Brigadia Generali Mary Hiki akizungumza na wanamichezo kutoka (Tanzania hawapo pichani) washiriki wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki linaloendelea jijini Bujumbura, Burundi. Brigadia Generali Hiki ambaye anahudumu katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi alizungumza na wanamichezo hao kwaniaba Kaimu ya Balozi. Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza nchi Burundi limetokana na maagizo ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.
Tamasha hili lenye kauli mbiu "kujenga Jumuiya ya Afrika Mashariki na amani kupitia michezo" linafanyika kuanzia terehe 16 hadi 30 Agosti, 2018. Washiriki zaidi 1000 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watashiriki kwenye michezo mbalimbali ya tamasha hili.
Tanzania imewakilishwa na jumla ya wanamichezo 58 ambao watashiriki katika michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, riadha na karatee.
Tamasha hili limefunguliwa tarehe 16 Agosti 2018 na Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, katika viwanja vya Sekondari vya SOS jijini Burundi na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji waserikali kutoka nchi wanachama. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.