Tuesday, October 11, 2022

BALOZI FATMA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA WATAALAM WA UMOJA WA AFRIKA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab leo terehe 11 Oktoba 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063, jijini Dodoma.

Ujumbe huo (Technical Working Group on the Evaluation of Agenda 2063) unaoongozwa na Bi. Josephine Etima upo ziarani nchini kuanzia tarehe 10 hadi 14 Oktoba 2022, ambapo utakutana na wadau mbalimbali wa Serikali katika ngazi ya wakurugenzi kwa lengo la kupata maoni yao kuhusu mpango wa utekelezaji wa Agenda 2063 katika kipindi cha muongo mmoja wa kwanza. 

Bi. Josephine na ujumbe wake ambao ulikutana na Balozi Fatma kwa lengo la kuelezea kuhusu ziara yao nchini, amebainisha kuwa maoni yatakayo tolewa na wataalam kuhusu mpango wa utekelezaji wa kipindi cha miaka 10 ya kwanza yatawasaidia kubaini musuala muhimu zaidi ya kuzingatia wakati wa kuandaa mpango wa pili wa miaka 10 ya utekelezaji wa Agenda 2063. 

Kwa upande wake Balozi Fatma akizungumza na ujumbe wa wataalam hao ameelezea hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa nchini ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Agenda 2063. Ametaja baadhi ya maendeleo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mpango utoaji elimu bila malipo, uboreshwaji wa upatikanaji na usambazaji wa madawa na vifaa tiba na uboreshwaji wa huduma za afya vijijini. 

Mbali na hayo Balozi Fatma aliongeza kuwa jitihada zingine zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza Agenda 2063 ni pamoja na kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kuwahamasisha Diaspora kushiriki katika shughuli za maendeleo nchini. Vilevile ameeleza kuwa Wizara na Serikali kwa ujumla inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya biashara miongoni wa Waafrika wenyewe kupitia fursa zinazotokana na Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA). 

Agenda 2063 ambayo imebeba kauli mbiu isemayo “Afrika Tuitakayo” ("The Africa We Want") inalenga pamoja na mambo mengine kuliunganisha Bara la Afrika katika masuala ya kukuza uchumi; kuhamasisha utawala bora na utawala wa sheria; kuhakikisha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja; kuhakikisha amani na usalama unaimarika na kuiweka Afrika kwenye nafasi ya mchangiaji mkuu wa uchumi duniani
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kulia) akiwa katika mazungumzo na na Bi. Josephine Etima kiongozi wa ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063, yaliyofanyika jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kulia) akisalimiana na Bi. Josephine Etima kiongozi wa ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063 walipowasili Wizarani jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (mwenye kilemba) akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (mwenye kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063 (kulia kwa Balozi Fatma) na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje (kushoto kwa Balozi Fatma)
Mazungumzo yakiendelea
Mazungumzo yakiendelea

Monday, October 10, 2022

TAMKO LA PAMOJA KATI YA TANZANIA NA KENYA


 

                                       





 

TANZANIA KENYA ZAKUBALIANA KUENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipozungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akizungumza katika  Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Mhe. Rais Samia Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akizungumza katika  Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Mhe. Rais Samia Ikulu jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kabla ya kuanza kwa Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camilius Wambura akifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto baada ya kumalizika kwa  mazungumzo kati yao Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman (kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam.


 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi zao kwa manufaa ya pande zote mbili.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hayo Ikulu jijini Dar wa Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea walichojadili katika mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili  nchini .

 

Ziara hii ya Mhe. Ruto nchini, imetuwezesha kujadili na kuhuisha mahusiano yetu na kutupa nafasi ya kujitathmini mashirikiano baina ya Tanzania na Kenya, na tumekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano baina yan chi zetu, alisema Mhe. Rais

 

Amesema katika mazungumzo yao wamejadili masuala ya kimkakati kuhusiana na ushirikiano baina ya nchi hizo, kikanda na kimataifa na kuongeza kuwa wamekubaliana kukuza na kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Kenya.

 

Mhe. Rais Samia amesema Tanzania inajivunia kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi ambavyo vilikuwa vinazuia ufanyaji wa Biashara kati ya Tanzania na Kenya.

 

“Wakati naingia madarakani kulikuwa na vikwazo visivyo vya kodi 68, lakini sasa vimefanyiwa kazi na kubaki 14, ni matarajio yetu kuwa vikwazo vilivyobaki navyo vitamalizwa na hivyo kurahisisha ufanyaji biashara baina ya nchi zetu”, alisema Mhe. Rais.

 

Amesema wamekubaliana kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa Kenya kupitia Nairobi.

Amesema kuwa wamejadili jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa lengo la kuzifanya nchi zao kuwa sehemu salama  na kuongeza kuwa wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya kikanda na kimataifa na kukuza Jumuiya ya Afrika Mashariki Kama viongozi waanzilishi wa Jumuiya hiyo pamoja na nchi ya Uganda

 

Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Kenya Mhe. William Ruto amesema amedhamiria kuyafikisha mahusiano kati ya Tanzania na Kenya katika levo nyingine na dhamira hiyo itafanikiwa kutokana na utayari uliopo baina ya nchi hizo.

