Wednesday, September 18, 2013
Sunday, September 15, 2013
Friday, September 13, 2013
Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Italia nchini
Balozi Scotto akisalimiana na Balozi Msechu. |
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Scotto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho. Mwingine katika picha ni Afisa wa Ubalozi wa Italia hapa nchini aliyefuatana na Balozi huyo. |
Mhe. Balozi Scotto akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili IKULU. |
Kikundi cha Brass Band kikiwa kazini wakati wa mapokezi ya Balozi Scotto.
Picha na Reginald Philip Kisaka.
|
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akutana na Mwakilishi wa UNFPA nchini
Balozi Celestine Mushy akimkaribisha Wizarani Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) nchini Tanzania Bibi Mariam Khan. |
Bibi Khan akimweleza jambo Balozi Mushy kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Shirika lake hapa nchini |
Naibu Waziri awatembelea Watanzania wanaojishughulisha na biashara mjini Lusaka
Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushurikiano wa Kimataifa akizungumza na mmoja wa wajasiriamali wa kitanzania
wanaofanya shughuli zao katika soko la Comesa lililopo mjini Lusaka, Zambia
alipofanya ziara ya kuwatembelea Watanzania wanaojishughulisha katika eneo
hilo, tarehe 12 Septemba 2013.
|
Mhe. Naibu Waziri akikagua shughuli za wajasiriamali
Watanzania katika soko la Comesa. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mhe.
Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na kushoto ni Bw. Mboweto, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Comesa ambaye ni Mtanzania.
Naibu Waziri azungumza na Wajasiriamali wa Kitanzania, Lusaka
Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.),
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania amewatembelea Wajasiriamali ambao ni Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya
shughuli zao nchini Zambia katika maeneo ya Viwanja vya COMESA. Katika ziara
hiyo iliyofana, Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa
Tanzania nchini Zambia pamoja na Maofisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Baada ya kutembelea mabanda mbalimbali na kukagua shughuli zinazofanywa na Watanzania hao, Mhe. Naibu Waziri alipata fursa ya kubadilishana nao mawazo. Watanzania hao walielezea furaha yao kwa kutembelewa na kiongozi wa Serikali ya Tanzania na kubainisha kufarijika kwao kwa namna Serikali yao inavyowajali. Waliomba juhudi zifanyike kupanua barabara katika eneo la Tunduma ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo. Aidha, waliomba mashauriano yafanyike ili kituo cha mpaka cha Tunduma/Nakonde kifanye kazi kwa masaa 24. Walisema hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano, kuongeza kasi ya biashara, kupunguza vitendo vya jinai na kuiongezea mapato Serikali. Kwa upande wake, Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza Watanzania hao kwa kuamua kufanya shughuli zinazoweza kuwapatia kipato cha halali na kujenga taifa lao. Aliwataka wahakikishe kwamba wote wanaishi kisheria na kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka za Zambia ili kuepusha usumbufu kwao na kwa Serikali. Aidha, aliwataka wasijihusishe na vitendo vyovyote vya jinai ili kuepusha kuchafua sifa nzuri za taifa la Tanzania. Mhe. Naibu Waziri yupo nchini Zambia akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa kimataifa kuhusu Mkataba unaolenga Kutokomeza matumizi ya Mabomu ya kusambaa (Convention on Cluster Munitions). Kabla ya kutembelea wajasiriamali, Mhe. Naibu Waziri alikutana na kuzungumza na Watanzania wa rika na kada mbalimbali wanaoishi nchini Zambia, mazungumzo ambayo yalifanyika katika Ubalozi wa Tanzania, Lusaka |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard K. Membe (Mb.) amemteua Brigedia Jenerali Mstaafu, Balozi Francis
Mndolwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Balozi Mndolwa ameteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na
Balozi Wilson Masilingi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Uholanzi hivi karibuni.
Brigedia Jenerali Mstaafu Mndolwa aliwahi kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Burundi kabla ya kustaafu utumishi wa umma.
Uteuzi wa Balozi Mndolwa unaanza mara moja.
Imetolewa na:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
12 SEPTEMBA, 2013.
Thursday, September 12, 2013
Permanent Secretary attends meeting on Thai-Africa Initiative
The Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Mr. John Haule (Centre), makes a point during bilateral talks with his Thailand counterpart, Mr. Sihasak Phuangketkeow in Bangkok, Thailand on September 5, 2013. He is flanked by Ambassador Mbelwa Kairuki, Director of Asia and Australasia (second right) and Mr. Rogatius Shao, Charge d'Affaires of the Tanzania High Commission in Kuala Lumpur, Malaysia. Others in the delegation were Mr. Dismas Asenga (Right), Foreign Service officer from the High Commission in Kuala Lumpur, Mrs. Naomi Zegezege (Second left) and Mr. Adam Isara (Left), Foreign Service Officers from the Ministry.
The Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs of the Kingdom of Thailand, Mr. Sihasak Phuangketkeow (Third left) opening a Thailand-Tanzania bilateral meeting in Bangkok, Thailand on September 5, 2013. The Tanzania delegation to the follow-up meeting of the visit of Thai Prime Minister Yingluck Shinawatra to Tanzania, was led by the Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Mr. John Haule.
