|
Timu za mpira wa miguu za Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) na Burundi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mechi ya marudiano iliyofanyika katika uwanja wa Gitega, Burundi. Katika mpambano huo wa Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea nchini humo Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Burundi.
Aidha, Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki katika kipengele cha mpira wa miguu limekamilisha ratiba kwa mpambano kati ya Tanzania na Burundi, ambapo Tanzania imejishindia medali ya dhahabu kufuatia ushidi ilioupata. Burundi imejitwalia medali ya fedha kwa kushika nafasi ya pili katika mchezo huo.
Katika mchezo wa awali Tanzania iliibuka na ushindi wa goli 8-1 dhidi ya wenyeji wa tamasha Burundi. |
|
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi wa medali za dhahabu kufuatia ushindi wa goli 5-0 ilioupata dhidi ya Burundi katika Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki |
|
Sehemu ya mashabiki wakishangilia mchezo uliokuwa ukiendelea kati ya Tanzania na Burundi |
|
Mmoja wa wachezaji wa timu ya Tanzania akipongezwa na Bw. Addo Komba Afisa kutoka Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo mara baada ya kuvishwa medali ya dhahabu |
Picha na Matukio ya Mpira pete
|
Timu ya mpira wa pete ya Tanzania ikiwa tayari kwa mchuano dhidi ya Uganda kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki. Katika mchuano huo Uganda iliibuka na ushindi wa goli 53-33 dhidi ya Tanzania.
Katika mchezo wa awali Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa goli 79-14 dhidi ya wenyeji wa mashindano Burundi. |
|
Wachezaji wa timu ya Tanzania (waliovalia jezi rangi ya waridi) wakijaribu kuzuia moja ya shambulio lililofanywa na timu pinzani ya Uganda |
|
Mchezo wa mpira wa pete kati ya Tanzania na Uganda ukiendelea |
|
Mshambuliaji wa timu ya Tanzania akilekeza mashambulizi kwa timu pinzani ya Uganda kwenye moja ya pambano la Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.