
|
Rais wa “Korea-Africa Foundation”
waandaaji wenza wa Kongamano hilo, Balozi CHOI, Yeon-ho, akitoa neno katika
hafla ya ufunguzi.
|
“Congressman” na Katibu wa “National Assembly Forum for Africa’s New Era” katika Bunge la Jamhuri ya Korea, Mhe. KIM, Gyu-hwan akitoa salamu za pongezi katika Kongamano hilo. |
Picha ya Pamoja ikijumuisha meza
kuu na watoa mada kutoka: TIC, TFDA, MSD, Korea Health Industry Development
Institute (KHIDI) na “Korea Medical Devices Industrial Association”.
|
Add caption |
Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania
wakiwa na mwenyeji wao Balozi Matilda Swilla Masuka, baada ya kufanikisha
Kongamano hilo la aina yake na lililovutia makampuni ya madawa na vifaa tiba
zaidi ya 100.
|
Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa katika
picha ya pamoja na Wana Diaspora ambao walishiriki kikamilifu katika Kongamano
hilo la kuhamasisha wawekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba.
|
Ziara ya Kikazi ya Chuo cha Diplomasia nchini India.
Chuo cha Diplomasia Tanzania (Center for Foreign Relation -CFR) wamefanya ziara ya kikazi nchini India kuanzia tarehe 13-15 Agosti 2018. Ziara hiyo imekuja kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia ya India (Foreign Service Institute-FSI), na ililenga kujua shughuli za FSI na taasisi zinazoshirikiana nazo, pamoja na kujadiliana juu ya uwezekano wa kuingia katika makubaliano ya ushirikiano.
Wajumbe wa CFR waliongozwa na Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi (Mst.), ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya CFR. Wajumbe wengine walikuwa ni pamoja na Kaimu Mkuu wa cha Diplomasia (CFR), Dr Bernard Achiula, Dr Lucy Shule wa CFR, Dr Richard Mbunda kutoka UDSM, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia (DAA), Bibi Justa Nyange. Kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India, alikuwepo Balozi Baraka Luvanda na Bibi Natihaika Msuya, Afisa Mambo ya Nje.
Aidha, wajumbe hao walipata fursa ya kutoa mihadhara katika Kituo cha Stadi za Masuala ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Nehru, Taasisi ya Stadi za Masuala ya Ulinzi na Usalama (IDSA) pamoja na Taasisi ya Tafiti Mahususi kuhusu ushirikiano baina ya Nchi za Kusini (South Cooperation Research Information System-RIS).
Kwa ujumla, ziara hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa ambapo taasisi wenyeji zimeonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na CFR katika kujenga uwezo wa wanadiplomasia wa Tanzania.
Balozi Ombeni Sefue akimkabidhi Mkuu wa Taasisi ya Stadi za Masuala ya Afrika, Profesa Ajay Dubey zawadi ya Kinyago. |
Newly elected Member of Parliament in Pakistan with African Origin.
Tanzeela Qambrani, an African- Pakistanis woman whose ancestors originate from Tanzania has been elected as a Member of Parliament in Pakistan. She was nominated by the Pakistan People Party (PPP). Qambrani has been elected to a special seat for women in the provincial parliament in Sindh. She aims at eliminating the stigma attached to her community, known as the Habashi, Sibbi or Sheedi who are the descendants of the Bantu people from Africa.
Tuesday, August 14, 2018
Wajumbe wa Mauritius wa wasili nchini kuangalia maeneo ya Uwekezaji wa viwanda vya sukari.
Ujumbe wa Serikali ya Mauritius ukiongozwa na Balozi wao mwenye Makazi yake Mjini Maputo, Msumbiji Mhe. Jean Pierre Jhumun umewasili nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uwekezaji wa viwanda vya sukari.
Ukiwa nchini, ujumbe huo umepanga kukutana na Viongozi mbalimbali wakiwemo; Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mazingira (Ofisi ya Makamu wa Rais), Uongozi wa kituo cha Uwekezaji (TIC), Bodi ya Sukari pamoja na kuonana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Awamu ya pili ya Mradi huo (baada ya miaka mitano) inategemewa kufanyika Mkoani Kigoma ambapo sukari itakayozalishwa pia itasafirishwa na kuuzwa katika nchi za jirani.
