Monday, October 30, 2023

BALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA

 





Balozi wa Tanzania Nchini Algeria Mhe. Iman Njalikai amekutana na kuzungumza na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha Ukombozi ambaye alikuwa Balozi wa Kwanza wa Algeria nchini Tanzania Mhe. Noureddine DJoudi .

Mazungumzo na Balozi huyo mwenye historia na kumbukumbu kubwa ya uhusiano wa Algeria na Tanzania yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers.

Mheshimiwa Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na Serikali ya Algeria.

Katika mazungumzo yao Balozi Njalikai alimshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya Ubalozi na Mamlaka mbalimbali za Algeria ikiwemo sekta binafsi.


Mhe. Balozi Joudi ameuomba Ubalozi kuimarisha kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini hapo kwa lengo la kuitangaza Lugha hiyo na kuifundisha kwa Wa' Algeria wengi zaidi.

Sunday, October 29, 2023

DMI YAINGIA MKATABA WA KUBADILISHANA UZOEFU NA CHUO CHA ITALY.

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italy ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu

MOU hiyo imesainiwa nchini Italy na Dkt.Tumaini Gurumo, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM) Bw. Eugenio Massolo. 

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha DMI Dkt. Tumaini Gurumo amesema kuwa makubalino hayo ya miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia” Alisema Dkt. Tumaini.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Italy Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi.

Kwa upande wake Balozi Kombo amesema kuwa Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilevile Balozi Kombo ametoa wito kwa upande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili izae matunda yanayotarajiwa.

Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijiNI Roma, Italy.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakipongezana baada ya kusaini MOU ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia, tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijini Roma, Italy.

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt.Tumaini Gurumo na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy(FAIMM) Eugenio Massolo wakionesha Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo ya ubaharia na tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu katika hafla iliyofanyika jijiNI Roma, Italy.

ZIARA YA KIKAZI YA RAIS WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI NCHINI, MHESHIMIWA DKT. FRANK-WALTER STEINMEIER

 







Mkataba wa Euro Milioni 36 kwa Ajili ya Mradi wa Umeme wa Kakono Wasainiwa

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila A. Mkumbo (kushoto) akifurahia baada ya uwekaji saini wa mkataba baina ya EU na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ambapo EU imetoa msaada (grant) kwa Tanzania wa Euro milioni 36 sawa na Shilingi bilioni 95 kwa ajili ya Mradi wa Uzalishaji wa Umeme kwa njia ya Maji wa Kakono, mkoani Kagera wa MW 87.8).

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila A. Mkumbo (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas A. Nyamanga (wa kwanza kulia) wakifutilia majadiliano ya Mkutano wa Global Gateway Forum uliofanyika Brussels, Ubelgiji tarehe 25 na 26 Oktoba 2023 






 

Saturday, October 28, 2023

KAMATI YA BUNGE YA NUU YATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU ARUSHA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipokutana katika ofisi za Mahakama hiyo jijini Arusha

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato  akizungumza kitu alipokutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud (katikati) kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa walipotembelea Mahakama hiyo jijini Arusha


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa (kushoto) akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walipowasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha



Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud walipotembelea Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Iman Aboud na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato  na wajumbe wengine wa Kamati hiyo katika picha ya pamoja na watendaji wengine wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Arusha



 
 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama imetembelea Mahakama ya Afrika ya Haki za  Binadamu na Watu (AFCHPR) yenye makao yako jijini Arusha na kuzungumza na Rais wa Mahakama hiyo Mhe. Jaji Iman Aboud.
 
Kamati ya NUU pia imetembelea Eneo la Lakilaki jijini Arusha ambako Serikali ya Tanzania inajenga  Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AFCHPR)
 
Kamati imeipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuigawia  Mahakama hiyo eneo la Lakilaki na kwa kutimiza ahadi ya kujenga Mahakama hiyo.
 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NUU YATEMBELEA AICC



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) akiwa na baadhi wa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo walipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) walipotembelea kituo hicho jijini Arusha kujionea  kinavyotekeleza majukumu yake na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru akiwaelezea Waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) walipotembelea majumba ya Kituo hicho yaliyopo eneo la uzunguni jijini Arusha  walipotembelea kituo hicho  na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa kwanza kulia) akiwa na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (wa pili kulia) na baadhi wa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) walipotembelea kituo hicho jijini Arusha



Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru akiwaelezea Waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) walipotembelea majumba ya Kituo hicho yaliyopo eneo la uzunguni jijini Arusha  walipotembelea kituo hicho  na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC


Mwenyekiti wa Kamati ya NUU  Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wa pili kulia) akimsikiliza mmoja wa Wabunge na mjumbe wa kamati hiyo akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha  (AICC) Bw. Ephraim Mafuru  wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha 

Mwenyekiti wa Kamati ya NUU  Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) (wakwanza kulia) akiwa na  Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (katikati) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa wakimsilikiza wasilisho kutoka AICC  wakati wajumbe ya Kamati hiyo walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  wa AICC Balozi Begam Taj  akizungumza kuwakaribisha Wajumbe wa Kamatiya NUU walipotembelea Kituo hicho jijini Arusha


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya NUU wakifatilia majadiliano kati ya Kamati ya NUU na Menejimenti ya AICC wakati  Kamati ya Bunge ya NUU ilipotembelea Kituo hicho jijini Arusha

 

 

        
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imetembelea  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)  na kuzitaka  Taasisi za Umma na Binafsi zinazo daiwa na kituo hicho kulipa madeni yao ili Kituo hicho kiendeshe shughuli zake kwa ufanisi na kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuvutia utalii wa Mikutano Nchini.
 
Wito huo umetolewa na 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Vita Kawawa, (Mb.) alipotembelea AICC na kamati yake kujionea Kituo hicho kinavyotekeleza majukumu yake na kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na kuendeshwa na AICC  jijini Arusha.
 
Akizungumza katika kikao na menejimenti ya AICC, Mhe. Kawawa amezitaka taasisi za umma na zile za binafsi kuhakikisha zinalipa madeni wanayodaiwa na Kituo hicho ili kiweze kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.
 
“Tumemsikia MD wa AICC, Bw. Mafuru akiongelea changamoto mbalimbali zinazoikabili AICC kuwa ni pamoja na madeni ambayo taasisi za umma na za binafsi zinadaiwa, naseme hivi, taasisi zote za umma na za binafsi zilipe madeni ya AICC, ili kituo kiweze kujiendesha kwa ufanisini, kuunga mkono harakati za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuvutia mikutano mikubwa nchini na kutoa mchango stahiki kwa pato la taifa,” alisema Mhe. Kawawa.
 

Amesema kwa AICC kufanya kazi kwa ufanisi ni lazima iondokane na hiyo changamoto ya madeni kwani kulipwa kwa madeni hayo kutaiwezesha kufanya kazi zake kwa tija na ufanisi na hivyo kupata matokeo chanya na kupongeza uendeshaji wa miradi ya maendeleo inayoendeshwa na kituo hicho jijini Arusha
 
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato, (Mb.) ameishukuru Kamati ya NUU kwa kutembelea AICC na kuitaka Bodi ya AICC kuhakikisha inashughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo yakiwemo madeni ya taasisi mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
 
Mhe. Byabato amewataka AICC wapitie upya na kwa ukamilifu orodha ya madeni wanayodai na kuangalia namna bora ya kukusanya  madeni hayo, kuwakumbusha kwa viambatisho na kuangalia mbinu mpya za namna ya kudai madeni hayo ikiwa ni pamoja na kuangalia kama utoaji wa "offer" za kulipa madeni hayo kama unaweza kusaidiwa kupunguzwa kwa madeni hayo.
 
“ pitieni upya madeni yenu, angalieni njia za kulazimishana pia kama itawezekana, muwe na mikakati mahususi ya wadeni na njia za kulipa madeni, kuna  madhara kwa madeni hayo kuendelea kuonekana katika vitabu vyenu nadhani mnajua kuwa yanaweza sababisha mshindwe kukopesheka pale mtakapotaka kufanya hivyo katika taasisi za kimataifa,” alisisitiza Mhe. Byabato.
 
Awali akizungumza katika kikao na Kamati ya NUU, Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Ephraim Mafuru amesema AICC inaandaa mkakati wa kipaumbele utakaoiwezesha AICC kutekeleza vipaumbele vyake ili iende na wakati na kuhimili ushindani wa soko la Diplomasia ya Mikutano.
 
Amesema AICC pamoja na kufanya shughuli zake katika mazingira ya ushindani, inakabiliwa na changamoto mbalimbali yakiwemo madeni ya muda mrefu ambayo taasisi za serikali na za binafsi hazijailipa AICC kwa muda mrefu sasa.
 
“Kwa sasa AICC inatekeleza shughuli zake kwa kuitangaza nchi katika nyanja ya utalii wa mikutano na matukio na hivyo kuvutia mikutano mingi kuja nchini kwa kuwa vituo vya mikutano duniani hufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine ambao ni wanufaika wa moja kwa moja wageni wanapo kuja nchini kwa ajili ya mikutano,” alisema Bw. Mafuru.
 
Amesema AICC imeamua kuwekeza katika miundombinu ya kisasa na kufanya mabadiliko yanayoendana na wakati kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Kituo wa mwaka 2022/2023-2026/2027 ulioidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi mwezi Juni 2022 na kuanza kutumika rasmi mwezi Julai 2022.  
 
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Saidi Shaib Mussa akizungumza katika kituo hicho ameipongeza Bodi na Menejimenti ya AICC kwa  kutokufanya kazi kwa mazoea na kuwaahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na kufanya nao kazi bega kwa bega ili kufanikisha utendaji wao.

Kamati Hiyo pia imekagua miradi mbalimbali ya uwekezaji ya nyumba za makazi, na hospitali na viwanja vya Kituo hicho na kuonyesha kuridhishwa na usimamizi na uendeshaji wa miradi hiyo.


