Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika (The 38th Ordinary of the SADC Summit of
Heads of State and Government) utafanyika tarehe 17-18 Agosti, 2018.
Mkutano huu utatanguliwa na mikutano ifuatayo;
(i)
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on
Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao
utapitia na kujadili hali ya siasa, ulinzi
na usalama katika kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. Mkutano
huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao
ni Angola (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi
na Usalama), Zambia (Makamu Mwenyekiti wa
Organ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda
wa uenyekiti wa Asasi).
(ii)
Mkutano wa Mawaziri
utakaofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 14 Agosti 2018 pamoja; na
(iii)
Mkutano wa Makatibu
Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe
9 hadi 11Agosti 2018.
Prof Adolf Mkenda, Katibu Mkuu, Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki anaonagoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Makatibu
Wakuu akisaidiana na Eng. Joseph Nyamhanga,
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ( Ujenzi), Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango.
Mhe Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ataongoza ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
utapokea, kujadili na kutolea maamuzi ya mapendekezo mbalimbali yanayotokana na
mikutano ya kisekta na kamati za jumuiya kwa kipindi cha mwaka 2017/18.
Pamoja na mambo mengine mkutano huu;
1. Utafanya uteuzi wa Mwenyekiti wa SADC na
inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Namibia
ambayo ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha 2018/2019.
Nafasi ya Makamu mwenyekiti itajazwa pia na nchi itakayoteuliwa itajulikana
tarehe 17Agosti 2018
2. Uteuzi wa Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Inatarajiwa kuwa Jamhuri ya Zambia, ambayo
ni Makamu Mwenyekiti wa sasa itateuliwa kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha
2018/2019. Hivi sasa Tanzania ni Mwenyekiti
anayemaliza muda wake kwenye
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on
Politics, Defence and Security)
3. Maeneo mengine yanayotarajiwa kujitokeza na kujadiliwa katika mkutano
huu ni haya yafuatayo
(i)
masuala ya fedha;
(ii)
Utekelezaji wa Mpango
Mkakati wa Viwanda wa SADC ( Report on the operaionazaition Maendeleo ya
viwanda;
(iii)
Kutia saini itifaki mbalimbali ikiwa ni pamoja na tifaki ya Kulinda
Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina Mpya za Mbegu za Mimea ya mwaka 2017.
(iv)
Pia Mkutano huu utatoka
na Tamko la nchi wanachama wa SADC la kutokomeza malaria katika ukanda wa SADC
ifikapo mwaka 2030.
=======================================================
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.