Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amefanya mazungumzo
na kampuni ya Burmeister & Partiners (PTY) LTD ya nchini Namibia
tarehe 10 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.
Akiongea
na uongozi wa kampuni hiyo Prof. Mkenda alieleza Tanzania ina eneo kubwa la
ardhi yenye rutuba ambayo haitumiki
na rasilimali watu ya kutosha hivyo ni fursa kwa mwekezaji mwenye nia thabiti kuwekeza nchini.
“Lengo
la Serikali ni kupata mwekezaji aliye makini kama wewe nimeona una mradi mkubwa
wa shamba la mifugo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya machinjio nina imani ukija
kuwekeza Tanzania hautajutia kabisa kwakuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa
katika miradi itaongeza thamani ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa na kuwezesha kupatikana kwa soko la kimataifa” alisema Prof. Mkenda
Naye
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Hendrik Boshoff alieleza kampuni imekuwa ikifanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kampuni hiyo imefungua kampuni ya maziwa nchini Rwanda ambayo inauza na kusafirisha mataifa mengine pia imewekeza nchini Angola katika miradi ya uvuvi na imekuwa ikifanya vizuri katika biashara zake zote.
Pia
alisema kampuni imebobea katika miradi ya ujenzi, nishati, miradi ya maji, usafiri, usanifu majengo, ujenzi wa
majengo, miradi ya machinjio, mashamba ya mifugo na pia ipo katika mpango
wa kuanzisha miradi ya viwanda vya dawa za binadamu ambapo utekelezaji wake utaanza mara baada ya kukamilisha mazungumzo na
wataalamu kutoka nchini Cuba.
Prof. Mkenda alieleza miradi yote kutoka katika kampuni hiyo inatija kubwa kwa maendeleo ya taifa la Tanzania hivyo akaikaribisha kampuni hiyo kuja mapema nchini ili kuweza kujionea rasilimali zilizopo na kuainisha miradi watakayoweza kuanza nayo. Vilevile akaeleza kampuni hiyo ina nafasi ya kutumia fursa za mji wa
Dodoma katika uwekezaji kufuatia kuhama kwa mji wa Serikali kutoka
Dar es Salaam.
Kampuni ya Burmeisters & Partiners (PTY) LTD ilianza kufanya kazi zake nchini Namibia mwaka 1984 na baadae kuwa miongoni mwa kampuni kubwa zilizowekeza nchini humo. Pia ni kampuni hiyo inatoa huduma za kihandisi na huduma za usimamizi wa miradi katika taaluma mbalimbali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister & Partners (PYT) LTD, Mhandisi Hendrik Boshoff akielezea usanifu wa miradi mbalimbali unaofanywa na kampuni ya Burmeister & patners (PTY) LTD. |
Sehemu ya ofisi iliyosanifiwa na kampuni hiyo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Mwakilishi kutoka kampuni hiyo akiwasilisha miradi mbalimbali iliyosanifiwa na kampuni ya Burmeister & Partners (PTY) LTD |
Prof. Mkenda akifafanua tunu na rasilimali zilizopo nchini ambazo ni fursa kwa uwekezaji. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.