Wednesday, April 19, 2023

WATANZANIA WALIOPO SUDAN WAPO SALAMA: DKT. TAX


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akitoa Taarifa ya Serikali kuhusu Hali ya Amani na Usalama nchini Sudan Bungeni jijini Dodoma, tarehe 19 Aprili 2023 

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuchukua hatua stahiki kwa kushirikiana na nchi jirani, Jumuiya za Kikanda, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ili kuhakikisha watanzania na raia wengine waliopo nchini Sudan wanakuwa salama wakati huu ambapo nchi hiyo ipo katika changamoto za kiusalama.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax Bungeni jijini Dodoma, tarehe 19 Aprili 2023 wakati akitoa Taarifa ya Serikali kuhusu Hali ya Amani na Usalama nchini Sudan.

 

Amesema tangu kuibuka kwa mapigano mjini Khartoum tarehe 15 Aprili 2023 kati ya vikosi vya Serikali (Sudan Armed Forces - SAF) na Vikosi vya Msaada yaani Rapid Support Forces (RSF) na kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza ikwemo vifo vya watu 185 majeruhi zaidi ya 1,000 na uharibifu wa mali.

 

Amesema mapigano hayo pia yamechangia kurudisha nyuma jitihada zinazoendelea za kutafuta amani Sudan na kwamba Serikali ya Tanzania inasikitishwa na kuzorota kwa hali ya amani na usalama inayoendelea nchini humo.

 

Ameongeza kusema Tanzania kama zilivyo nchi nyingine inao raia wake wapatao 210 nchini Sudan wakiwemo wanafunzi 171, wanadiplomasia na raia wengine ambao hadi sasa wapo salama na hakuna aliyeathiriwa na mapigano hayo.

 

 

Mhe. Dkt. Tax amesema kuwa, jitihada za pamoja za Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi na taasisi mbalimbali zimefanikisha kusitishwa kwa mapigano nchini Sudan kwa muda wa saa 24 kuanzia tarehe 18 Aprili 2023 jioni ili kutoa nafasi kwa misaada ya kibinadamu kutolewa kwa raia.

 

Pia  Mhe. Dkt. Tax amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Sudan, Mhe. Silima Haji Kombo kwa kuendelea kuhakikisha usalama wa watanzania waliopo Sudan na kwamba Serikali inaendelea kufuatilia hali nchini humo pamoja na kuandaa mpango wa kuwaondoa raia wa Tanzania kadri itakavyohitajika.

 

Amesema  Tanzania ambayo ni Mjumbe wa Baraza la Amani la Afrika inaendelea kuunga mkono tamko lililotolewa na Baraza hilo katika mkutano wake uliofanyika tarehe 16 Aprili 2023 la kulaani mapigano yanayoendelea na kutoa wito kwa pande zote mbili katika mgogoro huo kusitisha mapigano hayo.

 

Pia Tanzania inaendelea kuzitaka pande hizo mbili hasimu kutatua mgogoro huo kwa njia za amani na usalama huku zikihakikisha mahitaji ya kibinadamu, usalama na ustawi wa raia wa Sudana na raia kutoka nchi nyingine.

 

 

TUSAMBAZE ELIMU YA UKUZAJI VIUMBE MAJI NCHI NZIMA - BALOZI MLIMA

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Bi. Judith Ngoda (kulia) akimuelezea Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz Mlima (hayupo pichani) kuhusu Mkutano wa Tano Baraza la Mawaziri la kisekta la Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji la Jumuiya ya Afrika Mashariki waliofika Ubalozini kumpa taarifa kuhusu mkutano huo unaoendelea jijini Kampala, Uganda, kushoto ni Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Didas Clemence


Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz Mlima (wa pili kulia ) katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Tano Baraza la Mawaziri la kisekta la Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji la Jumuiya ya Afrika Mashariki waliofika Ubalozini kumpa taarifa kuhusu mkutano huo unaoendelea jijini Kampala, Uganda



 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz Mlima ameisihi sekta ya uvuvi nchini kuangalia namna ya kufanya ili juhudi za ukuzaji viumbe maji zisambae nchi nzima.

Mhe. Balozi Mlima ametoa rai hiyo jijini Kampala alipozungumza na washiriki wa Mkutano wa Tano Baraza la Mawaziri la kisekta la Uvuvi Ukuzaji Viumbe Maji la Jumuiya ya Afrika Mashariki waliofika Ubalozini kumpa taarifa kuhusu mkutano huo unaoendelea jijini Kamapala.