 

Amesema biashara kati ya Tanzania imekuwa ikiongezeka na viongozi hao wanadhamira ya kuongeza ufanyaji wa biashara baina ya Kenya na Tanzania na kufafanua kuwa biashara kati ya nchi hizo  imeongezeka na kuifanya Tanzania kuwa mnufaika mkubwa kuliko ilivyokuwa awali.

 

“Mauzo ya Tanzania nchini Kenya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi , kabla ya kuondolewa vikwazo visivyo vya kodi, sasa Kenya wananunua zaidi Tanzania kuliko ilivyo kuwa,” alisema

 

Amesema mauzo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 31 hadi shilingi bilioni 41 na biashara imekuwa kutoka shilingi bilioni 27 hadi shilingi bilioni 51 na hivyo kuleta picha kuwa Tanzania sasa inanufaika sana na ufanyaji wa biashara na Kenya.

 

Amesema wamekubaliana kuwa Mawaziri na wadau wengine wote wanaohusika na biashara wananakutana na kuzifanyia kazi changamoto zinazokabili sekta ya biashara baina ya nchi hizo ili wananchi waweze kufanya biashara .

 

Amesema uongozi wake utatilia mkazo na kuhakikisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es salaam hadi Mombasa unaharakishwa na kukamilika kwa wakati.

 

“Tutahakikisha tunatumia fursa ya ujenzi wa bomba la gesi kwenda Mombasa ili kuhakikisha tunatumia maliasili zetu na kuongeza ufanisi wa biashara na kuboresha maisha ya watu wetu, kuongeza na kuimarisha ushindani wa viwanda na wawekezaji wetu ,nchi zetu na ukanda wetu kwa ujumla

 

Amesema kukamilika kwa bomba hilo kutasaidia kukuza mpango wa viwanda katika nchi hizo na kuongeza kuwa utekelezaji wa mpango wa kuwa na mtandao mmoja kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kwani walishakubaliana na baadhi ya nchi kuwa na mtandao mmoja

 

“Tutahakikisha tunatekeleza mpango huo ili kuwafanya wananchi wetu waweze kufanya biashara na kuwasiliana kwa urahisi na kwa gharama nafuu na hivyo kuendelea kuimarisha mahusiano yetu,” alsiema

 

Amesema wamewaelekeza watendaji katika nchi zao kukutana na kuandaa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya kabla mwaka huu haujaisha ili kujadili namna ya kuendelea kutatua changamoto zilizopo na hivyo kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo

 

Amewaambia Watanzania wajue kuwa wana marafiki na ndugu kutoka Kenya na kuahidi kuwa watafanya kazi pamoja na kuongeza kuwa Tanzania na Kenya hawawezi gawana njaa bali watagawana utajiri na fursa ili kujenga umoja kwa manufaa ya nchi zote mbili na watu wake

 

Rais Ruto aliwasili nchini tarehe 09/10/2022  kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili na aliondoka nchini kurejea Kenya tarehe 10/10/2022


RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA RAIS RUTO IKULU DAR ES SALAAM

Mkuu wa Itifaki Tanzania Balozi Yusuph Mndolwa akiwa na Mkuu wa Itifaki Kenya Balozi Betty Cherwon wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto nchini  

 
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akizungumza wakati wa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan walipokutana Ikulu Dar es Salam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto  walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam   

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (katikati) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Dkt. Alfred Mutua (kushoto) wakati wa mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam 










 

RAIS DKT. RUTO ALIPOWASILI IKULU DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungno Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene  alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Azizi alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.


 

 

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Ruto na mke wake Mama Rachel Ruto wako nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili waliwasili nchini tarehe 09/10/2022 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Akiwa Ikulu Mhe. Dkt. Ruto alifanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na baadaye walikuwa na mazungumzo rasmi ambayo yalihudhuriwa na wajumbe wa pande zote mbili.

Viongozi hao walipomaliza mazungumzo yao walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia walichojadili kwa umoja wao.

Baadaye viongozi hao walielekea katika ukumbi maalum ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliandaa dhifa malum kwa ajili ya mgeni wake Mhe. Rais Ruto.

Baada ya dhifa hiyo Mhe. Rais Ruto na ujumbe wake waliondoka nchini kurejea Kenya.

Sunday, October 9, 2022

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini

 

 


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando  na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua  walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini



Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin.




 

 

 



Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.

Tarehe 10 Oktoba 2022 asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni wake Mhe. Dkt. Ruto.

baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Kenya.


TAARIFA KWA UMMA: RAIS RUTO KUWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI


 

Friday, October 7, 2022

DKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashriki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), amekutana na kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe.  Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara Mtumba, Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Mhe. Mkingule alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Mhe. Waziri na kumpongeza kufuatia uteuzi alioupata hivi karibuni na kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mhe. Mkingule pia alipokea maelekezo kutoka kwa Mhe. Waziri Dkt. Tax tayari kuelekea katika kituo cha kazi nchini Zambia.