Tuesday, January 9, 2024

TANZANIA KATIKA ANGA LA KIMATAIFA INA SIFA NA HADHI YA KIPEKEE DUNIANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amesema Tanzania katika eneo la kidiplomasia ina sifa na hadhi ya kipekee duniani.

Waziri Makamba ametoa kauli hiyo akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Januari 2024.

“Ili nchi iweze kufanya mambo yake vizuri duniani, lazima iwe na ushawishi mkubwa duniani, na Tanzania ni moja ya nchi zenye ushawishi mkubwa duniani,” alisema Waziri Makamba.

Aliongeza kuwa Nchi au Kiongozi lazima ilinde utu, uhuru wake duniani na hayo yote yataonekana kupitia Sera ya Mambo ya Nje. 

“Kupitia Sera ya Mambo ya Nje, nchi inapata kukuza uwezo wa kujiamulia mambo yake, na kujipambanua jinsi ambavyo itaendesha mambo yake”, alisema.

Akizungumzia kufanyiwa marekebisho kwa Sera hiyo, Waziri Makamba amesema marekebisho hayo yamelazimika kufanyika kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea duniani kwa wakati huu na hivyo kuilazimu Tanzania kuendesha mambo yake kwa mujibu wa mabadiliko hayo.

Ametaja mabadiliko hayo kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, kuibuka kwa taasisi zenye nguvu, ushawishi na uwezo wa kubadilisha vitu duniani, maendeleo ya teknolojia  ya Habari na mawasiliano na uwepo wa asilimia kubwa ya watanzania waliozaliwa baada ya mwaka 2001 wakati sera hiyo ilipotengenezwa.

Amesema kutokana na hali hiyo Wizara iliyona kuna haja ya kufanyia maboresho sera hiyo ili kutoa nafasi kwa watanzania kutoa maoni yao juu ya sera hiyo kwa ajili ya kuunda kesho yao na kuendana na wakati wa sasa na wakati ujao.

Kongamano hilo la kukusanya maoni lilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wanasiasa, viongozi wa dini, wazee wa Dar es salaam, wasomi, wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Dar es Salaam, makundi ya kijamii na vijana.

Akifanya majumuisho ya kongamano hilo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) alipata fursa ya kujibu baadhi ya hoja ambazo ziliibuliwa na washiriki wa Kongamano hilo.

Balozi Mbarouk amesema kuwa msimamo wa Tanzania toka enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa ni ule ule, haujabadilika, msimamo wa Tanzania kwa Palestina na Saharawi unajulikana vizuri na haujawahi badilika, siku zote Tanzania imekuwa ikitoa matamko yake.

Alisema tangu yaanze mapigano kati ya Palestina na Israeli, Tanzania imeunga mkono matamko yote Saba ya Umoja wa Mataifa yaliyolenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu.

“Hatujakataa azimio hata moja, maazimio yote yalilenga kusitishwa kwa mapigano hayo na kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu tuliyaunga mkono,” alisema Balozi Mbarouk.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akifungua Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) akifunga Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Bakari Machumu akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mwanasisa Mkongwe, Prof. Anna Tibajaijuka akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Bishara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi John Ulanga akiendesha mjadala wakati wa Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akiongea katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau  kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akiwasilisha mada kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam

Moja kati ya mdau akichangia mjadala katika Kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 tarehe 9 Januari, 2024 Jijini Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.