Tuesday, December 3, 2019

Tanzania na Namibia Zajizatiti kukuza Biashara baina yao


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya Mhe. Nandi-Ndaitwah kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Tume ya Kudumu ya  Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia.
Naibu Waziri Mkuu naWaziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AAfrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiangalia picha za matukio ya wapigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Namibia.

Naibu Waziri Mkuu naWaziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiweka saini Kitabu cha Wageni alipowasili Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia leo jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, (Mb) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, (Mb)
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiwasilisha hotuba yake wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia leo jijini Dar es Salaam. Wenginine kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (Mb) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb)
Baadhi ya Makatibu Wakuu, maafisa waandamizi wa Serikali, maafisa wa Serikali pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa JPC leo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Kuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) wakiweka saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kati ya Tanzania na Namibia. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kati ya Tanzania na Namibia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakisaini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Masuala ya Utalii kati ya Tanzania na Namibia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Masuala ya Utalii kati ya Tanzania na Namibia.

Meza kuu katika picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Theresia Samaria Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, (Mb) na Waziri wa Viwanda Mhe. Innocent Bashungwa, (Mb) Pamoja na Makatibu Wakuu, na Viongozi waandamizi wa Serikali.

Saturday, November 30, 2019

Tanzania na Nambia zaweka Mikakati ya Kujiimarisha Kiuchumi




Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo akifanya utambulisho wa viongozi wa Tanzania wanaoshiriki mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Waliokaa mstari wa mbele ni Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wanaoshiriki mkutano wa JPC ambao walikuwa wanatambulishwa na Bw. Kayombo.
Viongozi katika Meza Kuu. Kutoka kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Theresia Samaria; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Joseph Buchweishaija.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano wa JPC ngazi ya Makatibu Wakuu akisoma hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia.
Dkt. Mnyepe akiendelea kusoma hotuba, huku wajumbe wakimsikiliza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi ambaye ni Mwenyekiti mwenza akisoma hotuba ya ufunguzi katika mkutano huo.
Wajumbe wanaoshiriki kikao cha JPC wakifuatilia hotuba za viongzo zilizokuwa zinawasilishwa.
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Namibia, Dkt. Faraji K. Mnyepe na Balozi Selma Ashipala-Musavyi wakipongezana baada ya kuwasilisha hotuba za ufunguzi katika Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Namibia.
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Elizabeth Rwetunga akiongoza wajumbe wa mkutano kupitia rasimu ya taarifa ya masuala waliyoyajadili na kukubaliana.
Watumishi kutoka Taasisi za Serikali wakifuatilia Mkutano wa JPC.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo akiongea na vyombo vya habari kuhusu mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia. 
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za Tanzania na Namibia, Dkt. Faraji K. Mnyepe (mwenye suti) na Balozi Selma Ashipala-Musavyi wakiongea na waandishi wa habari kuhusu JPC kati ya Tanzania na Namibia.


Viongozi wa Tanzania na Namibia wakiwa katika picha ya pamoja.

Wednesday, November 27, 2019

Tanzania Mwenyeji wa Mkutano wa JPC na Namibia


Tumbi Kutumia Sanamu Kufanya Mafunzo ya Afya kwa Vitendo


Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi, Kibaha), Dkt. Sylas Msangi akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya makabidhiano ya Sanamu kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wataalamu wa afya. Sanamu hilo limetolewa msaada na Umoja wa Wataalamu wa Afya wa Watanzania wanaoishi Uingereza (Tanzania-UK Healthcare Diaspora Asociation-TUHEDA)
Mwakilishi wa TUHEDA ambaye ni Mtanzania anayeishi Uingereza na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Sukari, Bw. Nasibu Mwande akiongea machache kuhusu umuhimu wa Sanamu kwa wataalamu wa afya katika mafunzo kwa vitendo.
Mkurugenzi wa Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega akitoa maelezo namna Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuhamasisha Diaspora waweze kuchangia maendeleo ya nchi yao.
Meza Kuu ikipiga makofi kuunga mkono maelezo ya Balozi Anisa.
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Caroline Damian ambaye alikuwa Mgeni Rasmi aliyepokea Sanamu kwa niaba ya Serikali.
Sanamu ambayo, Dkt. Damian alimpokea kwa niaba ya Serikali akiwa anapatiwa matibabu kwa madhumuni ya wataalamu wa afya kujifunza kwa vitendo. Anayetoa maelezo ni mtaalamu kutoka Uingereza ambaye ni rafiki wa Watanzania wanaoishi Uingereza.


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye alimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa katika hafla ya makabidhiano ya Sanamu.

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya cha Kibaha (Kibaha College of Health and Allied Science) wakishuhudia hafla ya makabidhiano ya sanamu.
Mgeni Rasmi, Dkt. Damian (kushoto), Dkt. Msangi anayefuatia, Balozi Anisa na Dkt. Mwande (kulia) wakikata utepe kuashiria kuanza kutumika kwa sanamu kwa wataalamu wa afya katika kufundishia.
Sanamu aliyebatizwa jina la Msafriri amezinduliwa rasmi ili watalamu wa afya wamtumie kufanya mafunzo kwa vitendo.
Dkt. Damian akipokea vitabu vya msaada vyenye thamani ya milioni 30 za Kitanzania kutoka taasisi ya TUHEDA. Vitabu hivyo vitasambazwa kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Picha ya Pamoja






Tuesday, November 26, 2019

MKUTANO WA 39 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC KUANZA KESHO JIJINI ARUSHA

 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliomalizika leo Jijini Arusha
 Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili jambo wakati wa Mkutano wao. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Afrika Mashariki - Uganda, Bibi. Edith Mwanje, akifuatiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Tanzania, Dkt. Faraji Mnyepe. Wengine ni Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masula ya EAC - Sudani Kusini, Bw. Mou Mou Athian Kuol, akifuatiwa na Meja Generali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa - Uganda, Balozi Charles Karamba. Wengine pichani ni Katibu Mwandamizi, Wizara ya Afrika Mashariki na - Kenya, Dkt. Margaret Mwakima na katibu Mkuu, Office ya Rais Inayohusu masula ya Afrika Mashariki - Burundi, Balozi Jean Rigi. 



Makatibu Wakuu Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano wao (Ngazi ya Makatibu Wakuu) uliomalizika leo jijini Arusha
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiwasilisha mada kwa Makatibu wakuu (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Makatibu wakuu wa EAC Jijini Arusha

   

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kwanza kesho tarehe 27 Novemba 2019  jijini Arusha.

Kuanza kwa mkutano huo kunafuatia kukamilika kwa Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ulioanza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Novemba 2019.

Mkutano wa Makatibu Wakuu  pamoja na mambo mengine, umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo kwa mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya hiyo utakaoanza  tarehe 27 Novemba 2019.

Mkutano huu wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeandaliwa kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari, 2020.


Monday, November 25, 2019

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA TDB

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema leo, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse ,Ikulu jijini Dodoma.

Bw. Tadesse akiwa ameambatana na ujumbe wake amewasili  uwanja wa ndege wa jijini Dodoma leo, Novemba 25, 2019 na kulakiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert  A. Ibuge. 

Akizungumza muda mfupi baada kumaliza mazungumzo na Mheshimiwa Rais Magufuli,  Bw. Tadesse amesema TDB itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania na kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili  ya kutekeleza miradi mbalimbali maendeleo nchini.

Mhe. Dkt. Mpango amesema TDB imekuwa moja ya Benki kinara ambayo imekuwa ikitoa mikopo ya masharti nafuu kwa Tanzania hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya maendeleo.

Aidha, Bw. Tadesse akiwa nchini atatembelea maeneo mbalimbali sambamba na kujionea miradi ya maendeleo inayotelezwa na Serikali ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, mradi wa kuzalisha umeme wa Kilwa na miradi mingine ambayo mkopo kutoka (TDB) utaelekezwa.  

Bw. Tadesse amesifu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya  Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika. 

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati), Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (mweji vazi la Jeshi) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Watatu kushoto) wakijongea usawa wa ndege kumlaki Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse alipowasili jijini Dodoma Novemba 25, 2019.
Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisalimiana na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse wakati anawasili jijini Dodoma. 
Viongozi na Watendaji wa Serikali wakiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse mara baada ya kumlaki katika uwanja wa ndege jijini Dodoma. 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Bw. Admassu Tadesse wakifurahia jambo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dodoma


Picha ya pamoja


Sunday, November 24, 2019

BARUA HII IPUUZWE

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa barua hii inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii inayodaiwa kutoka kwa Bw. Steyn kutelekezwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba John Kabudi (Mb) si ya kweli na anuani zilizotumiwa hazitumiwi na Wizara wala Wizara hivyo jamii IIPUUZE barua hiyo.
Taarifa zote rasmi zitatolewa kupitia mitandao rasmi ya Wizara na vyombo mbalimbali vya habari.