Makamu wa Rais wa Cuba,
Mhe. Salvador Mesa amemaliza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini aliyoifanya
kuanzia tarehe 23 hadi 25 Januari, 2025.
Akiwa nchini, Mhe. Mesa
alikutana kwa mazungumzo na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Katika mazungumzo yao,
Viongozi hao walikubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina
ya Tanzania na Cuba hususan kwenye maeneo ya kimkakati ya kilimo, afya,
teknolojia na elimu.
Vilevile viongozi hao walishuhudia utiaji saini wa Hati mbili za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Artimesa Diaz Gonzalez cha
Cuba.
Hati ya pili ya Makubaliano iliyosainiwa ilihusu ushirikiano
kati ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
Tanzania(TMDA) na Kituo cha Afya cha Taifa cha Udhibiti na Vifaa Tiba (CECMED)
cha Serikali ya Cuba kwa lengo la kupanua wigo na kuongeza matumizi ya
teknolojia katika masuala ya dawa na vifaa tiba.
Mhe. Mesa pia
alitembelea Taasisi ya Mwalimu Nyerere ya jijini Dar es Salaam pamoja na
kutembelea Kiwanda cha Viuadudu cha Biotech kilichopo Kibaha, Pwani.
Mhe. Mesa pia alipata nafasi ya kumtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere kwenye makazi yake jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumsalimia na kumjulia hali.
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa akiagana na Maafisa wa Ubalozi wa Cuba nchini mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini aliyoianza tarehe 23 hadi 25 Januari, 2024. |
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa akiagana na wadau mbalimbali |
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu akiagana na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini aliyoianza tarehe 23 hadi 25 Januari, 2024. |
Mawaziri wakimpungia mkono wa kwaheri Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Mesa mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini aliyoianza tarehe 23 hadi 25 Januari, 2024. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.