Akizungumza na wataalamu hao Mhe. Balozi Dkt. Mlima amesema sekta ya Uvuvi kupitia eneo la ukuzaji viumbe maji lazima ihakikishe programu za ufugaji samaki zinaenea katika maeneo mengine yenye maziwa na isiishie maeneo ya Ziwa Victoria pekee ili nchi itumie fursa hiyo vizuri na kunufaika nayo.

“Tanzania tuna eneo kubwa la maji lakini ufugaji wa samaki kwetu sio mzuri Inabidi tuoneshe njia, suala hili linatoa ajira na lina soko kubwa niwaambie tu kuwa bidhaa zitakazozalishwa soko liko DRC,” alisema na kuongeza kuwa Tanzania lazima kufanya ufugaji samaki kuwa suala la kimkakati.

Amesema kinachotakiwa kufanywa au kuangaliwa ni suala la kuzalisha chakula cha samaki ili kuwa na uhakika wa malisho yao na hapo mambo yataenda vizuri kwani suala la kutengeneza chakula ni kubwa na ana hakika chuo cha uvuvi na Taasisi ya Utafiti ya uvuvi wanaweza kusimamia eneo hilo.

Amesema sekta inabidi ioneshe njia na kutilia mkazo suala la ufugaji wa samaki nchini kwani ajira nyingi zitatengenezwa katika eneo hilo na kwa kuzingatia kuwa kuna soko kubwa kwa nchi jirani ya DRC na hivyo nchi itanufaika na fursa hii kuwa na mashine za uhakika za uzalishaji wa chakula cha Samaki

“Tuangalie na tufanye suala hili kimkakati hasa katika eneo la kutengeneza chakula cha samaki ni suala kubwa na la msingi, nina hakika chuo cha uvuvi na taasisi ya utafiti wakilisimamia hili tutapata mitambo ya kuzalisha chakula cha samaki.

Amesema anaona ufugaji Samaki ukizingatia masharti na vigezo vyake ni kitu rahisi kwa mwananchi kufanya kwakua changamoto pekee inayoweza kumsumbua mfugaji husika ni wizi wa mazao yake tu na kwamba akijipanga kudhibiti hilo hakuna shida nyingine kama ana uhakika wa chakula bora.

Mhe.Balozi Dkt. Mlima atashiriki katika Mkutano huo utakaofanyika tarehe 19 Aprili akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo utaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo Prof. Riziki Shemdoe kwa ngazi ya Makatibu Wakuu.






Tuesday, April 18, 2023

KAMATI KUTATHMINI UTEKELEZJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI YAANZA KAZI RASMI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Kamati ya Kutathmini Utendaji wa Wizara alipokutana nayo jijini Dodoma tarehe 18 Aprili 2023 kama ishara ya kuanza rasmi kwa kazi ya Kamati hiyo. Kamati hiyo ambayo iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Machi, 2023 inao wajumbe saba (7) na inaongozwa na Balozi Msatafu, Mhe. Hassan Simba Yahya (wa kwanza kushoto)
Kikao na Kamati kikiendelea
Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianio wa Afrika Mashariki, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiwa kwenye Kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax. Kushoto ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) na Balozi Peter Kalaghe wakati wa kikao kati ya kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax

Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka (kulia) akiwa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati (kushoto)
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Tuvako Manongi (kushoto) na Mhe. Balozi George Madafa wakati wa kikao kati ya Kamati na Mhe. Waziri Tax
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza), Wajumbe wa Kamati pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo


STATEMENT BY THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, ON THE SECURITY SITUATION IN THE REPUBLIC OF SUDAN


 

Monday, April 17, 2023

TANZANIA - WADAU WAMAENDELEO KUENDELEA KUSHIRIKIANA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameeleza utayari wa Serikali ya Awamu ya Sita chini na usimamizi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuboresha maisha ya wananchi. 

Waziri Tax ameeleza hayo leo tarehe17 Aprili 2023 alipokutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary O’Neill, na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Zlatan Milisic jijini Dodoma. 

Waziri Tax akizungumza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Milisic ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita yamefayika madiliko na maboresho makubwa yanayolenga kukuza Demokrasia na Utawala Bora na Haki za Binadamu. 

Waziri Tax sambamba na kumshukuru Bw. Malisic kwa kuendelea kusaidia programu mbalimbali za maendeleo nchini, aliongeza kusema mafanikio yaliyopatikana katika kuboresha maeneo hayo yameendelea kuwavutia wadau wa maendeleo kuwekeza na kusaidia katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini. 

“Dunia imeendelea kushuhudia kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha hali ya Demokrasia na Utawala Bora nchini, hali hii imeendelea kuwavutia wadau wengi wa maendeleo kushirikiana na Tanzania; na Serikali ya Tanzania inaahidi kuendelea kushikiana na wadau wote katika kuondoa umaskini na kuboresha maisha ya Wananchi” ameeleza Dkt. Tax.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Milisic amepongeza juhudi zilizofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha hali ya Demokrasia na Utawala Bora nchini, huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali kupitia nyanja mbalimbali ili kuendelea kuboresha hali ya maisha ya Wananchi.

Wakati huohuo Waziri Tax ameipongeza na kuishukuru Serikali ya Ireland kupitia Balozi wake nchini Mhe. O’Neil kwa kuendelea kufadhili programu na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya kuondoa umaskini kupitia TASAF. 

Kwa upande wake Balozi O’Neil ametoa pongezi na kueleza kuridhishwa kwake na namna Serikali ya Tanzania inavyojidhatiti katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijami kwa wananchi huku ikizingatia na kufuata misingi ya Utawala Bora, huku akitolea mfano usimamizi mzuri wa progamu na miradi ya kuondoa umaskini nchini kupitia TASAF. 

Kadhali Waziri Tax alitumia fursa hiyo kumweleza Balozi wa Ireland Mhe. O’Neill kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ireland kuwezekeza nchini katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda na uchumi wa buluu. 

MKUTANO WA TANO WA BARAZA LA MAWAZIRI LA SEKTA YA UVUVI NA UKUZAJI VIUMBE MAJI WA EAC WAANZA KAMPALA, UGANDA


Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Kampala, Uganda tarehe 17-21 Aprili, 2023

Meza Kuu ikiongoza Mkutano wa Maafisa Waandamizi wakati wa Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023 ikiongozwa na mwenyeji Uganda na Katibu wa Sekretarieti ya LVFO

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023
Ujumbe wa Jamhuri ya Kenya katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023

Ujumbe wa Jamhuri ya Burundi katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023
Ujumbe wa Jamhuri ya Uganda katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023



Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023.

Mkutano huo umeanza kwa kuwakutanisha Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda unafanyika tarehe 17 - 18 Aprili 2023. 

Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 19 Aprili 2023 na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 20 - 21 Aprili 2023.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Maafisa Waandamizi unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla. Aidha, ujumbe wa Tanzania unajumuisha ushiriki wa maafisa  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania

Katika kikao hicho, maafisa waandamizi wanajadili na kuandaa nyaraka zitakazojadiliwa katika kikao cha Makatibu Wakuu kinachotarajiwa kufanyika tarehe 19 Aprili 2023 kitakachojadili taarifa nyingine na kupitia utekelezaji wa maamuzi/maagizo ya mikutano iliyopita na Utekelezaji wa Program na Miradi ya Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe maji katika Ziwa Victoria.

Ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha Makatibu Wakuu unatarajiwa kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe na kujumuisha ushiriki wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz Mlima ambaye atamuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

Tarehe 20 - 21 Aprili 2023 kitafanyika kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho pamoja na mambo mengine kitakamilisha Mkutano wa Nne ulioishia ngazi ya Makatibu Wakuu, kupitia, kujadili na kuridhia taarifa ya kikao cha Makatibu Wakuu itakayowasilishwa katika kikao hicho.

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kikao cha Mawaziri unatarajiwa kuongozwa na Naibu Waziri wa  Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa David Silinde.

 

 

      

 

 


Ujumbe wa Jamhuri ya Burundi katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023

 

Ujumbe wa Jamhuri ya Uganda katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 17-21 Aprili 2023
 







Friday, April 14, 2023

MFUMO WA KIELEKRTONIKI WA KUSAJILI DIASPORA KUKAMILIKA MWEZI JUNI 2023 - BALOZI MBAROUK

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipojibu swali la Mhe. Dennis Lazaro Londo, Mbunge wa Mikumi aliyetaka kujua idadi ya Diaspora wa Tanzania na mchango wao katika uchumi wa nchi


 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inakamilisha mfumo wa Kidigitali wa uandikishaji wa Diaspora unaotarajiwa kukamilika mwezi June 2023 ili kuwezesha ukusanyaji endelevu wa takwimu za Diaspora.

 

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma tarehe 14 Aprili 2023 na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipojibu swali la Mhe. Dennis Lazaro Londo, Mbunge wa Mikumi aliyetaka kujua idadi ya Diaspora wa Tanzania na mchango wao katika uchumi wa nchi.

Mhe. Balozi Mbarouk amesema Diaspora kama walivyo raia wengine wa Tanzania wana mchango mkubwa kwa  uchumi wa nchi na maendeleo kwa ujumla kupitia shughuli mbalimbali wanazozifanya ikiwemo utumaji wa fedha za kigeni nchini (remittances), uwekezaji, kuleta mitaji, utaalam na teknolojia ambayo huchangia katika kukuza uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma mbalimbali zenye tija kiuchumi.

Ameongeza kuwa, Diaspora pia wanachangia uchumi wa nchi kwa kutangaza fursa za kiuchumi, biashara, utalii na uwekezaji zinazopatikana nchini na kwamba kwa mujibu wa taarifa kutoka Balozi za Tanzania na maeneo yake ya Uwakilishi, hadi sasa idadi ya Diaspora wa Tanzania ni Milioni 1.5.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la utumaji wa fedha za kigeni nchini kutoka kwa Diaspora hadi kufikia Shilingi Trilioni 2.6 mwezi Desemba 2022.

 

“Diaspora huchangia katika maendeleo ya nchi kwa kutuma fedha za kigeni nchini (Remittances); kuwekeza, kuleta mitaji, utaalamu na Teknolojia inayoweza kuchangia kukuza uzalishaji wa mazao, bidhaa na huduma mbalimbali zenye tija kiuchumi. Mathalan katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2022, Diaspora walituma nchini kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 1.1 sawa na Shilingi Trilioni 2.6. Vilevile, katika kipindi hicho Diaspora wamewekeza kupitia ununuzi wa nyumba na viwanja wenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.4 na ununuzi wa Hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5” amesema Balozi Mbarouk. 

 

DKT. TAX AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MSUMBIJI

 




Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joaquim Chisano akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax aliyefika kumsalimia. Mhe Chisano yuko nchini kwa mwaliko wa kushiriki utoaji wa Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwl. Nyerere uliyofanyika  tarehe 13 Aprili, 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joaquim Chisano walipokutana jijini Dar es Salam kwa mazungumzo. Mhe Chisano yuko nchini kwa  mwaliko wa kushiriki utoaji wa Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwl. Nyerere uliyofanyika  tarehe 13 Aprili, 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joaquim Chisano walipokutana jijini Dar es Salam kwa mazungumzo. Mhe Chisano yuko nchini kwa  mwaliko wa kushiriki utoaji wa Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwl. Nyerere uliyofanyika  tarehe 13 Aprili, 2023.
mazungumzo yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Joaquim Chisano walipokutana jijini Dar es Salam kwa mazungumzo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chisano jijini Dar es Salam.

Mhe.Dkt. amemshukuru Mhe. Chisano kwa kukubali mwaliko wa kuja kushiriki utoaji wa Tuzo za Taifa za Uandishi Bunifu za Mwl. Nyerere zilizofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Aprili, 2023.

“Mhe. Chisano naomba nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kitendo cha kukubali kuja nchini na kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo uliofanyika jana, tunakushukuru sana na karibu tena Tanzania,” alisema Dkt Tax.

Amesema kitendo hicho kinaonesha uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji na pia kunaongeza jitihada za kuitangaza lugha ya Kiswahili katika bara la Afrika na Duniani kwa ujumla

 

NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA SLOVENIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon na ujumbe wake amewasili nchini tarehe 13 Aprili 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kukuza uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na Slovenia sambamba na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Waziri Fajon katika siku yake ya kwanza nchini amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax jijini Dodoma, ambapo mazunguzo yao yalijikita kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kuanisha maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Slovenia. 

Mazungumzo hayo pia yalihusisha uandaaji wa mazingira na utaratibu wa kusainiwa kwa Hati za Makubaliano katika maeno mapya ya ushirikiano yaliyoainishwa. 

Maeneo mapya ya ushirikiano yaliyoibuliwa wakati wa mazungumzo hayo ni uzalishaji dawa (pharmaceuticals), usimamizi wa rasilimali maji, utunzaji wa mazingira, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, sayansi na teknolojia, kilimo, Elimu,biashara na uwekezaji. 

Mbali na hayo Waziri Dkt. Tax alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Fajon kuhusu juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mafanikio yaliyopatikana nchini kutokana na juhudi hizo ikiwemo kupatikana kwa maridhiano ya kisiasa, kuimarika kwa Demokrasia, Haki za Banadamu, uhuru wa vyombo vya habari na uzingatiwaji wa usawa wa jinsia katika maendeleo.

Waziri Fajon kwa upande wake ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kuboresha mazingira ya Demokrasia na Utawala Bora nchini sambamba na kuendelea kusimamia vyema maendeleo ya uchumi licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali duniani zinazo dhoofisha ustawi wa uchumi. 

Ziara hii ni muendelezo wa matokeo ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mataifa mengine duniani. 

Waziri Fajon akiwa nchini anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi mbalimbali Serikalini.
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimpokea Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe.Tanja Fajon alipowasili katika Ofisi ya Wizara Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon wakiwa katika picha ya pamoja punde baada kuwasili Wizarani Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe.Tanja Fajon walipokuna kwa mazungumzo katika jijini Dodoma
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe walioambatana nao. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme akifuatilia mazungumzo yaloyokuwa yakiendelea baina ya Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon yaliyofanyika jijini Dodoma
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon yakiendelea.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Waziri Dkt. Tax na Waziri Fajon (hayupo pichani)
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (hayupo pichani). 
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akifafanua jambo alipokuwa katika mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon (hayupo pichani)

Thursday, April 6, 2023

SERIKALI YAAINISHA MAFANIKIO ZAIRA YA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI NCHINI

Serikali imewasihi watanzania kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuliletea maendeleo taifa. 

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alipozungumza na waandishi wa Habari kuelezea mafanikio ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris aliyoifanya nchini tarehe 29 – 31 Machi, 2023.

Dkt. Tax amesema ziara ya Mhe.Kamala Harris, nchini imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kuitangaza Tanzania duniani.  

Amesema kupitia ziara hiyo, Serikali ya Marekani ilitoa ahadi mbalimbali kwa Serikali ya Tanzania na Mikataba na Hati za Makubaliano kusainiwa ambapo Serikali ya Marekani itajenga kiwanda kikubwa nchini kitakachokuwa cha pekee barani Afrika.  Kiwanda hicho cha kuchakata madini ya Nikel yanayotumika kutengenezea betri za gari za umeme kwa ajili ya soko la Marekani na duniani ifikapo mwaka 2026. 

Amesema mradi huo unatarajiwa kutekelezwa na Kampuni ya Life Zone Metals na kampuni ya TechMet zinazomilikiwa kwa ubia na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (DFC).  Ameongeza kuwa kiwanda hicho kitatoa ajira kwa watanzania na kuchangia katika pato la Taifa.

Dkt. Tax alisema Amesema Mkataba wa Msaada wa Maendeleo kati ya Tanzania na Serikali ya Marekani kupitia USAID wa Dola za Marekani bilioni 1.1 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ulisainiwa.

“Mkataba wa Msaada wa Maendeleo kati ya Tanzania na Serikali ya Marekani kupitia USAID wa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.1 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ulisainiwa; na Hati ya Makubaliano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani ilisainiwa pia. Kupitia Makubaliano hayo Serikali ya Marekani itatoa ushauri wa kitaalam na kujenga uwezo kwa wataalam kuhusu usimamizi wa bandari za Tanzania, hususan katika upanuzi wa bandari, vifaa vya kisasa na uendelezaji wa Bandari,” alisema Dkt. Tax.

Dkt. Tax aliongeza kuwa pamoja na Mkataba huo na Hati za Makubaliano hizo zilizosainiwa, Tanzania itanufaika kupitia ahadi mbalimbali ikiwemo Serikali ya Marekani kuahidi kutoa nyongeza ya Dola za Marekani milioni 1.3 kupitia Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya kuendelea kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Serikali ya Marekani itatoa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.0 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake wa Afrika walio katika sekta ya Umma, na sekta binafsi kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii; Serikali ya Marekani kuingia Makubaliano na Tanzania yatakayowezesha Marekani kuuza bidhaa za usafirishaji, uchukuzi, teknolojia ya digitali na nishati safi zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 500.

Serikali ya Marekani kupitia USAID itatoa Dola za Marekani 600,000 kwa ajili ya kushirikiana na kampuni za mawasiliano na teknolojia ya sekta binafsi na Serikali ili kupanua huduma za nishati safi na kutoa umeme kwa takriban vituo 100 vya afya katika maeneo ya magharibi, kati, na kusini mwa Tanzania. Mradi huo utawezesha kampuni za mawasiliano ya simu kuimarisha huduma za takwimu na kuwezesha vituo vya afya kutumia mifumo ya kidijitali kutoa huduma.

Serikali ya Marekani kuendelea kuwekeza katika Mpango wa Dharura wa Rais wa Kusaidia UKIMWI (PEPFAR) na Tanzania kuendelea kunufaika ambapo Marekani inapanga kuwekeza Dola za Marekani milioni 433 katika kipindi cha miaka miwili ijayo. 

Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Rais wa kupambana na Malaria kutenga kiasi cha Dola za Marekani milioni 39 kwa mwaka 2024. Mradi huo unalenga kupambana na malaria ikiwa ni pamoja na kusambaza vyandarua, dawa za malaria, vifaa vya uchunguzi wa haraka wa malaria na dawa za kuzuia malaria kwa wajawazito ambapo Tanzania itaendelea kunufaika.

Serikali ya Marekani itatenga Dola za Marekani milioni 16.4 katika Bajeti ya Marekani ya Mwaka 2024 kwa ajili ya kuendeleza demokrasia, haki, na programu za utawala nchini. 

Vilevile Serikali ya Marekani kupitia USAID inatarajia kutoa Dola za Marekani milioni 1 za ziada kwa ajili ya programu ambazo utekelezaji wake utaanza mwaka huu.

Serikali ya Marekani kuipatia Tanzania kiasi cha Dola za Marekani milioni 1 kwa ajili ya miradi inayolenga kuondoa vikwazo vya uhuru wa kujieleza kwa umma na vyombo vya habari vya Tanzania na Serikali ya Marekani itatoa Dola za Marekani 400,000 kusaidia kazi ya Kituo cha Demokrasia kuleta pamoja wadau kujadili mageuzi zaidi ya kidemokrasia na sheria na kuwajengea uwezo vijana kushiriki kwenye shughuli za kisiasa.

Mafanikio mengine ni Serikali ya Marekani kutoa Dola za Marekani milioni 16 kwa ajili ya mpango wa Kilimo Tija unaolenga kusaidia wakulima nchini, hususan wanawake na vijana katika kukabiliana na changamoto za usalama wa chakula; na Tanzania na Marekani kuanzisha majadiliano ya kuongeza muda wa ukomo wa visa (Visa ya miaka mitano).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) mafanikio ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris aliyoifanya nchini tarehe 29 – 31 Machi, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) mafanikio ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris aliyoifanya nchini tarehe 29 – 31 Machi, 2023



SERIKALI YAIHAKIKISHIA JUMUIYA YA KIMATAIFA IMEDHIBITI UGONJWA WA MARBURG

Serikali kupitia Wizara za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Afya imekutana na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na taasisi zao hapa nchini  na kuwatoa hofu juu ya ugonjwa wa Mabarg ambao tayari umedhibitiwa.

Akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa wa marbug tangu ulipoanza na hadi sasa hakuna maambukizi mapya.

“Napenda kuwatoa hofu Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kuwa Tanzania ni salama na hivyo tuendelee kufanya kazi zetu kama kawaida kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya,” alisema Dkt. Tax 

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu amesema tangu ugonjwa huo ulipoibuka Serikali imechukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo na hadi sasa hakuna maambukizi tena.

“Jumla ya visa vya ugonjwa huo vimebaki 8 na kati yao watu 5 wamefariki ,watatu wanaendelea na matibabu na mgonjwa mmoja ameruhusiwa na wagonjwa waliolazwa wanaendelea vizuri,” alisema Prof. Nagu

Kwa Upande wake Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comorro nchini, Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed ameipongeza Serikali kwa hatua ilizochukua za kutoa taarifa za ugonjwa wa Maburg kwa wakati.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua ilizochukua kuukabili ugonjwa wa Maburg ikiwemo utoaji sahihi wa taarifa, elimu kwa umma kuhusu ugonjwa huo,” alisema Dkt. El Badaoui Mohamed.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comorro nchini, Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed (kushoto) na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu (kulia)

Balozi wa Marekani Nchini, Mhe. Michael Battle akichangia jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Maj. Gen. Charles Karamba akichangia jambo wakati wa mkutano 

Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Regina Hess akichangia jambo wakati wa mkutano 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akieleza jambo kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa mkutano















VACANCY ANNOUNCEMENT