Mhe. Mesa ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Januari
2024 alipotembelea Kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya
siku tatu nchini kuanzia tarehe 23 hadi 25 Januari 2024.
Amesema nchi yake itaendelea kutoa msaada wa
kitaalam kwa mamlaka za Tanzania ili kukiwezesha kiwanda hicho kuzalisha bidhaa
tofautitouti mbali na viuadudu vya malaria, zikiwemo mbolea, viuatilifu
na bidhaa nyingine za kilimo
Pia amesema kiwanda hicho kitaendelea kuwa mfano
wa ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya Tanzania na Cuba katika sekta
mbalimbali ikiwemo ya afya.
“Nimepata bahati ya kukitembelea kiwanda hiki kwa
mara ya pili sasa, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2016 wakati kinakamilishwa.
Napongeza hatua iliyofikiwa kwenye uzalishaji” amesema Mhe. Mesa.
Amesema kiwanda hicho kinatakiwa kutunzwa kwani ni
chanzo cha ajira kwa watanzania lakini pia kinakuza uchumi wa Tanzania pamoja
na kuimarisha afya za watanzania.
Awali akizungumza kumkaribisha Mhe. Mesa katika
kiwanda hicho, Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhe. Abubakar Kunenge amesema kuwa
anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda kwenye mkoa huo na
kuwakaribisha wawekezaji zaidi kutoka Cuba kuja kuwekeza.
Miongoni mwa Viongozi wengine walioshiriki ziara
ya Mhe. Mesa kwenye kiwanda hicho ni Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Angellah Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Humphrey Polepole
na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera.
Mhe. Mesa akiwa amepokelewa na Mhe. Dkt. Kijaji mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya Mbu wanaoeneza Malaria kilichopo Kibaha mkoani Pwani. |
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Mesa alipotembelea kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya Mbu wanaoeneza Malaria kilichopo Kibaha mkoani Pwani. |
Meza kuu |
Mkutano ukiendelea |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.