Wednesday, October 24, 2018

Dkt. Mahiga azungumza na Watanzania wanaoishi Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa kwenye  Taasisi ya kidini ya Mt.Egidio Padri Angelo Romano, Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi ya Taasisi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2018 jijini Roma. Dkt. Mahiga yupo Italia kwa ajili ya kuhudhuria mikutano mbalimbali ikiwemo Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka Afrika na Italia ambao utafanyika tarehe 25 Oktoba,2018 pamoja na kukutana na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendedelo ya Kilimo (IFAD) tarehe 26Oktoba,2018.

Dkt. Mahoiga akiagana na Padri Angelo Romano mara baada ya kumaliza mazungumzo.


=====Dkt. Mahiga akutana na Watanzania nchini Italia=====

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Madafa leo tarehe 25 Oktoba,2018 akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Dkt. Augustine Mahiga(Mb), kwenye kikao na Watanzania waishio nchini Italia. Kikao hicho kilifanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Italia Bw.Andrew Mohele akitoa salamu za wanadiaspora kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga. Mkutano huo ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2018 kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Rome, Italia.
Baadhi ya Watanzania waishio Italia wakiwa kwenye mkutano huo



Tuesday, October 23, 2018

Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 73 tokea kuanzishwa


Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Waandishi leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ikiwa ni matayarisho ya kusherehekea miaka 73 ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 24 Oktoba husherehekewa Duniani kote na kwa Tanzania yataadhimishwa jijini Dar es Salaam na Zanzibar,  kushoto ni Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu  Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania  na kulia  Bw. Deusdedit  B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.

Bw. Deusdedit  B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikianoano wa Kimataifa kulia akimkaribisha Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kushoto kuzungumza na waandishi  wa habari katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mkutano huo ulifanyika kufuatia tarehe 24 Oktoba, Umoja wa Mataifa utaadhimisha Miaka 73 ya tokea kuanzishwa kwake. Katikati Mhe. Dkt. Damas Ndumaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Bw. Alvaro Rodriguez,  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania aliyekaa kushoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere akilelezea juu ya maendeleo ya Umoja huo na kaulimbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba iliyobeba ujumbe wa "Uwezeshaji  Vijana na Ubunifu kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu" 
Baadhi wa waandishi wa Habari walioshiriki katika mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
 Add caption

Friday, October 19, 2018

Dkt. Ndumbaro akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kamati ya CPPCC ya China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya  Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC), Bw. Lou Jiwei alipofika ofisini kwake Dodoma leo tarehe 19 Oktoba, 2018 kwa lengo la kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Mkurugenzi huyo anaongoza ujumbe wa watu wanne wa Kamati hiyo ambao wapo nchini kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai.

Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Jengo la LAPF jijini Dodoma kwa mazungumzo. Mkurugenzi huyo ni mgeni wa kwanza kutoka nchi za nje kumtembelea katika ofisi yake ya  Dodoma.

Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akimkabidhi zawadi ya kitabu  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ikiwa  ni kumbukumbu ya kukutana naye  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akibadilishana mawazo na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.  Wang Ke baada ya kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC).

Thursday, October 18, 2018

Makabidhiano rasmi ya Ofisi ya Naibu Waziri yafanyika

Mhe. Dkt. Damas Ndubaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo amekabidhiwa rasmi Wizara hiyo na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan A. Kolimba (Mb), hafla ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtaa wa Makole jingo la LAPF  jijini Dodoma. Katika hafla  ya makabidhiano walihudhuria Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo waliosimama nyuma ya viongozi hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Ndumbaro (Mb) akimshukuru aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan A. Kolimba (Mb) katika hafla ya makabidhiano rasmi ya ofisi jijini Dodoma.

Picha ya pamoja ya Mhe. Dkt. Ndubaro Naibu Waziri Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeingia katika ofisi na Mhe. Dkt. Suzan A Kolimba aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayeondoka katika ofisi hiyo wakiwa wamekaa wakibadilishana mawazo.