Tuesday, September 24, 2013

Mhe. Balozi Batilda Burian aongoza Watanzania kujitolea damu, mjini Nairobi


Mhe. Balozi Batilda S. Burian akishiriki katika zoezi la utolewaji wa damu pamoja na Watanzania wengine aliyoambatana nao, mapema leo mjini Nairobi.

Mhe. Balozi Batilda S. Burian akishiriki katika zoezi la utolewaji wa damu pamoja na Watanzania wengine aliyoambatana nao, mapema leo mjini Nairobi.




WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA

Mhe. Balozi Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi leo kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la Ugaidi lililotokea Tarhe 21 Septemba 2013 Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na Hospitali ya MP Shah.

Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoaa wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa  kwa risasi na magrunet katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.




Picha na maelezo kwa hisani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.