Sunday, January 14, 2024

MKUTANO WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA ANGOLA WAANZA ZANZIBAR

Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola umeanza tarehe 14 Januari 2024 Zanzibar.

Mkutano huo unafanyika katika ngazi mbili za maafisa waandamizi unaofanyika tarehe 14 — 15 Januari 2024 na ngazi ya mawaziri utafanyika tarehe 16 Januari 2024.

Mkutano huo unalenga kujadili mambo mbalimbali muhimu ya ushirikiano ya siasa, diplomasia, ulinzi, usalama, Sheria, kilimo, uchumi wa buluu, biashara na uwekezaji.

Maeneo mengine ni pamoja na maendeleo ya miundombinu, ujenzi, uchukuzi, nishati, madini, tehama na huduma za kijamii za afya, elimu, sayansi, na teknolojia ya Habari na mawasiliano. Mkutano huo pia unalenga kuibua maeneo mapya ya ushikiano ili  kuchagiza maendeleo kati ya Tanzania na Angola.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya Maafisa Waandamizi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa amebainisha kuwa mkutano huo utatoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo uchumi hususan biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, miundombinu na fedha. 

“Katika mkutano wetu tunategemea kujadili masuala ya uchumi hususan msingi wa diplomasia ya uchumi. Mkutano huu utatoa mipango na mikakati ya pamoja itakayoimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili,” Alisema Balozi Mussa.

Balozi Said aliongeza kuwa mkutano huo unajenga na kuendeleza misingi madhubuti ya mashirikiano katika nyanja mbalimbali na kuhakikisha kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Angola unaendelea kuimarika zaidi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Angola, Balozi Carlos Sardinha Dias amesema mikutano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano imekuwa ikitoa fursa mbalimbali za kujadili masuala ya kisekta katika maeneo mahususi ya kipaumbele kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Mikutano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano itaendelea kujadili masuala ya kisekta katika maeneo mahususi ya ushirikiano katika nyanja za diplomasia, usalama, ulinzi na uboreshaji wa huduma za kijamii,” alisema Balozi Sardinha Dias.  

Mkutano huu umejumuisha Mabalozi, Watendaji Wakuu na Maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania na Angola.

Mkutano wa kwanza ulifanyika mwezi Oktoba, 1988 Jijini Dar es Salaam. Kufanyika kwa mkutano huu wa Pili kunafuatia kusainiwa kwa Hati mbili za Makubaliano (MoUs) za kuhuisha/kufufua Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Hati ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola mwezi Februari 2023 Addis Ababa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola tarehe 14 Januari 2024 Zanzibar

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Mambo ya Nje - Angola, Balozi Carlos Sardinha Dias akizungumza katika Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola tarehe 14 Januari 2024 Zanzibar

Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola tarehe 14 Januari 2024 Zanzibar

Viongozi wa Meza kuu katika picha ya pamoja wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa (mwenye tai nyekundu), Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje - Angola, Balozi Carlos Sardinha Dias (mwenye kamba ya njano shingoni) , Balozi wa Tanzania nchini Zambia, anayewakilisha pia Tanzania nchini Angola, Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule (wa kwanza kushoto) pamoja na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe. Sandro de Oliveira (wa kwanza kulia).

Viongozi wa Meza kuu katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Angola tarehe 14 Januari 2024 Zanzibar



Saturday, January 13, 2024

TANZANIA, RWANDA ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO UENDELEZAJI WA SEKTA YA MAZIWA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa na Jamhuri ya Rwanda.

Hati hiyo imesainiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi - Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega, (Mb.) na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Ulega alisema Tanzania kwa kushirikiana na Rwanda wakifanya jitihada za pamoja za kuzalisha maziwa ya kutosha na kuyasindika wananchi watapata ajira za kutosha, kuwapatia wananchi lishe pamoja na kupunguza maradhi.

