Wednesday, February 15, 2023

DT. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 42 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023.  

Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 18-19 Februari 2023.

Pamoja na mambo mengine, mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya kimkakati yanayohusu Bara la Afrika ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika-AfCFTA, uhakika wa chakula, hali ya ulinzi na usalama, mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali za Umoja wa Afrika.

Akichangia katika mkutano huo, Dkt. Tax alisisitiza umuhimu wa Kamisheni na Taasisi za Umoja wa Afrika kusimamia vyema rasilimali za Umoja wa Afrika kwa kuchukua hatua za kuondoa mapungufu yaliyobainika kwenye taarifa ya ukaguzi wa rasilimali za Umoja wa Afrika. 

Mhe. Waziri pia alieleza hatua ambazo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua katika kutekeleza Mikataba ya Uenyeji ya Taasisi za Umoja wa Afrika zilizopo Tanzania ambazo ni Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Umoja wa Posta Afrika na Bodi ya Umoja wa Afrika ya Ushauri dhidi ya Rushwa.

Awali akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Moussa Faki Mahamat alisisitiza umuhimu wa Umoja wa Afrika kuendelea kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayowagusa wananchi wa Afrika ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za mabadiliko za kijamii, kiuchumi na kiusalama. Alisisitiza umuhimu wa Afrika kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za vyakula ndani ya bara la Afrika pamoja na kutumia fursa za mkataba wa AfCFTA katika kukuza Mtangamano wa Kiuchumi.

Bw. Faki aliongeza kuwa Umoja wa Afrika umeendelea kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika katika nchi za Ethiopia, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Libya ambapo jitihada zilizofanyika zimelenga zaidi kupata suluhisho la amani kwa mataifa hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen amesema Ethiopia ameshukuru Umoja wa Afrika kwa mchango na ushirikiano wake ambao umewezesha kupatikana amani na utulivu nchini Ethiopia na kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda wa miaka miwili. “Ethiopia inaamini kuwa kupitia Umoja wa Afrika amani, ulinzi na usalama vitailetea Afrika maendeleo zaidi,” alisema Mhe. Mekonnen.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, Mhe. Deng Dau Deng Malek katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Mhe. Demeke Mekonnen akijadili jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023 

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja

Mawaziri mbalimbali walioshiriki Mkutano wa 42 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja. Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa tarehe 15 – 16 Februari 2023. 





TANZANIA MWENYEKITI WA SEKTA YA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU KATIKA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI



 

Tuesday, February 14, 2023

MKUTANO WA MAJADILIANO YA KIMKAKATI YA NGAZI YA JUU KATI YA SERIKALI NA WADAU WA MAENDELEO WAFANYIKA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Sterrgomena Tax wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

 Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo katika meza kuu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.


Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki balozi Joseph Sokoine (wa pili kulia) akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo  uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifuatilia Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023.

Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 ukiendelea.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 katika picha ya pamoja.

Meneja ratiba wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakti ya Ngazi ya Juu kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salam tarehe 14 Februari, 2023 bi Ellen Maduhu akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kuzungumza katika mkutano huo.



Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati ya Ngazi ya Juu ulioshirikisha watendaji wakuu wa Serikali na wadau wa maendeleo wafanyika jijini dar es Salaam.

Akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amewahakikishia wadau wa maendeleo ushirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja mipango ya maendeleo.

Balozi Mbarouk amesema kufanyika kwa kikao hicho kunadhihirisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wa maendeleo na Taasisi za Umoja wa Mataifa.

“Uwepo wenu hapa katika kikao hiki unadhihirisha ushirikiano usliopo kati ya Tanzania na wadau wa maendeleo, Sio kwamba uwepo wenu unachochea ubia wetu na kuimarisha nia yenu ya kuhakikisha tunatekeleza kikamilifu Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo ambao umelenga kutekeleza malengo Endelevu ya Milenia ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya Addis Ababa ya kuchangia maendeleo na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Balozi Mbarouk

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye uwakilishi wao hapa nchini, wadau wa maendeleo , sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikal.