The Permanent Secretary in the Ministry of
Foreign Affairs and International Cooperation, Mr. John Haule, in discussion
with Mr. Waranon Laprabang, Senior Vice President of PTT Exploration and
Production Public Company Limited of Thailand, who called on him at Sukosol
hotel in Bangkok on September 8, 2013. The PTT Group company is interested in
investing in Tanzania's oil and gas industry. Others in the meeting were Mr.
Rogatius Shao (Right), Charge d'Affaires of the Tanzania High Commission
in Kuala Lumpur, Malaysia, and Mrs. Naomi Zegezege (Left), Foreign Service
Officer in the Ministry.
|
The Director of the Department of Asia and
Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation,
Ambassador Mbelwa Kairuki (Second right) emphasises a point during discussions
with a delegation of Thonburi Hospital Group (THG) of Thailand, at Sukosol
hotel in Bangkok on September 8, 2013. The team was led by Vice President, Dr.
Tanatip Suppradit (Partly hidden, left) and Mr. Timothy Lertsmitivanta,
Assistant to Chairman of the THG Board (second left). on Ambassador Kairuki's
right is Mr.Adam Isara, Foreign Service Officer in the Foreign Ministry.
|
The
Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International
Cooperation, Mr. John Haule (Second right, seated) in a group picture with
participants in the Second Senior Officlals Meeting on the Thai-Africa
Initiative, which ended at the Hua Hin resort town in Thailand on
September 8, 2013. Mr. Haule led the Tanzanian delegation, which included the
Director of Africa and Australasia in the Foreign Ministry, Ambassador Mbelwa
Kairuki and the Charge d'Affaires at the Tanzania High Commission in Kuala
Lumpur, Malaysia, Mr. Rogatius Shao. |
Wednesday, September 11, 2013
Maonesho ya bidhaa za China yafunguliwa Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb) akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya China - Africa Show yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam tarehe 10 Septemba, 2013. |
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. LV Youqing naye akitoa hotuba katika maonesho hayo |
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) akitoa neno la kumkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia watu waliohudhuria ufunguzi wa maonesho ya China - Africa Show. |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia), Bw Omar Mjenga na Bw. Mkumbwa Ally, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje wa tatu kutoka kulia wakisikiliza kwa makini hotuba zinazotolewa na viongozi mbalimbali |
Baadhi ya watu waliohudhuria ufunguzi huo. Mstari wa mbele ni viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na ya China akiwemo Mhe. Waziri Mkuu wa tano kutoka kulia. |
Mhe. Mizengo Peter Pinda wa nne kutoka kulia akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa maonesho hayo |
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia mfano wa nyumba ya kisasa baada ya kufungua maonesho hayo. |
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia zana mbalimbali kama vile matrekta na majenereta |
Tuesday, September 10, 2013
A Congratulatory Message to the President of the Islamic Republic of Pakistan
H.E.
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania
has sent a congratulatory message to H.E.
Manmoon Hussain, President of the Islamic Republic of Pakistan following
his election as the President of Pakistan.
The
Message reads as follows:
His
Excellency Manmoon Hussain,
President
Elect,
Islamabad,
PAKISTAN.
Your Excellency
I have received with great joy the news
of your election as the President of the Islamic Republic of Pakistan.
On behalf of the Government and people
of the United Republic of Tanzania and, indeed, on my own behalf, I wish to
extend to you and through you to the Pakistan Muslim League-N Party, our
profound congratulations on your momentous victory. Your election to lead your great country and
its people is a clear testimony of confidence and trust that the people of
Pakistan have to your Pakistan Muslim League-N Party.
As you prepare to assume office in your
new mandate, I wish to assure, you of my personal commitment as well as that of
the Government of the United Republic of Tanzania, to continue to work closely
with you and your Government to further strengthen the excellent bilateral
relations that so happily exist between our two countries.
While wishing you a very successful
term and continued personal good health, please accept, Mr President, the
assurances of my highest consideration and esteem.
Issued by:
The Ministry of Foreign Affairs and International
Co-operation,
Dar es Salaam
9th September, 2013
Saturday, September 7, 2013
A Congratulatory Message to the Australian Prime Minister Elect
H.E. Jakaya Mrisho
Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Congratulatory
Message to the Australian Prime Minister Elect, Rt. Honourable Tony Abbott
(MP).
The message reads as
follows
“Rt. Honourable Tony Abbott (MP)
Prime Minister Elect,
Sidney,
AUSTRALIA.
I have received with great joy the news
of your election as the 28th Prime Minister of Australia.
On behalf of the Government and people
of the United Republic of Tanzania and, indeed, on my own behalf, I wish to
extend to you and through you to the Australian Liberal Party our profound
congratulations on your momentous victory.
Your coalitions' election to lead your great country and its people is a
clear testimony of confidence and trust that the people of Australia have to
your Party and its coalition partners.
As you prepare to assume office in your
new mandate, I wish to assure, you of my personal commitment as well as that of
the Government of the United Republic of Tanzania, to continue to work closely
with you and your Government to further strengthen the excellent bilateral
relations that so happily exist between our two countries.
While wishing you a very successful
term and continued personal good health, please accept the assurances of my
highest consideration and esteem.
Jakaya
Mrisho Kikwete
PRESIDENT
OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”
Issued
by:
The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es
Salaam.
7TH
SEPTEMBER, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)