 


Friday, October 27, 2023

RAIS DKT. SAMIA APONGEZWA KWA KUTAMBUA MCHANGO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI

Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu na kutambua mchango wao kwenye maendeleo ya  nchi.

 

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 27 Oktoba 2023 na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe.  Prof. Remy Ngoy Lumbu mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya Tanzania kuhusu Hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu kwenye kikao cha 77 cha Tume hiyo kinachoendelea jijini Arusha.

 

Prof. Lumbu amesema kuwa amefurahishwa na taarifa ya Tanzania iliyowasilishwa kwenye kikao hicho kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Watetezi wa Haki za Binadamu na kuishukuru nchi hiyo kwa kutambua na kuthamini mchango wa Watetezi wa Haki za Binadamu kama washirika muhimu katika maendeleo ya nchi.

 

Pia ameeleza kuwa, kauli ya  Serikali hiyo ya kufungua  milango yake kwa ajili ya kushirikiana na watetezi wa haki za binadamu ni ya kupigiwa mfano na nchi nyingine na kuuunga mkono wito wa Serikali ya Tanzania wa kuwataka watetezi wa haki za binadamu kuendelea kuheshimu katiba ya nchi na miongozo yote inayosimamia haki za binadamu na watu nchini humo.

 

“Naomba ujumbe wa Tanzania mfikishe salamu zangu za pongezi kwa Mhe. Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na kuwalinda watetezi wa haki za binadamu nchini kwake. Nimefurahishwa pia na kauli ya Serikai ya Tanzania kwamba milango yake ipo wazi wakati wote kwa ajili ya kuwapokea na kushirikiana na watetezi hao wa haki za binadamu,” alisema Mhe. Prof. Lumbu.

 

Awali akiwasilisha Taarifa ya Tanzania kuhusu Hali ya Watetezi wa Haki za Binadamu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Richard Kilanga amesema kuwa Serikali za Tanzania Bara na Zanzibar zimeendelea kushirikiana na watetezi wa haki za binadamu nchini katika kuboresha masuala yote yanayohusu usimamizi, uimarishaji, na ulinzi wa haki za binadamu nchini.

 

Amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuyawezesha mashirika hayo na watetezi wa haki za binadamu kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ambapo amesema hadi sasa Tanzania inayo mashirika yasiyo ya kiserikali 9,900.

 

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafahamu umuhimu wa watetezi wa haki za binadamu ndiyo sababu zipo sheria mbili zinazosimamia. Ipo Sheria ya Mashirika yasiyo ya kiserikali na Sheria ya Jumuiya za Kiraia kwa pande zote mbili Bara na Visiwani” alisema Bw. Kilanga.

 

Ameongeza kusema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na  mashirika hayo katika kukuza na kulinda  haki za binadamu na watu nchini pamoja na kujenga uchumi wa nchi  ambapo ameeleza kuwa kwa mwaka 2022 mashirika hayo yamechangia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.24 sawa na Dola za Marekani milioni 800 kwenye uchumi wa nchi.

“Hakuna shaka kwamba Serikali inatambua mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali, mkiwemo watetezi wa haki za binadamu katika kukuza na kulinda haki za binadamu na watu pamoja na kuleta maendeleo nchini, hususan kwa kuzingatia Mpango Kazi wa Tatu wa Nchi wa Mwaka 2021/22-2025/26 inayotekeleza agenda ya nchi ya Maendeleo ya 2025. Mpango Kazi huu uliandaliwa kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwamba Mashirika hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi huo” alisema Bw. Kilanga.

 

Kadhalika, Bw. Kilanga amesema kutokana na jitihada za kuimarisha na kusimamia utekelezaji wa haki za binadamu nchini zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, mwezi Mei 2022 ulimtunukia zawadi kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kutetea haki za binadamu na utawala wa sheria nchini.

 

Vilevile ameongeza kusema milango ya Serikali ipo wazi kwa watetezi wa haki za binadamu katika kuendelea kushirikiana na Serikali ili kutimiza lengo la pamoja la kila mwananchi kunufaika na haki za binadamu na watu huku akisisitiza wajibu wa taasisi za watetezi wa watu wa kuendelea kutii sheria za nchi na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 26 (1).

 

Kikao cha Kawaida cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kilifunguliwa rasmi jijini Arusha tarehe 20 Oktoba 2023 na kinatarajiwa kumalizika tarehe 09 Novemba, 2023. Pamoja na mambo mengine kikao kinapokea na kujadili agenda  mbalimbali zinazohusu haki za binadamu katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Mwenyekiti wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu (katikati) akizungumza wakati wa Kikao cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoendelea jijini Arusha. Pamoja namambo mengine, Prof. Lumbu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na watetezi wa haki za binadamu na kutambua mchango wao kwemye maendeleo ya nchi


kwa kuendelea kushirikiana na Watetezi wa Haki za Binadamu na kutambua mchango wao kwenye maendeleo ya  nchi.