Friday, January 14, 2022
WAZIRI MULAMULA AMUAGA BALOZI WA MALAWI NCHINI
TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MISRI KATIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Serikali ya Tanzania imepokea tani 16 za Dawa, Vifaa Tiba na Vifaa Kinga
ikiwa ni msaada wenye thamani ya shillingi milioni 864 kutoka Serikali ya Misri.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali wakati wa hafla fupi ya kupokea shehena
ya dawa hizo iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi
amesema Tanzania inaishukuru Serikali ya Misri kwa msaada huo muhimu kwa
wananchi wa Tanzania na kwamba itandelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya
Misri hususan katika kuboresha sekta ya afya na kuahidi kuusimamia kikamilifu msaada huo ili uwafikie walengwa kwa wakati.
Pia aliongeza kusema kuwa, msaada
huo umewasili wakati mwafaka ambao Tanzania inaendelea kuboresha sekta ya afya kwa
kusogeza huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuongeza upatikanaji wa Dawa na
Vifaa Tiba katika maeneo ya mijini na vijijini.
Aidha, alipongeza ushirikiano wa kidiplomasia uliopo
kati ya Tanzania na Misri ambao umekuwa wa manufaa makubwa tangu kuanzishwa
kwake na kupongeza jitihada zinazofanywa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha Sekta ya Afya nchini ambapo
alisema msaada huo ni miongoni mwa matokeo ya ziara ya Mhe. Rais aliyoifanya
nchini Misri mwezi Novemba, 2021.
"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na pia kwa
niaba ya Waziri wa Afya. Mhe. Ummy Mwalimu napokea msaada huu wa Dawa na Vifaa
Tiba wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 800 kutoka Serikali ya Misri. Kama
Serikali, tunaendelea kuboresha na kusogeza huduma za afya kwa wananchi hivyo
msaada huu utachangia jitihada hizo. Ninakuomba Mhe. Balozi ufikishe salamu
zetu za shukrani kwa Mhe. Abdel Fattah Al-Sisi, Rais wa Misri kwa msaada huu
ambao tumeupokea kwa dhati na utatimiza lengo lilokusudiwa la kuwasaidia wananchi
wa Tanzania" alisema Dkt. Makubi.
Kwa upande wake, Balozi wa Misri hapa nchini. Mhe.
Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na
Tanzania na inaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya
uongozi makini wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania za kuwaletea watanzania maendeleo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.
Kadhalika, Mhe. Balozi Abulwafa alieleza kuwa,
mbali na ushirikiano wa Tanzania na Misri kwenye sekta ya afya, Nchi yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kutoa fursa za mafunzo ya kuwajengea uwezo watu
wa sekta ya afya na fani mbalimbali kwa watanzania.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifelo Sichwale, Mfamasia Mkuu wa Serikali, Bw. Daudi Msasi, Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Celestine Kakele na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi kwa pamoja na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Mohamed Gaber Mohamed Abulwafa wakisaini Hati ya Makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba vilivyopokelewa nchini kutoka Misri
Afisa Mambo ya Nje katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Faith Masaka akibadilishana mawazo na Afisa kutoka Ubalozi wa Misri hapa nchini, Bw. Mahmoud Hamdy Khalifa wakati wa hafla ya makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba kutoka Misri |
Thursday, January 13, 2022
WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WATEULE WA SAUDI ARABIA, KOREA, INDONESIA NA MOROCCO NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mhe. Abdullah bin Ali Alsheryan. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma. Mara baada ya makabidhiano viongozi hao walipata fursa ya kuzungumza juu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo pamoja na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano. |
Balozi Mulamula akimkaribisha Mhe.Abdullah bin Ali Alsheryan katika ofisi za Wizara zilizopo mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Kim Sun Pyo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma. |
Mara baada ya makabidhiano hayo Waziri Mulamula alimhakikishia Mhe.Kim Sun Pyo kuwa serikali ya Tanzania itampa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake mapya katika kipindi chake atakachohudumu nchini. Jamhuri ya Korea imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika sekta za teknolojia ya mawasiliano, elimu, afya, utalii na ujenzi wa miundobinu.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Triyogo Jatmiko. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma. |
Mhe. Balozi Mulamula na Mhe. Triyogo Jatmiko walijadili juu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na masoko, viwanda, elimu, utalii na kufungua fursa nyingine za kiuchumi kupitia ushirikiano imara wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ufalme wa Morocco, Mhe.Zacharia El Guoumiri. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma. |
Mazungumzo baina ya Mhe.Balozi Mulamula na Mhe. Balozi Zacharia El Guoumiri yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baiba ya Tanzania na Morocco hususani katika sekta za michezo, elimu, maendeleo ya jamii na kuinua ujasiliamali kwa lengo la kukuza viwanda ili kuweza kuwanufaisha wananchi mataifa yao. |
Mazungumzo yakiendelea, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Azizi akifatilia mazungumzo hayo. |
SADC YAKUBALIANA KUENDELEA KUISADIA MSUMBIJI KULINDA AMANI
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji ulioanza jana tarehe 11 Januari 2022 nchini Malawi umemalizika leo tarehe 12 Januari 2022 ambapo Nchi wanachama wa SADC wamekubaliana kuendelea kuisaidia Jamhuri ya Msumbiji katika kuhakikisha Amani na usalama vinapatikana.
Pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali, wamekubaliana kuendelea kujitolea kulinda amani na usalama nchini Msumbiji hasa katika Jimbo la Cabo Delgado licha ya nchi nyingi kuendelea kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa uviko 19.
Akifunga Mkutano huo leo, Rais wa Jamhuri ya Malawi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Lazarus Chakwera amewashukuru wakuuu wa Nchi na Serikali kwa Ushirikiano na umoja ambao nchi wanachama wa SADC wamekuwa wakionesha katika kuisaidia Jamhuri ya Msumbiji kupambana na ugaidi.
“Lazima tuungane kwa pamoja na kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Msumbiji inakuwa na Amani na Usalama……hivyo basi ni jukumu letu sisi sote katika kuhakikisha wananchi wa Msumbiji wanakuwa na amani kwani bila amani hakuna maendeleo,” amesema Rais Chakwera.
Awali akisoma tamko la pamoja, Katibu Mendaji wa SADC Bw. Elias Magosi amesema Wakuu wa Nchi na Serikali wameipongeza SADC kwa dhamira yake isiyoyumba ya kusimamia na kutetea amani na usalama, na kwa kutumia rasilimali zake katika kushughulikia na kupambana na ugaidi katika jimbo la Cabo Delgado.
Mkutano huo pia umepongeza hatua ya mshikamano iliyooneshwa kwa ahadi za chakula zilizotolewa na Jamhuri ya Malawi, Afrika Kusini na Zimbabwe ili kupunguza matatizo yanayowakabili wakimbizi katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.
Rais wa Jamhuri ya Malawi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Lazarus Chakwera akifunga Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC Msumbiji |
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC Msumbiji |
Mkutano ukiendelea |
Wakuu wa Nchi na Wawakilishi wa Wakuu wa nchi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC Msumbiji |
Wednesday, January 12, 2022
BALOZI MBAROUK ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI, KUKAGUA MALI ZA SERIKALI
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Ubalozi pamoja na kukagua mali za Serikali nchini humo.
Balozi Mbarouk mara baada ya kukagua mali za Serikali, aliushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kuendeleza kiwanja cha Serikali kwa kujenga jengo la Ubalozi na kitega uchumi.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba amemshukuru Mhe. Naibu wa Waziri – Nje kwa kutenga muda wa kutembelea Ofisi ya Ubalozi na kukagua mali za Serikali zilizopo Lilongwe, licha ya kuwa na ratiba ngumu ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akioneshwa kiwanja cha Serikali na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akikagua moja kati ya nyumba za Serikali zilizopo Lilongwe, nchini Malawi. Katika ukaguzi huo, Naibu Waziri ameambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Nchini Mawali na kupokelewa na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Benedicto Mashiba |
BALOZI MBAROUK KATIKA MKUTANO WA DHARURA BARAZA LA MAWAZIRI SADC
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameshiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Lilongwe, nchini Malawi.
Mbali na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali, pia mkutano huo ulitanguliwa na kikao cha Kamati ya Fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi na kuhudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali kutoka nchi wanachama wa SADC.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akishiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Lilongwe, nchini Malawi |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC Jijini Lilongwe, nchini Malawi |
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC ukiendelea Jijini Lilongwe nchini Malawi |
Mawaziri walioshiriki katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi |
BALOZI FATMA ASHIRIKI KIKAO KAMATI YA FEDHA SADC
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab ameshiriki katika kikao cha Kamati ya Fedha ya SADC kilichofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi.
Kikao hicho kimetanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji ulioanza tarehe 11 Januari 2021 Lilongwe, Malawi.
Katika Mkutano wa Dharuar wa Wakuu wa Nchi na Serikali, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika kikao cha Kamati ya Fedha ya SADC kilichofanyika Jijini Lilongwe, nchini Malawi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika kikao cha Kamati ya Fedha ya SADC
Tuesday, January 11, 2022
DKT. MPANGO AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA DHARURA MALAWI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango akifuatilia Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji. Mkutano umefanyika Lilongwe Malawi. Kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango akiongoza ujumbe wa Tanzania katika ukumbi wa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji leo Lilongwe, Malawi |
Baadhi ya Ujumbe wa Tanzania, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajab pamoja na Maafisa Waandamizi wa Serikali |
Rais wa Jamhuri ya Malawi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Lazarus Chakwera akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Bishara za Kimataifa wa Zimbabwe Balozi Frederick Shawa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji. Mkutano umefanyika Lilongwe, Malawi. |
Rais wa Jamhuri ya Malawi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Lazarus Chakwera akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji, Lilongwe, Malawi |
Wakuu wa Nchi na Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi walioshiriki katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya SADC, Jamhuri ya Msumbiji na Nchi zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyoko nchini Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa Mkutano huo leo Lilongwe, Malawi |
Friday, January 7, 2022
BALOZI SHIYO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA ETHIOPIA
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) Mhe. Innocent Shiyo akiwasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Sahle- Work Zewde |
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Sahle- Work Zewde akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) Mhe. Innocent Shiyo mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho |
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Sahle- Work Zewde katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) Mhe. Innocent Shiyo |
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia Mheshimiwa Sahle- Work Zewde na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika (UNECA) Mhe. Innocent Shiyo katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waliohudhuria hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho |