Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mjini Windhoek, Namibia tarehe 18 Agosti 2018.
|
Katika Mkutano huo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan alisaini itifaki ya kazi na ajira, itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea ya mwaka 2017.
Pia amesaini Tamko la nchi wanachama wa SADC la kutokomeza malaria katika ukanda wa SADC ifikapo mwaka 2030 na maboresho ya Katiba inayosimamia masuala ya Kamati ndogo ya Wakuu wa Polisi katika Organ.
|
Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo aliwashukuru wanachama wote kwa kuendelea kuiamini Tanzania katika nafasi za uongozi ndani ya Jumuiya hiyo pamoja na kuahidi kuendelea kushirikiana katika shughuli za maendeleo, siasa, ulinzi, na usalama. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.