Friday, September 13, 2013

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi mpya wa Italia nchini

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Dkt. Luigi Scotto, Balozi mpya wa Italia hapa nchini. hafla hiyo fupi ilifanyika IKULU, Dar es Salaam tarehe 13 Septemba, 2013.
 
Mhe. Balozi Scotto akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha huku Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Dora Msechu akishuhudia.
 
Balozi Scotto akisalimiana na Balozi Msechu.
 
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Scotto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho. Mwingine katika picha ni Afisa wa Ubalozi wa Italia hapa nchini aliyefuatana na Balozi huyo.
 
Mhe. Balozi Scotto akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili IKULU.
 
Mhe. Balozi Scotto akisikiliza wimbo wa Taifa lake  ukipigwa na Bendi ya Polisi (Brass Band) (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili IKULU. Kushoto kwa Balozi Scotto ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed M. Juma na kulia ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
 
Kikundi cha  Brass Band kikiwa kazini wakati wa mapokezi ya Balozi Scotto.

 
 
Picha na Reginald Philip Kisaka.
 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.