 

 


TANZANIA, COMORO KUANZIASHA TUME YA KUDUMU YA PAMOJA

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakisaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili.  Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakionesha Mkataba wa Makubaliano (MoU) uliosainiwa kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakionesha Mkataba wa Makubaliano (MoU) uliosainiwa kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro, Mhe. Dhoihir Dhoulkamal katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Comoro baada ya kusaini Mkataba wa kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Comoro. Mkataba huo umesainiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, Ethiopia.



Saturday, February 11, 2023

TANZANIA, IRAN KUSHIRIKIANA SEKTA ZA KIMKAKATI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeahidi kushirikiana katika sekta za kimkakati hususani kilimo, pamoja na biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza na kuimarisha diplomasia ya uchumi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam.

“Tanzania na Iran tumekuwa tukishirikiana katika maeneo mbalimbali, hadi sasa tumekuwa tukishirikiana katika sekta za elimu, afya, utalii, nishati, madini. Pia kwa sasa Irani imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa ukizingatia kilimo ni kipaumbele cha Serikali,” alisema Dkt. Tax

Waziri Tax ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Iran katika maeneo mapya ya kimkakati ikiwemo sekta ya kilimo ili kupata uzoefu katika maendeleo na uwekezaji wa kuifanya nchi kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha pamoja na kuongeza viwanda. 

Akielezea kuhusu biashara na uwekezaji, Dkt. Tax alisema kuwa kupitia kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji lililofanyika Mwezi Agosti, 2022 limefungua fursa za biashara na uwekezaji. “Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi kuwekeza nchini,” alisema Dkt. Tax

Naye Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh alisema kuwa Iran imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania kwa miaka 40 hadi sasa na mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana kijamii, kisiasa, kiuchumi na utamaduni kwa maslahi ya pande zote mbili.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania zimekuwa marafiki wa muda mrefu na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha sekta za kilimo, elimu, afya pamoja na biashara na uwekezaji kwa maslahi ya mataifa yote mawili.

Balozi Alvandi aliongeza kuwa mazingira ya biashara kati ya Iran na Tanzania yanaridhisha kwani hadi mwaka jana 2022 biashara kati ya Iran na Tanzania iliongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70.

“Biashara kati ya Iran na Tanzania imeongezeka kutoka dola milioni 20 hadi dola milioni 70 mwaka jana, hii ni ishara kuwa uchumi wa mataifa yetu mawili unazidi kuimarika,” alisema Balozi Alvandi 

Tanzania na Iran zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1983 na zimekuwa zikishirikiana katika sekta za biashara, kilimo, masoko, utalii, uwekezaji, afya, madini, nishati na utaalamu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwasiliha hotuba yake katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwa amesimama na Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh katika sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam

Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza katika maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya washiriki wakifuatilia maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akikata keki pamoja na Balozi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakati wa maadhimisho ya miaka 44 ya siku ya Taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Iran na Tanzania zilizofanyika tarehe 10 Februari 2023 Jijini Dar es Salaam



WAZIRI TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA MISRI, MAREKANI

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi mteule wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi mteule wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Friday, February 10, 2023

DKT. TAX ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UTURUKI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki tarehe 6 Februari, 2023.

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dkt. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.

“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.

Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo. Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam








TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaofanyika jijini Bujumbura, Burundi 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu

Mkutano huo ulianza tarehe 6 - 8 February 2023 kwa ngazi ya wataalamu waandamizi, ulifuatiwa na kikao cha ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika tarehe 9 Februari 2023 na utakamilishwa kwa kuwakutanisha Mawaziri katika kikao kitakachofanyika tarehe 10 Februari 2023 jijini humo. 

Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu umepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa Programu na Miradi; Maamuzi; na Maagizo ya Mikutano ya awali katika sekta za Mawasiliano; Hali ya Hewa na Miundombinu ya Uchukuzi inayojumuisha sekta za Barabara, Vituo vya Huduma kwa pamoja Mipakani (OSBP), Reli, Usafiri wa anga na Bandari kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Mkutano huo pia ulipokea taarifa ya utekelezaji wa Maagizo 12 kati 34 ya mikutano ya awali ya Baraza la Mawaziri wa sekta husika yaliyokamilika na maagizo mengine yaliyosalia utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali. 

Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia sekta za ujenzi, uchukuzi, mawasiliano na fedha.
 Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) ukiendelea jijini Bujumbura, Burundi 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Balozi Jilly Maleko
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma M. Rajabu (kushoto) akifuatilia Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) unaoendelea jijini Bujumbura, Burundi

Thursday, February 9, 2023

TANZANIA YAJIZATITI KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA NDANI NA NJE YA NCHI KUKUZA UCHUMI


Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kushirikiana na nchi mbalimbali duniani ili kukuza  uchumi wa nchi kupitia fursa za biashara, uwekezaji na utalii zilizopo ndani na nje ya nchi.

 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Bungeni leo tarehe 09 Februari,2023 wakati akijibu swali la  Mhe. Felista Njau, Mbunge wa Viti Maalum kuhusu umuhimu wa Serikali wa kuainisha nchi zenye fursa za biashara na uwekezaji ili kukuza pato la Taifa.

 

Amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Wizara za kisekta na Balozi za Tanzania imeendelea kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zenye manufaa kwa Taifa na kwamba Wizara inaandaa Mpango wa Kitaifa wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi utakaojumuisha Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kufikia malengo tarajiwa. 

 

Amesema Mpango huu ambao unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba 2023, pamoja na mambo mengine unalenga kuhakikisha fursa za biashara, uwekezaji na utalii zinakuwa na tija zaidi kwa wananchi wa Tanzania. Pia Mpango huo utajumuisha Sekta zote husika ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo muhimu ya kisekta yatakayo changia katika kukuza uchumi na pato la Taifa.

 

Akichangia hoja kuhusu mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi kuhusu dhana ya Diplomasia ya Uchumi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali na kufafanua kwamba Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi unaoandaliwa pia utajumuisha Mpango  wa kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo ili kuwawezesha wananchi kuielewa dhana hii na kuwawezesha kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.


Kuhusu taarifa hasi zinazotolewa na vyombo vya kimataifa dhidi ya Tanzania, Mhe. Dkt. Tax amesema tayari Wizara imeanza kushirikiana na vyombo vya habari vya Nje hususan vile vinavyorusha matangazo yake kwa Kiswahili ili kupitia vyombo hivyo fursa  na taarifa chanya kuhusu Tanzania zitangazwe duniani kote.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akichangia hoja kuhusu Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi wakati wa kipindi cha maswali na majibu kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma tarehe 09 Februari, 2023
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akijibu swali bungeni jijini Dodoma tarehe 09 Februari 2023
 

Wednesday, February 1, 2023

BALOZI LUVANDA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO, NEW ZEALAND

Balozi wa Tanzania nchini New Zealand mwenye makazi yake Tokyo, Japan, Mhe. Baraka Luvanda akisalimiana na Gavana Jenerali na Amiri Jeshi Mkuu wa New Zealand, Mhe. Cindy Kiro kabla ya zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho lililofanyika tarehe 31 Januari 2023. 

Balozi wa Tanzania nchini New Zealand mwenye makazi yake Tokyo, Japan, Mhe. Baraka Luvanda akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Gavana Jenerali na Amiri Jeshi Mkuu wa New Zealand, Mhe. Cindy Kiro kwenye hafla iliyofanyika kwenye makazi ya Gavana huyo tarehe 31 Januari 2023. 

Balozi wa Tanzania nchini New Zealand mwenye makazi yake Tokyo, Japan, Mhe. Baraka Luvanda akiweka saini Kitabu cha Wageni alipowasili kwenye Makazi ya Gavana Jenerali na Amiri Jeshi Mkuu wa New Zealand, Mhe. Cindy Kiro kuwasilisha Hati za Utambulisho 

Balozi wa Tanzania nchini New Zealand mwenye makazi yake Tokyo, Japan, Mhe. Baraka Luvanda (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana Jenerali na Amiri Jeshi Mkuu wa New Zealand, Mhe. Cindy Kiro (katikati) baada ya hafla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho iliyofanyika kwenye makazi ya Gavana huyo tarehe 31 Januari 2023.