Kaimu Katibu Mkuu Mhe Balozi. Ramadhan Mwinyi akikaribisha wageni hao. |
Pichani ni Wajumbe wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), pamoja na Balozi Jhumun akiwa na Bw. Boodram kutoka Mauritius (kulia, mwisho). |
Monday, August 13, 2018
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC wafunguliwa mjini Windhoek, Namibia
Mkutano wa
siku mbili wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC) umefunguliwa rasmi katika Hoteli ya Safari mjini Windhoek, Namibia
tarehe 13 Agosti 2018.
Ujumbe wa
Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye ameambatana na
viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania ambao ni pamoja na Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda;
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayesimamia masuala ya
Ujenzi) Mhandisi Joseph Myamhanga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt.
Evaristo Longopa; Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu
Kazungu na Naibu Katibu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Edwin
Paul Mhede.
Mkutano huu
ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi
na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini
Windhoek, Namibia. Mikutano mingine ya awali ni mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC
uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa , Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on
Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao
utapitia na kujadili hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda kwa kipindi
cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018.
Mkutano wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na
Usalama utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe
wake ambao ni Angola (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa
Siasa, Ulinzi na Usalama), Zambia (Makamu
Mwenyekiti wa Organ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mwenyekiti wa Organ
aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi).
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utapokea, kujadili na kutolea
maamuzi ya mapendekezo mbalimbali yanayotokana na mikutano ya kisekta na kamati
za jumuiya kwa kipindi cha mwaka 2017/18. Pamoja
na mambo mengine mkutano huu;
Utafanya uteuzi wa Mwenyekiti wa SADC na inatarajiwa kuwa Jamhuri
ya Namibia ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa
Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha 2018/2019. Nafasi ya Makamu mwenyekiti
itajazwa pia na nchi itakayoteuliwa ambayo itajulikana tarehe 17Agosti 2018.
Uteuzi wa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama
ya SADC. Inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Zambia, ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa
sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha 2018/2019. Hivi sasa
Tanzania ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake kwenye Asasi
ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on
Politics, Defence and Security).
Mambo
mengine yanayotarajiwa kujitokeza na kujadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na; masuala ya fedha;
Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda wa SADC
(Report on the operationazaition) na Maendeleo ya Viwanda;
Kutia saini itifaki
mbalimbali ikiwa ni pamoja na itifaki ya Kulinda
Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea ya mwaka 2017. Pia Mkutano huu utatoka na tamko la nchi wanachama wa SADC la kutokomeza
malaria katika ukanda wa SADC ifikapo mwaka 2030.
==========================================================
Mwenyekiti mpya wa Mawaziri wa SADC, Mhe. Nandi-Ndaitwa akihutubia mara baada ya kupokea nafasi hiyo. Katika hotuba yake alisistiza umuhimu wa kuwawezesha vijina kwa kuwa ndio nguzo kuu katika kuinua uchumi wa taifa lolote duniani sambamba na uwekezaji katika viwanda. Pamoja na hayo akaeleza malengo makuu ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kuondoa umasikini na kuinua uchumi ndani ya kanda. |
Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Mhe. Sylivester Ambokile na wajumbe wengine wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa mkutano. |
Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia mkutano. |
Balozi wa Namibia nchini Tanzania pamoja na wajumbe wengine wa mkutano huo wakifuatilia hafla ya ufunguzi. |
Saturday, August 11, 2018
Katibu Mkuu Mambo ya Nje atembelea Chuo Kikuu cha Tiba cha Namibia
Prof. Kenneth Matengu (wa kwanza kulia) akimwongoza Prof. Mkenda na ujumbe wake kutembelea chuo hicho. |
Wa kwanza kushoto ni Mhadhiri katika chuo hicho akifafanua taratibu za masomo ya nadharia na vitendo zinavyoendeshwa katika chuo hicho. |
Wakitembelea Maabara za kufundishia. |
Wakitembelea vyumba vya semina kwa wanafunzi. |
Baadhi ya majengo ya ofisi na madarasa katika Chuo kikuu cha Tiba cha Namibia. |
Wizara ya Mambo ya Nje yahamasisha uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Mifugo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amefanya mazungumzo
na kampuni ya Burmeister & Partiners (PTY) LTD ya nchini Namibia
tarehe 10 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.