“Tukifanikiwa kuwa na uzalishaji mzuri wa maziwa tutaweza kuongeza uchumi wetu, na kuifanya biashara ya maziwa kuwa kubwa zaidi,” alisema Waziri Ulega.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe alisema amefarijika na hatua hiyo iliyofikiwa kwani waliisubiri muda mrefu na ni imani yake kuwa tija kubwa itapatikana katika sekta ya maziwa kupitia ushirikiano huo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe. 

Viongozi wengine ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Maj. Gen. Ramson Godwin Mwaisaka, Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Hererimana Fatou pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Bodi ya Maziwa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi - Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega, (Mb.) akizungumza wakati wa hafla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa na Jamhuri ya Rwanda. Kushoto ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar. Wengine pichani ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.). 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi - Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega, (Mb.) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe wakisaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa kati ya Tanzania na Rwanda tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar

Waziri wa Mifugo na Uvuvi - Tanzania, Mhe. Abdallah Ulega, (Mb.) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa kati ya Tanzania na Rwanda tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza wakati wa Hafla ya utiaji saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa kati ya Tanzania na Rwanda tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar

Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa kati ya Tanzania na Rwanda tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar

Viongozi na badhi ya watumishi wakiwa katika picha ya pamoja ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika uendelezaji wa Sekta ya Maziwa kati ya Tanzania na Rwanda tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda wa Rwanda, Mhe. Jen. (Rtd.) James Kabarebe tarehe 12 Januari 2024, Visiwani Zanzibar


Friday, January 12, 2024

DKT. MWINYI AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa New Amani Complex, Mkoa wa Mjini- Magharibi Unguja, ambapo pia imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sherehe za mapinduzi zimehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa mataifa jirani ambao ni Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Rigathi Gachagua pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Viongozi wengine ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Akson pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali zote mbili.

Akitoa salamu katika sherehe hizo, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi matukufu.

“Nawashukuru na kuwapongeza wazanzibar na watanzania kwa ujumla kwa kuulinda Muungano, nawasihi tuendelee kushikamana na kuwa wamoja kwani tumebaini kuwa Bara la Afrika haliwezi kuendelea bila kushikamana,” Alisema Mhe. Museveni

Naye Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mapinduzi, na kusema kuwa kufanyika kwa Mapinduzi kumedhihirisha ushirikiano na umoja wa Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla. 

Kadhalika, Naibu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe.Rigathi Gachagua ameipongeza Zanzibar na kuwasihi kuendelea kushikamana kama kaka na dada na kuhakikisha umoja wetu hautenganishwi na jambo lolote. “Nawapongeza Wazanzibar kwa kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi,” alisema.

Viongozi wengine walioshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ni Waziri Mkuu wa Burundi Mhe. Gervais Ndirakobuca na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Marais wastaafu walioshiriki ni pamoja na Rais Mustaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mhe. Aman Abeid Karume. Wengine ni Mawaziri Wakuu Wastaafu, Mhe. Fredrick Sumaye, Mhe. Peter Pinda pamoja na Mawaziri mbalimbali.

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964 ambapo chama cha Afro Shirazi kwa kushirikiana na wanachama wa Chama cha Umma waliiondoa madarakani serikali ya mseto wa vyama vya Wazalendo wa Zanzibar, ZNP, na Chama cha Watu wa Zanzibar na Pemba, ZPPP na kutangaza Jamhuri ya Watu wa Zanzibar badala ya serikali ya Kisultani.

Tukio hilo lilichochea/waafrika wengi, kutanzua tatizo hilo, vyama viwili vya waafrika, Afro Shirazi Party (ASP) viliungana na Umma Party kuongeza nguvu, tarehe 12 Januari 1964, ASP ikiongozwa na John Okello, ilihamasisha wanamapinduzi wapatao 600 kuingia mji wa Zanzibar (Unguja) na kupindua Serikali ya Sultani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia wananchi waliojitokeza kushiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikagua gwaride katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi (mgeni rasmi) pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akifuatilia sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Museveni akiongea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame akiongea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar



Thursday, January 11, 2024

NJE SPORTS YAENDELEZA UBABE, YAITWANGA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI 3 - 0

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) imeendeleza shangwe kwa mashabiki wake baada ya kuifumua timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kwa magoli 3 - 0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mao Zedong’s mjini, Zanzibar.

