Thursday, September 26, 2013

Ujumbe kutoka Japan watembelea Wizara ya Mambo ya Nje


Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia akielezea maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Japan.  Balozi Kairuki alikutana mapema leo na Profesa Takahashi Motoki kutoka Taasisi ya Masomo ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kobe, nchini Japan.  Profesa Motoki na Ujumbe wake hupo nchini kutathmini malengo ya misaada inayotolewa na Serikali ya Japan kwa Tanzania. 

Mkutano ukiendelea.

Profesa Takahashi Motoki (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo.  

Balozi Kairuki (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalamu kutoka Japan, ikiongozwa na Profesa Takahashi Motoki kutoka Taasisi ya Masomo ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kobe, nchini Japan.


Picha na Reginald Phillip


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.