Akiongea
na uongozi wa kampuni hiyo Prof. Mkenda alieleza Tanzania ina eneo kubwa la
ardhi yenye rutuba ambayo haitumiki
na rasilimali watu ya kutosha hivyo ni fursa kwa mwekezaji mwenye nia thabiti kuwekeza nchini.
“Lengo
la Serikali ni kupata mwekezaji aliye makini kama wewe nimeona una mradi mkubwa
wa shamba la mifugo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya machinjio nina imani ukija
kuwekeza Tanzania hautajutia kabisa kwakuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa
katika miradi itaongeza thamani ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa na kuwezesha kupatikana kwa soko la kimataifa” alisema Prof. Mkenda
Naye
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Hendrik Boshoff alieleza kampuni imekuwa ikifanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kampuni hiyo imefungua kampuni ya maziwa nchini Rwanda ambayo inauza na kusafirisha mataifa mengine pia imewekeza nchini Angola katika miradi ya uvuvi na imekuwa ikifanya vizuri katika biashara zake zote.
Pia
alisema kampuni imebobea katika miradi ya ujenzi, nishati, miradi ya maji, usafiri, usanifu majengo, ujenzi wa
majengo, miradi ya machinjio, mashamba ya mifugo na pia ipo katika mpango
wa kuanzisha miradi ya viwanda vya dawa za binadamu ambapo utekelezaji wake utaanza mara baada ya kukamilisha mazungumzo na
wataalamu kutoka nchini Cuba.
Prof. Mkenda alieleza miradi yote kutoka katika kampuni hiyo inatija kubwa kwa maendeleo ya taifa la Tanzania hivyo akaikaribisha kampuni hiyo kuja mapema nchini ili kuweza kujionea rasilimali zilizopo na kuainisha miradi watakayoweza kuanza nayo. Vilevile akaeleza kampuni hiyo ina nafasi ya kutumia fursa za mji wa
Dodoma katika uwekezaji kufuatia kuhama kwa mji wa Serikali kutoka
Dar es Salaam.
Kampuni ya Burmeisters & Partiners (PTY) LTD ilianza kufanya kazi zake nchini Namibia mwaka 1984 na baadae kuwa miongoni mwa kampuni kubwa zilizowekeza nchini humo. Pia ni kampuni hiyo inatoa huduma za kihandisi na huduma za usimamizi wa miradi katika taaluma mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister & Partners (PYT) LTD, Mhandisi Hendrik Boshoff akielezea usanifu wa miradi mbalimbali unaofanywa na kampuni ya Burmeister & patners (PTY) LTD. |
Sehemu ya ofisi iliyosanifiwa na kampuni hiyo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Mwakilishi kutoka kampuni hiyo akiwasilisha miradi mbalimbali iliyosanifiwa na kampuni ya Burmeister & Partners (PTY) LTD |
Prof. Mkenda akifafanua tunu na rasilimali zilizopo nchini ambazo ni fursa kwa uwekezaji. |
Friday, August 10, 2018
Tanzania na Namibia kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Elimu ya juu.
Serikali ya Tanzania imeonesha
nia ya wazi ya kuongeza maeneo ya ushirikiano katika sekta ya elimu ya juu na
Serikali ya Namibia ambapo ushirikiano huo utawezesha walimu na wanafunzi kuwa
na progamu za kubadilishana kwa lengo la kupeana uzoefu na kujengeana uwezo.
Hayo yamesemwa wakati wa ziara
ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Adolf F. Mkenda katika chuo kikuu cha Namibia cha Sayansi na Teknolojia Mjini Windhoek, Namibia tarehe 09 Agosti 2018.
Katika ziara hiyo Prof. Mkenda
aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake mjini
Pretoria nchini Afrika Kusini, Mhe. Balozi Sylivester Ambokile, Balozi wa
Namibia nchini Tanzania, Mhe. Theresia Samaria na Mkurugenzi wa Sera na Mipango
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James
Lugaganya.
Lengo la ziara hiyo ni kujadili
namna ya kuongeza ushirikiano katika sekta ya elimu ya juu kwenye masuala ya utafiti
na ugunduzi katika taaluma za teknolojia zinazotolewa na vyuo vitakavyoingia
makubaliano ya ushirikiano.
“Nimekuja tushirikishane mikakati mbalimbali tunayoweza kujiwekea ili kuvifanya vyuo vyetu viwe bora ndani ya kanda na Afrika kwa ujumla pia tujadili mbinu mpya za kielimu ambazo Tanzania na Namibia zinaweza zikashirikiana,”alisema Prof. Mkenda
Pia akaeleza nchi nyingi za
Afrika zinapata changamoto ya uwezo mdogo na uhaba wa rasilimali fedha katika
kuhakikisha upatikanaji wa malazi kwa wanafunzi, upatikanaji wa elimu kwa
vitendo na kwamba ni vema Tanzania na Namibia zikatumia fursa za ushirikiano wa
elimu zinazosainiwa katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Namibia cha Sayansi na Teknolojia,
Dkt. Tjama Tjivikua alieleza kuwa hadi sasa chuo kimefanikiwa kuanzisha
ushirikiano na taasisi, makampuni na viwanda mbalimbali nchini humo na hata nje
ya nchi ili kuwawezesha wahitimu katika chuo hicho kupata nafasi ya elimu kwa
vitendo.
“Jitihada hizi zimeshaanza
kuleta matunda kwa kuwa kwa sasa wahitimu wa chuo hiki wamefanikiwa kupata
ajira katika taasisi hizo na wengine walifanikiwa kupata ajira kabla ya kuhitimu
muda wa mafunzo” alisema Dkt. Tjivikua
Vilevile chuo kinashirikiana
na wadau mbalimbali ambapo alieleza Tanzania ni mmoja wa wadau kupitia chuo cha
Sayansi ya Kilimo Sokoine(SUA) na chuo kikuu cha Ardhi, wadau wengine ni pamoja
na Afrika Kusini, Cameroon, Kenya,
Botwana, Uswiss, na mashirika mengine ya kimataifa.
Balozi wa Tanzania nchini
Namibia, Mhe. Sylivester Ambokile naye alisema kwa kuwa jumuiya ya wanamibia
imezungukwa na jamii inayozungumza Kiswahili hivyo ni vema ushirikiano uliopo
ukazidi kuimarishwa kwa kuingiza lugha ya Kiswahili katika idara za lugha za
kigeni kwenye vyuo vikuu nchini Namibia.
“Katika hafla ya utambulisho
wangu kwa Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob niliwasilisha wazo la
Kiswahili kuingizwa katika Idara za Lugha ya kigeni na lilipokelewa vizuri,
hivyo kwa sasa ofisi za ubalozi zinafanya jitihada za kukumbushia katika sekta
husika ili utekelezaji wake ukamilike mapema”. alisema Mhe. Balozi Ambokile
Nchini Namibia elimu ya juu
imeanza mwaka 1979/1980 kutokana na kuchelewa huko kuliifanya Namibia kuhitaji
Walimu wa taaluma mbalimbali kutoka mataifa mengine. Tanzania ni miongoni mwa
nchi yenye walimu wengi katika vyuo vikuu ya Namibia. Pamoja na kuwepo kwa
ushirikiano huo Chuo kikuu cha Namibia cha Sayansi na Teknolojia tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1992 kimekuwa kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) katika kupata wataalamu wazuri wa masuala ya mifugo ambao
wamekuwa wakirejea baada ya masomo na kulitumikia taifa kwa tija.
====================================================
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akitembelea maeneo ya chuo kikuu cha Namibia cha Sayansi na Teknolojia ili kuweza kujionea uendeshaji wa vipindi vya masomo na mpangilio wa majengo kwa ajili ya madarasa na malazi ya wanafunzi. |
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na uongozi wa chuo, wa kwanza kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Theresia Samaria, kulia kwa Prof. Mkenda ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Ambokile na pembeni yake ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. James Lugaganya. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Subscribe to:
Posts (Atom)