Magoli  ya Nje Sports yalifungwa na mshambuliaji Fabian David (1) katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza ambalo lilidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili, Nje sports walirejea kwa kasi na kwa kupitia winga wake Yacoub Kibiga iliandika goli la pili lililopatikana dakika ya 79 na baadaye akafunga goli la tatu katika dakika ya 86 ya mchezo.

Nje Sports haikufungwa mchezo wowote tangu ilipowasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya bonanza la michezo. Aidha, katika mechi yake ya kwanza iliyochezwa tarehe 09 Januari 2024 dhidi ya Baraza la Wawakilishi ilitoka na ushindi wa mabao (3 - 1) mechi ya pili iliyochezwa dhidi ya Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar iliyochezwa tarehe 10 Januari 2024 ilitoka na ushindi mnono wa magoli (8 – 3) na katika mechi yake ya leo dhidi ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imeibuka na ushindi wa goli 3 – 0.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameipongeza Nje Sports kwa ushindi mnono na kuzitaka timu zote mbili kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni afya na inaimarisha ushirikiano baina ya wachezaji na jamii.

Naye Kocha wa Nje Sports, Bw. Shaban Maganga amesema pamoja na ushindi walioupata wataendelea kujifua zaidi na kuhakikisha kuwa kikosi chake kinakuwa imara wakati wote.

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) katika mazoezi kabla ya mpira kuanza katika Uwanja wa Mao Zedong's Unguja, Zanzibar

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza katika Uwanja wa Mao Zedong's Unguja, Zanzibar

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza katika Uwanja wa Mao Zedong's Unguja, Zanzibar


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa (aliyevaa shati) akifuatilia mechi kati ya Nje Sports na timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akifuatilia mechi kati ya Nje Sports na timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili mara baada ya kumalizika kwa mchezo 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa akizungumza na wachezaji wa timu zote mbili baada ya kumalizika kwa mchezo ambao Nje Sports imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3 - 0


Wednesday, January 10, 2024

NJE SPORTS YAIGALAGAZA TIMU YA IKULU ZANZIBAR

Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) imeigalagaza timu ya mpira wa miguu kutoka Ofis ya Rais Ikulu Zanzibar magoli 8 – 3 katika mchezo ulichezwa uwanja wa Mao Zedong’s Unguja, Zanzibar.

Nje Sports iliutawala mpira kwa asilimia kubwa ambapo kipindi cha kwanza iliongoza kwa magoli 5 – 1. Magoli ya nje sports yalifungwa na Ramadhani Chambuso (1), Said Kasanga (2), Selemani Mkonde (2), Fabian David (1), Yakubu Kibiga (1) na Benjamin Mhume (1).

Magoli ya timu kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar yalifungwa na Khamis Ramadhan (1) pamoja na Seif Hatibu Ally (2).

Ushindi wa Nje Sports umeiwezesha kusonga mbele ambapo tarehe 11 Januari 2024 itacheza na Hazina katika uwanja wa Mao zedong’s Unguja, Zanzibar majira ya saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa timu ya Nje Sports, Shaban Maganga amesema kuwa lengo la timu yake ni kuimarisha kikosi na kujihakikishia ushindi katika michezo inayaofuata. Kadhalika kocha huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuwawezesha vyema hadi kufikia hatua hiyo.

Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza katika Uwanja wa Mao Zedong's Unguja, Zanzibar


Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) katika picha ya pamoja na timu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar katika Uwanja wa Mao Zedong's Unguja, Zanzibar

Kocha wa timu ya Nje Sports, Shaban Maganga akizungumza na wachezaji











WAZIRI MAKAMBA AAGANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan aliyefika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan aliyefika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) na ujumbe wake (kulia) akizungumza na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan na ujumbe wake (kushoto) walikutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba katika picha na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimkabidhi zawadi ya picha ya Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.), ameagana na Balozi wa India anayemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salam tarehe 10 Januari, 2024, Mhe. Waziri Makamba amemshukuru Mhe. Binaya kwa jitihada zake za kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na India unakua na kuimarika.

Amempongeza pia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia ziara iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India na kufanikisha kusainiwa kwa Hati za Makubaliano ya Ushirikiano wakati wa ziara hiyo.

Naye Mhe. Balozi Binaya ameshukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla wakati wote wa kipindi chake alichohudumu nchini.

 

Tuesday, January 9, 2024

TANZANIA KATIKA ANGA LA KIMATAIFA INA SIFA NA HADHI YA KIPEKEE DUNIANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amesema Tanzania katika eneo la kidiplomasia ina sifa na hadhi ya kipekee duniani.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Januari 2024.

“Ili nchi iweze kufanya mambo yake vizuri duniani, lazima iwe na ushawishi mkubwa duniani, na Tanzania ni moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa duniani,” alisema Waziri Makamba.

Aliongeza kuwa Nchi au Kiongozi lazima ilinde utu, uhuru wake duniani na hayo yote yataonekana kupitia Sera ya Mambo ya Nje. 

“Kupitia Sera ya Mambo ya Nje, nchi inapata kukuza uwezo wa kujiamulia mambo yake, na kujipambanua jinsi ambavyo itaendesha mambo yake”, alisema.

Akizungumzia kufanyiwa marekebisho kwa Sera hiyo, Waziri Makamba amesema marekebisho hayo yamelazimika kufanyika kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea duniani kwa wakati huu na hivyo kuilazimu Tanzania kuendesha mambo yake kwa mujibu wa mabadiliko hayo.

Ametaja mabadiliko hayo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, kuibuka kwa taasisi zenye nguvu, ushawishi na uwezo wa kubadilisha vitu duniani, maendeleo ya teknolojia  ya Habari na mawasiliano na uwepo wa asilimia kubwa ya watanzania waliozaliwa baada ya mwaka 2001 wakati sera hiyo ilipotengenezwa.

Amesema kutokana na hali hiyo Wizara iliyona kuna haja ya kufanyia maboresho sera hiyo ili kutoa nafasi kwa watanzania kutoa maoni yao juu ya sera hiyo kwa ajili ya kuunda kesho yao na kuendana na wakati wa sasa na wakati ujao.

Kongamano hilo la kukusanya maoni lilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa dini, wazee wa Dar es salaam, wasomi, wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Dar es Salaam, makundi ya kijamii na vijana.

Akifanya majumuisho ya kongamano hilo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) alipata fursa ya kujibu baadhi ya hoja ambazo ziliibuliwa na washiriki wa Kongamano hilo.

Balozi Mbarouk amesema kuwa msimamo wa Tanzania toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa ni ule ule, haujabadilika, msimamo wa Tanzania kwa Palestina na Saharawi unajulikana vizuri na haujawahi badilika, siku zote Tanzania imekuwa ikitoa matamko yake.

Alisema tangu yaanze mapigano kati ya Palestina na Israeli, Tanzania imeunga mkono matamko yote Saba ya Umoja wa Mataifa yaliyolenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu.

“Hatujakataa azimio hata moja, maazimio yote yalilenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu tuliyaunga mkono,” alisema Balozi Mbarouk.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) akifunga Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Bakari Machumu akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mwanasisa Mkongwe, Prof. Anna Tibajaijuka akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Bishara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi John Ulanga akiendesha mjadala wakati wa Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiongea katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau  kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akiwasilisha mada kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam