KONGAMANO LA BIASHARA
NA UWEKEZAJI
KUHAMASISHA WADAU WA
MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA LAFANYIKA SEOUL, KOREA
Ubalozi wa Tanzania uliopo Seoul
nchini Korea kwa kushirikiana na “Korea-Africa Foundation” na “Korea Chamber of
Commerce and Industry” uliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa wadau wa
sekta ya Afya lililofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea. Kongamano hilo la aina yake, liliandaliwa ili
kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika kuboresha sekta ya Afya.
Kongamano hilo lililenga
kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Tanzania, lilihudhuriwa
na makampuni zaidi ya 100, kutoka pande zote mbili ikijumuisha: Makampuni ya
utengenezaji madawa na vifaa tiba; Vyuo Vikuu; Taasisi za utafiti; Hospitali;
Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Makampuni kutoka katika sekta
binafsi; na Diaspora wa Tanzania waliopo Seoul.
Wakati wa Kongamano hilo, mada
mbalimbali ziliwasilishwa zikijumuisha: Fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya
utengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Mazingira ya ufanyaji biashara na vivutio
“incentives” vinavyotolewa na Serikali; Hali ya soko na uhitaji (Market
Potentiality); Taratibu za kufuatwa katika uingizwaji wa bidhaa za madawa na
uanzishwaji wa viwanda husika; na Utayari wa sekta binafsi katika kushirikiana
na wenzao wa Korea katika biashara na ubia katika viwanda vya madawa na vifaa
tiba.
Kongamano
hilo lilijumuisha wadau kutoka Wizara na Taasisi za kuitendaji za hapa nchini
ikiwa ni pamoja na Wizara ya Afya;
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji; Kituo cha Uwekezaji (TIC); MSD; TFDA, na Chama cha wenye
Viwanda vya Dawa Tanzania (Tanzania Association Pharmaceutical Industries-TAPI).
Kwa upande wa Korea wawakilishi
walitoka Vyama vya watengenezaji wa madawa
na vifaa tiba walitoa mada iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na upande
wa Tanzania. Kongamano lilihitimishwa kwa B2B, ambapo makampuni na Taasisi
zilikutana kujadiliana zaidi fursa, maeneo ya ushirikiano, na kupata ufafanuzi
wa kina katika maeneo mbalimbali; na baadaye kutembelea Makampuni ya
Madawa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.