TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
wanawake (UN Women), Mhe. Bi. Phumzile Mlambo-Ngcuka anategemea kufanya ziara
ya kikazi hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 24 Agosti, 2018. Ziara hiyo pamoja
na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Shirika hilo
na Tanzania.
Akiwa nchini, Bi. Mlambo-Ngcuka atahudhuria Mkutano wa Usawa
wa Kijinsia,Malengo ya Maendeleo Endelevu na Vyombo vya Habari (Gender Equality, Sustainable Development
Goals and Media Summit), utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 hadi 24 Agosti, 2018.
Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, Mkurugenzi huyo
atatembelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na UN Women katika mkoa wa Dar es
Salaam. Aidha, Bi. Mlambo-Ngcuka ataonana
na viongozi wa kitaifa na viongozi wengine wa Serikali.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma.
20 Agosti, 2018
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.